Natafuta machimbo ya Nafaka kanda ya Ziwa

Natafuta machimbo ya Nafaka kanda ya Ziwa

Mhesu

Member
Joined
Nov 20, 2025
Posts
5
Reaction score
3
Salam Wana jukwaa.

Mimi ni mfanyabiashara. Natafuta machimbo ya nafaka Kanda ya ziwa na viunga vyake.
Nataka nipate nafaka kutoka kwa wakulima moja kwa moja au wafanyabiashara ambao Bei zao ziko chini sana

Nafaka ninazohitaji ni;

1 Karanga
2 Maharage njano
3 Dengu
4 Kunde, na
5 Njugu mchanganyiko

Mikoa ambayo ningependa machimbo yake ni;

Mwanza
Shinyanga
Kagera (maharage njano
Mara
Kigoma (maharage njano)

Pia Dodoma kwa ajili ya karanga.

Kama wewe ni mkulima wa nafaka tajwa au unajua machimbo ya nafaka hizo katika mikoa tajwa karibu Sana pm

Asanteni sana
 
Mtafute huyu dada yuko mitandaoni

1773608134193.png
 
Karanga nenda mikoa ya Tabora na Katavi nilikuwa huko wiki iliyopita kabla sijarudi jijini gunia kilo 42 zenye maganda ilikuwa ni tsh 45,000/= hadi tsh 50,000/= na mahindi 110kg ni 50,000 hizo bei ni za wilaya ya Mpimbwe Katavi.

Hivi garama ya usafirishaji huwa ikoje mkuu Kama una uzoefu
 
Karanga nenda mikoa ya Tabora na Katavi nilikuwa huko wiki iliyopita kabla sijarudi jijini gunia kilo 42 zenye maganda ilikuwa ni tsh 45,000/= hadi tsh 50,000/= na mahindi 110kg ni 50,000 hizo bei ni za wilaya ya Mpimbwe Katavi.
Sahihi au aende wilya ya Tanganyika
 
Back
Top Bottom