Hapo kwanza huwezi pata laptop mpya kwa hio bei yenye hizo specs na pia used ni ngumi ila possible ukiwa mtu wa kufuatilia sana.
Ili laptop itoboe masaa 10+ inatakiwa iwe na processor zinazokula umeme kidogo, ram kama za simu ambazo zinatumia umeme mdogo, storage za ssd ama emmc ama ufs, Hdd inakula zaidi, na display hizi za kisasa zinazotumia chini ya watt.
Processor za bei rahisi zinazokula umeme kidogo ni hizi pentium na celeron silver hazitumii technology kama i3 na i5 zinakuwa ni dhaifu zaidi, laptop zenye pentium silver ama celeron zinatumia pia emmc badala ya ssd kusave cost. Mfano mzuri ni Acer Aspire one, nilinunua laki 4 kkoo inakaa na chaji masaa 17 offline na test ya laptopmag ni masaa 14 kwa wifi inamaana kwa modem unaweza pata masaa ya kutosha pia 7+.
Acer's 14-inch Cloudbook offers decent Windows 10 performance, a good keyboard and chart-topping battery life, all starting at just $199.
www.laptopmag.com
Ila nunua hizi laptop kama ukaaji chaji kwako ni muhimu kuliko kitu chochote sahahu fifa 19, sijui photoshop, kuedit video na kazi nyengine yoyote nzito.
Processor ambazo zimebalance perfomance na pia zinakaa sana na chaji ni core m Series aka Y series inaweza kuwa i3 ama i5 ama i7 lakini inaishiwa na Y kwa mbele. Hizi zinakuwa kwenye ultrabook zote za kisasa sema bei nazo ni ndefu sana nyingi ni dola 700 kupanda.
Option nyengine ambayo itabidi uende njia used kutafuta laptop ya bei rahisi na extended batyery. Kanunua lenovo Thinkpad series then inunulie 9 ama 6 cell replacement battery pia utatoboa masaa 10.
Mfano thinkpad x240 zimejaa kibao kkoo bei around laki 4, ama x230 bei around laki 3 chenji inayobakia unaenda kununua battery lake extended kubwa, sema inakuwa na kitako kikubwa ukipachika battery ya namna hii kama picha ya kulia inavyoonesha
X240/230 zinakaa na chaji masaa 20 kwa test ya laptopmag
The Lenovo ThinkPad X240 delivers amazing battery life, powerful performance and a durable design, making it the best business ultraportable yet.
www.laptopmag.com