Nilidhani labda umefeli kama mimi lakini nilipoona matokeo yako hayo uliyoyaweka hapo
Ngoja nikushauri...
Kurisiti ni kupoteza muda ukizingatia saivi ujanja wa elimu siyo kujaza ndani makaratasi (vyeti) bali kujaza hela ndani (ajira).
Kwa ufaulu wako huo tafuta chuo chochote piga upate mizizi ya hela kwanza (ajira) halafu ndo utaamua kurisiti huko mbeleni japo mara nyingi hela ikikolea mtu hawazii tena uanafunzi
Halafu kuna jambo lingine (sina uhakika wala uelewa zaidi) kwamba shule za private zinachukua watu hata combination isipobalansi basi kama wewe ni mpenda kusoma ni heri uende huko ili usogee fasta lakini siyo kurisiti
Mimi ninayekushauri hapa ni fom foo feliya tena arts, kuna kipindi nilipanga kurisiti lakini nikawaza wee nikaja kuwazua kwamba ni ujinga na kupoteza muda tu nikaona ni bora nikasome (wenyewe wanaita kuchukua) diploma kisha degree tu basi