Natafuta kazi, nina shahada ya Development Studies

Natafuta kazi, nina shahada ya Development Studies

Nyie ndo mlikuwa mnaambiwa someeni ualimu mnajishebedua hamuwezi kushika chaki sasa hivi mnautamani ualimu.

Mwambie mkuu,eti anauwezo wa kufundsha o&a level kweli?,aache kudanganya,hv fan ya ualmu ni fan ya majaribio?Kwann hakuusomea?
 
Habarini wanaJF, nahisi nitapata msaada mkubwa maana waajiri wapo wengi hapa.

Sasa wakubwa nimesoma Bachelor of Arts in Development Studies na cheti ninacho GPA ndogo sana ya 3.3 nisaidieni Tafadhali naombeni msaada kaka zangu na dada zangu.

Nina ujuzi wa computer na fani yangu naiweza vizuri hakika sibabaishi.

Asanteni.

Aisee inaonekana ajira ni issue sana sikuhizi

Pita HAPA dada kuna kazi nyingi tuu
 
Habari gani?

Pengine baba yangu angekuwa Mkubwa ningeshapata kazi, Leo nimeaona nine tena jf kuwaomba mameneja na Human resources woote wa jf wanitazame kwa jicho la huruma walau waniite kwenye ofisi zaidi shida wanipe nafasi ya kujitolea, wala sioni faida za kusoma tena km nilivyofikiri.

Lakini pia sijui mama alikuwa anaonaje chuo kukuu na alipoona nimekosea loan na sasa naenda diploma akasema kwa Mara ya kwanza, maana kabla sikuwahi soma private atanigharamia sasa nimeenda chuo nimelipa ada 2.4 mil. Direct costs LAKI tano na 70 bado chakula na kibaya zaidi ni kwamba hadi saaa nang'aa machoo tu kwenye familia, simlaumu mungu hata kidogo lakini may be aliona ambavyo angeumia kama angekuwa hai,akamchukua, najua naweza pata mahali pa kujitolea buree kabisa mradi wanipe nauli na lunch huku nikisubiri neema za mungu zinishukie nami nipate kazi km wengine, naombeni kwa wale member wa jf wenye nafasi kwenye maofisi mnisaidie Mimi ni mtoto masikini.

Please ukihitaji CV yangu niambie tu, naamini mungu atasaidia kupitia Uzi juu huenda nikipata chochote.

Nipo mwanza kwa kujitolea ninaweza NYAMAGANA na ILEMELA, LAKINI PIA KM NI KAZI FROM 6 MONTHS CONTRACT POPOTE TANZANIA WALAU MDOGO WENU NIPATE MTAJI WA KUTOKEA, SINA NAMNA NYINGINE,, ninesomea Bachelor of arts in development studies.

Kutoka chuo kikuu cha Dodoma.
 
Duh pole ndugu umesomea nini ndugu itasaidia zaidi kuwafungua hawa watu. Kama ni mtaalamu wa kilimo nahitaji mtaalamu wa kilimo nifanye naye kazi za kilimo cha umwagiliaji mikoa ya morogoro na pwani
 
Mkuu strong woman,
Jaribu Kujieleza Vizuri Ueleweke
Usoma Nini?
Ngazi Gani Ya Elimu?
Japo Umesema Uko Mwanza
Jiweke Wazi Hao Watoa Kazi Wasiwe Na Maswali Hapa Jf.

Kazi Iwe Ni Kwenda Kufanya Tu Hiyo Kazi Kwa Ataye Kuwa Tayari Kukusaidia Kwa Moyo
 
Last edited by a moderator:
Duh pole ndugu umesomea nini ndugu itasaidia zaidi kuwafungua hawa watu. Kama ni mtaalamu wa kilimo nahitaji mtaalamu wa kilimo nifanye naye kazi za kilimo cha umwagiliaji mikoa ya morogoro na pwani
Arts in development studies bdani take kuna kilimo naomba nisaidieni jamani
 
Mkuu Strong Woman
Jaribu Kujieleza Vizuri Ueleweke
Usoma Nini?
Ngazi Gani Ya Elimu?
Japo Umesema Uko Mwanza
Jiweke Wazi Hao Watoa Kazi Wasiwe Na Maswali Hapa Jf.

Kazi Iwe Ni Kwenda Kufanya Tu Hiyo Kazi Kwa Ataye Kuwa Tayari Kukusaidia Kwa Moyo
Arts in development studies ngazi ya degree..
 
don't worry, utapata tu, kuwa na imani, jitihada zako zitazaa matunda someday, usikate tamaa na punguzA stress, mama yako anakuombea and you have the bright future, believe me
 
arts in development studies bdani take kuna kilimo naomba nisaidieni jamani
nakushauri ujieleze vya kutosha uweke particulars zote za muhimu angalau uweze kuuzika vizuri ili waajiri wasisumbuke kutambua potential uliyonayo. Punguza pia kulalamika.
Taaluma yako ni potential tosha sana kujiajili,
unafahamu kitu kinachoitwa social entrepreneurship?
Usifikirie sana ajira za kuwekwa kwenye ofisi za watu jaribu kuwa diverse kimawazo kila kitu kitakwenda vizuri tu
but kama umejitosa kwenye ajira fanyia kazi hayo yatakusaidia
 
Ajira za utumishi uombe mkuu usiache ndio watoto wa masikini tunapokimbilia
 
Back
Top Bottom