Pole sana kiongozi nimesoma vizuri ujumbe wako, na pengine sio wako tu ni wa vijana waliowengi hapa kwetu Tanzania ni wengi sana sana sana wako katika hali kama yako, jana tu nimekutana mwingine huyu sasa ni wa kiwango cha diploma. Mimi sio mtoa kazi na wala sina kazi lakini maneno haya nadhani yatakusaidia,
1. Wewe umesema umesoma Development studies, nina imani kwa ngazi ya bachelor bado haukuwa na specialisation, lakini bado sio tatizo, fanya ukae ujitathimini nini hasa katika development studies unakiona shida hapo ulipo Mwanza na Tanzania kwa ujumla,
2. Fikiri kwa umakini kabisa ni nini cha tofauti unaweza kufanya pengine bila pesa nyingi mfano naweza kutembea kwa kulipa nauli ukielimisha wana Mwanza kuhusu raslimali samaki na masoko yake duniani na Tanzania, pengine ukaomba hata shule ya msingi au sekondari ufundishe somo la maendeleo hata kwa kujitolea tu, Ngoja nikupe experience yangu mwenyewe, mimi nilipomaliza form six tu mwanza Nsumba secondary nirirudi nyumbani tabora, nikamwambia rafiki yangu tusikae nyumbani twende tukaombe darasa shule ya msingi tuanze kufundisha tuisheni, tulifanya hivyo na tukapata wanafunzi na majina yetu yaka kuwa kweli, nilivyomaliza chuo kikuu UDSM nilirudi nyumbani tabora, nikasema siwezi kukaa bila kazi, nilienda kujiunga na chama cha siasa kimoja wapo kama mtaalam kuwasaidia katika mambo ya kiutawala, nilifanya nao kazi kwa muda, lakini halikuwa lengo langu kuu, ndani ya muda mfupi nilimwambia rafiki yangu tukatafute kazi sehemu nyinine kwa kujitolea, nilikwenda kujitolea shule ya kata ya sekondali nikawa nalipwa nauli tu, Muda mfupi nikapata shule nyingine kubwa nikafundisha kwa muda wa miezi sita tu, nikaondoka na kurudi chuo kikuu, wakati nikiwa chuo kikuu nikatafuta NGO moja nikawa naudhuria seminar zao baadae kidogo nakatafuta NGOs kama tatu nikiomba nafasi ya kujitolea tu sikutaka nauli wala posho kumbuka wakati huo mimi ni mwanafunzi. na mwishowe nilipata kazi. Usitegemee kutoka kwa muudo mmoja wa kuomboa kazi kwa kutuma CV na vyeti kwa mabosi hawa.
3. jaribu kufanya kazi za kiushauri kama vile kuwashauri watu kuhusu uandishi wa miradi, kazi ambayo mpaka sasa naendelea nayo, na inaniingizia kipato japo sio kikubwa.
4. kunafursa hii lakini bado hatujaitumia jaribu kuangalia unaweza kufanya nini haswa na mifuko ya rambo, katika majiji yetu, unajua kwamba mifuko hii inachafua mazingira kwa asilimia kubwa lakini kuna vijana wanweza kabisa kusuka vikapu vya mikeka ambavyo vinaweza kuwa mbadala wa mifuko ya rambo, ukiliweka vizuri hili ukalishare na mamlaka zinazo husika unaweza kufaulu, usiwemwoga wa kuziendea mamlaka, kwenda kwa afisa maendeleo ya jamii, nenda kwa mkuu wa wilaya, nenda kwa mkuu wa mkoa, ongea nao nenda kwa wadau wa mazingira ongea nao waelezee hilo. Mimi ukiwa huko tiyari nitakusaidia kudevelop proposal ili tuwaombe wenye hela tuweze kufanya hilo.
Nakutakia harakati njema kiongozi utafutaji kazi ni kazi pia na ni harakati.