Natafuta karanga/ndizi

Black Mann

Senior Member
Jun 30, 2020
140
209
Habari ndugu zangu,

Naomba kwa anayejua mkoa naoweza kupata karanga nzuri zile kubwa kubwa kidogo, sio hizi ndogo ndogo (wakulima / wauzaji wanajua)

Pia, naomba kwa mtu anayeweza kujua zinakopatikana ndizi za kuiva zile ndogo ndogo.

Karanga nataka zije Dar!! naombeni bei elekezi kwa kilo.
 
Habari ndugu zangu,

Naomba kwa anayejua mkoa naoweza kupata karanga nzuri zile kubwa kubwa kidogo, sio hizi ndogo ndogo (wakulima / wauzaji wanajua)

Pia, naomba kwa mtu anayeweza kujua zinakopatikana ndizi za kuiva zile ndogo ndogo

Karanga nataka zije dar!! naombeni bei elekezi kwa kilo

Karanga na ndizi za uhalisia au za tafsida???.

Mfano unaposema "Nzi wa kijani" kwa tafsida inajulikana ni Chama fulani kikongwe cha siasa.
 
Hasara za kukomenti usingizini hizi.

Jibu lilikuwa litoke kwa mleta mada kwamba; ni karanga na ndizi halisi.

Wewe hujasikia akina dada wakisema; hawajazoea wao ni sungura hawajazoea maharage wamezoea karoti.--- hiyo ni tafsida.

Nenda kajifunze lugha.
 
Kwan hauwezi kusoma hata uzi upo jukwaa lipi? Nshafahamu sasa kumbe una shida mahali,nilijua ni maruweruwe ya usingizi kumbe sio.
 
Karanga za aina hiyo nenda Tabora na eneo la Inyonga wilaya ya Mlele utakusanya mpaka utapike

Za maganda kilo @ 400/= na ukimenya debe linatoa kilo 7
 
Similar Discussions

1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom