MwanaHaki
R I P
- Oct 17, 2006
- 2,401
- 710
Samsung Galaxy Pocket S-GT5300 kama simu zote za Galaxy Series ni simu ambayo iliingizwa hapa nchini kwa mbwembwe zote. Lakini jambo ambalo Samsung, kampuni inayozitengeneza, haikumwambia mteja ni kwamba Pocket ilikuwa na kasoro nyingi za kiufundi.
Kwa mfano, simu hii ina memory ndogo kiasi kwamba bila kuweka memory card, ufanisi wake unakuwa hafifu. Pia, inamlazimisha mtumiaji kufanya Software Update lakini kwa njia ya WiFi pekee. Lakini hili la mwisho pengine ndio baya zaidi. Baada ya matumizi ya mwaka mmoja, betri yake inakuwa imechoka kabisa kiasi kwamba haiwezekani simu ikamaliza saa 8 kabla ya kuzimika.
Ufumbuzi wa tatizo hili la mwisho ni kupata heavy duty battery ya kuaminika ambayo haijatengenezwa na Samsung.
Tafadhalini wadau nielekezeni wapi naweza kuipata betri hii na kwa gharama gani.
Asanteni.