Kusena
JF-Expert Member
- Aug 25, 2020
- 282
- 174
Habari zenu wapendwa, Poleni kwa mihangaiko ya kila siku. Kwa majina naitwa Kusena, mwanaume mwenye umri wa miaka 26, elimu yangu ni stashahada ya Maendeleo ya jamii. Mimi ni mzaliwa wa mkoa wa Pwani, halmashauri ya wilaya ya Chalinze, na kwa sasa ninaishi katika mkoa wa Mbeya.
Ndugu zanguni, naomba kwa moyo wa dhati msaada wa kupata ajira yoyote halali. Nina nguvu, bidii, na dhamira ya kujifunza ili niweze kutoa matokeo na mchango chanya mahali nitakapopata fursa ya kazi. Iwe ni ofisini, kiwandani, ujenzi, au kazi nyingine halali niko tayari kujituma kwa moyo wote.
Kwa kuwa sina kifaa cha smartphone wala kompyuta ya kufuatilia majibu mtandaoni, naomba tuwasiliane kwa njia ya simu ya kawaida kupitia namba zifuatazo:
📞 TTCL: 0733 323 349 📞 Airtel Tz: 0783 561 749
Samahani sana kwa usumbufu. Ninathamini sana msaada wowote kutoka kwenu. Mungu awabariki wote.
compyuta hii nimeiazima kwa ajili ya kutuma hili tangazo tu hivyo naomba sana tuwasiliane kwa hizo namba.