Natafuta fundi mwashi mzoefu

Natafuta fundi mwashi mzoefu

Nyani Ngabu

Platinum Member
Joined
May 15, 2006
Posts
97,988
Reaction score
142,393
Habari wanaJF,

Kama jina la mada linavyosomeka, mimi natafuta fundi mwashi mzoefu hususan katika mambo ya ukarabati wa nyumba.

Kwa vile JF ni jukwaa lenye mchanganyiko wa kila aina ya watu wenye fani anuai basi ni matumaini yangu kuwa watakuwepo watu ambao wataweza kunisaidia kwenye hii shida yangu.

Hivyo basi, kama unamjua fundi yeyote ambaye ni mwaminifu, mwenye tajiriba, na ustadi mkubwa, au kama wewe mwenyewe ni fundi mwenye hizo sifa, basi naomba uwasiliane nami hapahapa kupitia njia ya jumbe za faragha.

Natanguliza shukurani zangu.

Wenu katika gurudumu la maendeleo.

NN.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom