Natafuta Binti/Mwanamke wa Kuoa

Benylin

Member
Feb 9, 2017
44
26
Habari za mda huu wana JF?

Najitokeza hapa nikiwa na dhamira ya kutafuta rafiki wa kike/mpenzi, ambaye tutaoana na kuwa mke na mume.

Mimi ni mwajiriwa wa serikali, elimu yangu ni ya Chuo kikuu. Umri miaka 26. Mkristo, na nina mcha Mungu.

Sifa za mwanamke ninaye mtafuta, awe na umri usio zidi miaka 25, awe Mkristo na anae mcha Mungu. Awe na elimu ya kidato cha NNE na kuendelea. Akiwa ndani ya kanda ya ziwa, itapendeza zaidi kwan itakua rahisi kuonana naye kwa lengo la kufahamiana, Mimi nipo Mwanza kikazi.

Kwa binti yeyote mwenye sifa hizo, na mwenye hitaji kama langu la kutafuta mwenza wa maisha, ani PM ili tuzungumze zaidi.
 
Ebu tupe hali ya uchumi wako mbali na elimu uliyo nayo? maana kuna vigezo vya kuanzisha familia bora na sio bora familia.
Ni kwel kabisa unachokisema mkuu kuwa kuna vigezo vingi katika kuanzisha familia, mengine tutayazungumza PM kwa aliye na nia na uhitaji wa mwenza kama Mimi. Aje PM tutaongeza na kufahamiana zaidi
 
Dah ,ila sitaki kukutendea baya kaka kila la kheri katika utafutaji "nilitaka nikupe msichana mmoja ila atakusumbua sana ameolewa mara tatu kaachika na ana tabia mbaya kweli ila akiwa mpya kwako utasema malaika huyu alikuwa wapi muda wote huo"
Duh, Mara tatu huyo CV yake mbona inatisha sasa. Au hadi wafike saba kama yule aliyeulizwa Yesu na Mafarisayo, kuwa wakati wa ufufuo atakua mke wa nani
 
Habari za mda huu wana JF?
Najitokeza hapa nikiwa na dhamila ya kutafuta rafiki wa kike/mpenzi, ambaye tutaoana na kuwa mke na Mme.

Mimi ni Mwajiriwa wa serikali, elimu yangu ni ya Chuo kikuu. Umri miaka 26. Mkristo, na nina mcha Mungu.

Sifa za mwanamke ninaye mtafuta, awe na umri usio zidi miaka 25, awe Mkristo na anae mcha Mungu. Awe na elimu ya kidato cha NNE na kuendelea. Akiwa ndani ya kanda ya ziwa, itapendeza zaidi kwan itakua rahisi kuonana naye kwa lengo la kufahamiana, Mimi nipo Mwanza kikazi.

Kwa binti yeyote mwenye sifa hizo, na mwenye hitaji kama langu la kutafuta mwenza wa maisha, ani PM ili tuzungumze zaidi.
Safi sana mkuu, Muombe Mungu, atakupa Mke mwema, iwe kutoka hapa JF, au Mtaani kwako, au kazini kwako, au kwenye any social network. Binafsi Nakutakia kila lililo heri
 
Kanisani, kazini, kwenye usafiri, mtaani huko kote umeshindwa kukutana na bint? Kama una gari jaribu kupanda dala dala kwa mwezi mmoja kwenda na kurudi kazini unaweza kukutana na mwenza huko.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom