Mpenzi hivi umewaza kwamba what if huyo mtoto utakayemzaa ndo akawa mtoto wako wa pekee? What if ukiolewa baadaye afu ukashindwa kuzaa? Utarudi kumtafuta mtoto uliyemgawa? Utamwambia nini huyo mtoto hadi akuelewe sababu ya wewe kumgawa? Unadhani mtoto atakuwa na upendo na wewe kama mama as long as amekulia mikononi mwa mama mwingine ambaye yeye anaamini ni mama yake mzazi? Chochote kibaya kikitokea kwa huyo mtoto ndani ya hiyo familia, mwanao atakulaumu milele
Please my dear, kama umeweza kulea mimba hadi muda huu, basi na mwanao utamlea tu. Mungu ni wa ajabu, atakuinulia watu wa kukusaidia hadi utashangaa. Mungu ni muaminifu, atakupigania tu. Usitupe baraka yako (mtoto wako)