Natafuta ajira au kazi yoyote maalum ya kuingiza kipato

Sukari Mine

New Member
Dec 9, 2020
4
14
Habari zenu waheshimiwa!

Binafsi ni muhitimu wa ngazi ya shahada ya kwanza katika nyanja ya uhandisi migodi na uchenjuaji.

Ninaomba msaada kwa yeyote mwenye connection ya kazi nyanja yoyote anisaidie.

Nina uzoefu katika usimamiaji wa crusher na plant kama production supervisor katika kiwanda cha cement.

Nina uzoefu wa usimamizi wa ujenzi wa majengo kama site foreman.

Pia nina uwezo wa kufanya kazi za ujenzi kama skimming na kupiga rangi,kuweka tiles, kufunga ceiling boards na umeme wa majumbani ambavyo nimejifunzia mtaani.

Nina uzoefu wa kufundisha masomo ya sayansi kama Chemistry, Physics na Mathematics,katika mashule na tuition.

Uzoefu mwingine nilionao ni katika nyanja ya mauzo na masoko.

Sifa zingine za kiuongozi mm ni mjumbe wa kamati ya Chama Cha Mapinduzi ngazi ya tawi .Msimamizi wa uchaguzi ngazi ya kata 2020.

Ujuzi wa Softwares kama: Ms Word, Excel, Power Point, Scada ,AutoCAD n.k.

Naomba kama kuna kazi yoyote ya mda au ya kudumu ambayo inaendani na wasifu nilioweka hapo juu unikumbuke katika nyakati zako.

Nakaribisha maoni na ushauri .

Asanteni sana ,Mungu awabariki
 
Kama ukikosa na Kama unatafuta ajira yeyote na upo teyari kulinda....ebu njoo gardaword....ila hakikisha wewe ni mrefu...uwe na cheti cha kuzaliwa na kitambulisho cha nida...bila kusahau TIN...Ofisi zipo mikocheni kwa mwinyi mshahala kimo cha chini ni 250k
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom