Nasubiri kwa hamu sana maamuzi ya JWTZ dhidi ya ' Twiti ' ya Zitto Kabwe kwa kuvitaja vifaa vyao vya Siri Ngerengere

Zitto Kabwe ni nani mpaka aseme kwamba ana uhakika kuwa Jeshi la Wanachi la Tanzania ( JWTZ ) lina Vifaa ' Maalum ' vya Kijeshi vya Uokoaji ila anashangaa kuona halijahusishwa kikamilifu katika kuvitumia ili kuweza Kuokoa maisha ya Watanzania wenzetu katika Ajali ya MV Nyerere.

Ninavyojua ni kwamba Kutaja hovyo tena hadharani Vifaa vya Kijeshi ni sawa sawa na Kuuza Siri kwa Maadui wa Tanzania na kibaya zaidi Zitto Kabwe mwenyewe katika ' Twiti ' yake amekiri kabisa kwamba anajua na ana uhakika kuwa JWTZ wana hivyo vifaa katika Kambi yao tena ' Nyeti ' kabisa ya Ngerengere Mkoani Morogoro.

Sasa kama Zitto Kabwe anadhani kuwa JWTZ ni sawa sawa na Cyprian Musiba Kazi anayo na kama vile nawaona sasa JWTZ jinsi wanavyojipanga ili kuweza Kumfundisha adabu kwa kuwa na ' Kiherehere ' cha hadi kutaja Vifaa vyao Kinyume kabisa na Maadili na Utaratibu wao.

Kazi ipo hakyanani!

Nawasilisha.
Kwani yalikua ni maandamano mpaka hao aliowataja zitto waende kutumia hivyo vifaa?
 
Sasa Jeshi linaficha vifaa vya uokoji...ati ni suala 'nyeti'

Zitto kahoji na hajatoa siri yoyote, hakuna siri kwa vifaa vya uokoaji

Upuuus
 
Mbona mnapenda kutufunza kuwaogopa usalama na wanajeshi ni kama wamebeba wachawi wakati ni wanachi wa kawaida
Kazi yao kubwa inajulikana, Zitto kahoji kwa sababu anatambua kuwa vifaa vipo,
 
Vifaa ni Siri? Mbona mataifa makubwa yanaona fahari kujulikana Kwa silaha Zao? Wakifanya ugunduzi wa makombora wanatoa taarifa sembuse kutaja vifaa vya uokozi? Kuwa serious kidogo mkuu!
 
Back
Top Bottom