Nasubiri kwa hamu sana maamuzi ya JWTZ dhidi ya ' Twiti ' ya Zitto Kabwe kwa kuvitaja vifaa vyao vya Siri Ngerengere

JWTZ sio wale mgambo wanaopiga watu kisa Usafi..JWTZ ni nidhamu,pili mtu akisema ana uhakika alafu ni Mbunge haimaanishi aliona vifaa labda alipokuwa kwenye PAC anafahamu fedha za kutosha zinapelekwa JWTZ kwa ajili ya vifaa vya uokoaji..ni swala la serikali kuliomba jeshi litoe msaada kwa RAIA wa JMT
 
Vifaa vya Uokoaji wa Majini au Nchi Kavu? kama ni Majini nina uhakika haviwezi kuwepo Ngerengere labda kama angetaja kambi ya Jeshi iliyo karibu na Ziwani au Baharini!
 
Pengine alikuwepo bungeni wakati bunge linatoa budget ya kuvinunua hivo vifaa.

Labda ana ushahidi juu ya kile alichokiongea.



Article 13 (6) (B) of the Constitution (Katiba ya Nchi) Presumption Of Innocence "Everyone is pressumed to be innocent, until proved guilty" - (Kila mtu hana hatia ya kosa la jinai, mpaka itakapo thibitisha mahakama ya kua anahatia)
 
Nadhani Zito alimaanisha kuwa Ngerengere kuna, Vifaa yaani Makomandoo wa kutosha kuokoa ndugu zetu fasta bila kuchoka katika mazingira yoyote.

Madhani ndio maana yake.
Tusipende sana kukuza vitu vidogo ili tu kujenga mtafaruku . Hakuna siri yoyote iliyovuja kokote.
Jeshi letu lipo imara haliwezi kupata tishio kwa kauli nyepesi kama hiyo ya Zito tena ya kulisifu.

Na pia karne hii hakuna adui tena anayehangaika na silaha mdogo ndogo .
Jeshi duniani lipo Magharibu ,yaani Marekani na Washirika wake na Mashariki ,yaani China ,Urusi na Korea ya Kaskazini. Hao ndio matishio ya usalama wa dunia. Hao wengine ni njaa tu hakuna mtu wa kuingia gharama kuvamia nchi nyingine wakati uchumi wake ni tia maji tia maji.

Majeshi mengine duniani hasa kwenye nchi changa ni ya kusimamia uchaguzi,kusindikiza masanduku ya kura tu na kurusharusha kichura raia wao ambao ni walipa kodi kichura!Wasubiri wanasiasa wanasemaje.
Acha dharau mjomba hapa sio pangoni
 
Watampotezea kwasababu wanajua aidha anatafuta kiki au anafanya hivyo kulipigania tumbo lake.
 
Katika nchi za dunia ya tatu na masikini kama ya kwetu huwezi kudai unamiliki vifaa vya siri labda kama una maana ni vya siri kwa wananchi wako ambao unatumia kodi zao kuvinunua. Wenye vifaa vya siri ni wale wanaovitengeneza, si sisi makapuku tunaovinunua vikiwa tayari vimetengezwa na watu wa mataifa mengine.

Hivyo ni ujinga kuviita vya siri, siri kwa nani? Nani huyo tuliandika naye mkataba atutengenezeee sisi tu vifaa hivyo na iwe siri yetu tu? Halafu vifaa vyenyewe ni vya kuokoa wananchi wanapopatwa na majanga. Hizi mada za kijingajinga sasa zinazidi humu JF na sasa ni muda muafaka wa kuzitafutia dawa.
 
Back
Top Bottom