Ni Vipi Vifaa Vya Mafunzo Kwa Kozi Za Afya? Dkt. Adinan anashauri uwe na vifaa hivi

Dr Adinan

Member
Jul 11, 2021
14
22
Hongera siwezi kuiacha. Umeefanya kazi kubwa mpaka kuchaguliwa kusomea kozi za afya. Kozi ya afya yeyote ni nzuri na itakuwezesha kufanya vitu vingi hapa maishani ukiacha ukweli kwamba fani za afya bado zina HESHIMA kubwa mbele ya jamii na kuhitajika.

Baada ya hongera, nina habari nzuri kwako! Habari hii itaweza kukusaidia kusoma kwa raha kwa kuwa utaweza kupata vifaatiba bora muhimu kwa masomo yako. Habari hii inalengo la kuua ndege watatu kwa jiwe moja. Nafahamu ushazoea ndege wawili.

Lengo la kwanza ni kukusaidia kuwa mtaalamu bora wa afya, lengo la pili ni kukuepusha kutapeliwa unaponunua vifaa na lengo la tatu ni kukuwezesha kuchagua kwa uhakika vifaa vyako vya mafunzo hata kama una upungufu. wa pesa kwa sasa.

Kuwa bora katika kitu chochote kina uhusiano wa moja kwa moja na utendeaji wa kazi ile, kufanya mazoezi...fani za afya ni kozi zinazofundishwa kwa vitendo. Hivyo unahitaji nawe kujiweka tayari kwa kuweza kufanya vitendo hivyo. Practice.

Hapa namzungumzia kumpima mgonjwa. Itakubidi uwe unafanya mazoezi mwenyewe kwa kujituma haswa muda wa ziada. HIvyo unahitaji kuwa na vifaa vyako vya mafunzo.

Lakini uwe na vifaa vipi vya mafunzo? Kabla ya kukuambia utumie aina gani ya vipimo, ningependa kwanza kuisistiza ubora wa vipimo. Kumbuka majibu unayoyapata kwenye vipimo ndivyo unavyojifunza. Kwamfano, utajifunza aina za sauti ya mapafu na moyo kama tuu stethoscope yako itakuwa inadaka sauti vile vile ilivyotolewa na viungo hivi bila kubadilisha ubora. Hivyo sisitiza sana ubora.

Kitu cha pili cha msingi ni aina. Uwe na aina gani ya vifaa?

Aina za Vifaa Vya Mafunzo Na Matumizi Yake

Vifaa utakavyohitaji ni kwa ajili ya kumpa huduma mteja (Mgonjwa) ikiwamo kumfanyia vipimo kadhaa (physical examination). Vipimo hivi ni kwa mifumo mbalimbali ya binadamu.

  1. ๐Š๐š๐ญ๐ข๐ค๐š ๐ฆ๐Ÿ๐ฎ๐ฆ๐จ ๐ฐ๐š ๐๐š๐ฆ๐ฎ: BP Machine, Stethoscope & Torniquet โ€“ utampima mgonjwa presha ya damu (BP Machine), na mwenendo wa moyo (Stethoscope). Kwasababu utakuwa unachukuwa sampuli za damu kwa ajili ya uchunguzi, utahitaji torniquet.
  2. ๐Œ๐Ÿ๐ฎ๐ฆ๐จ ๐ฐ๐š ๐ก๐ž๐ฐ๐š (๐ซ๐ž๐ฌ๐ฉ๐ข๐ซ๐š๐ญ๐จ๐ซ๐ฒ ๐ฌ๐ฒ๐ฌ๐ญ๐ž๐ฆ)-Stethoscope & Pulse Oximeter: utampima mgonjwa mapafu (kwa kusikiliza hewa inavyoingia)- (Stethoscope), kiwango cha oxygen kwenye mwili (Pulse oximeter).
  3. ๐Œ๐ข๐ฌ๐ก๐ข๐ฉ๐š ๐ฒ๐š ๐Ÿ๐š๐ก๐š๐ฆ๐ฎ (๐ง๐ž๐ฎ๐ซ๐จ๐ฅ๐จ๐ ๐ข๐œ๐š๐ฅ ๐ฌ๐ฒ๐ฌ๐ญ๐ž๐ฆ)- Reflex/Patella hammer, Monofilament, Tuning fork, Pen torch: utimilifu wa mishipa ya fahamu kwa kupima kama mteja wako anahisi (Monofilament), anaona (Snellen chart), anasikia (Tuning fork) ikiwemo kuitikia vichocheo (Patella hammer). Pia namna ambavyo jicho linaitikia linapomulikwa (pen torch)
  4. ๐•๐ข๐Ÿ๐š๐š ๐ค๐ฎ๐ฆ๐ฎ๐ก๐ฎ๐๐ฎ๐ฆ๐ข๐š ๐ฆ๐ฃ๐š๐ฆ๐ณ๐ข๐ญ๐จ โ€“ Gestation wheel, Tape measure, Fetoscope: Utahitaji kupima umri wa ujauzito pamoja na kuweza kukadiria tarehe ya kujifungua (Gestation wheel & Tape measure). Na kama mtoto kwenye kizazi amekuwa, unaweza kusikiliza mapigo ya moyo ya mtoto (Fetoscope).
  5. ๐•๐ข๐Ÿ๐š๐š ๐ค๐ฐ๐š ๐š๐ฃ๐ข๐ฅ๐ข ๐ฒ๐š ๐ฎ๐œ๐ก๐ฎ๐ง๐ ๐ฎ๐ณ๐ข ๐ฐ๐š ๐ฆ๐š๐ฌ๐ข๐ค๐ข๐จ, ๐ฉ๐ฎ๐š ๐ง๐š ๐ค๐จ๐จโ€“ Otoscope: Utatumia otoscope kuchunguza sikio.
  6. ๐•๐ข๐Ÿ๐š๐š ๐ค๐ข๐ง๐ ๐š-Theatre goggles: Tukumbuke kwamba wewe utafanya kazi kama mtoa huduma wa afya, ispokuwa tu ni mwanafunzi. Si tu utashiriki kwenye majadiliano ya kitabibu ispokuwa utahudhuria na kusaidia upasuaji na kuzalisha. Utahitaji vifaa ambavyo vitakuzuia na hatari ya maambukizi ya magonjwa mbalimbali kutokana na majimaji / damu kukurukia na kuingia machoni (theatre goggles). Kulingana na kozi, utahitaji medical coat (mfano kozi za medicine) au apron (uuguzi).
  7. ๐•๐ข๐Ÿ๐š๐š ๐ฏ๐ข๐ง๐ ๐ข๐ง๐ž-Tape measure, MAUC Tape: vya kupima urefu, upana na mzunguko kwa mfano wa uvimbe (tape measure). Na wakati unataka kuchunguza hali ya lishe ya mtoto mdogo, utahitaji MUAC tape.
Nimeviainisha vifaa hivi hapa chini. Hatahivyo, kuna vifaa vingine ambavyo huwa maalumu kwa kozi husika.
Vifaa hivi nimeviweka katika kozi husika. Mfano Goniometer hutumiwa na wanafunzi wanaosomea fani ya physiotherapy.

Siwezi Kununua Vifaa Vyote Kwa Wakati Mmoja: Je, Nianze na Vifaa Vipi?​

Hili swali ni MUHIMU kujiuliza kwa kuwa wakati mwenignie tunapata changamoto za kifedha hivyo kutokuweza kununua vifaa vyote kwa pamoja.

Majibu ya hili swali yako ya aina mbili, lakini kama swali ni je vifaa gani naweza kuanza navyo na nikafanya mafunzo kwa ufaninisi

Nitakujibu kama ifuatavyo. Kwanza inahitaji ufahamu wa ratiba ya chuo chako au kundi lako kama mmegawanywa kwenye makundi. Kwasababu vifaa vingine huitajika zaidi katika idara fulani.

Licha kuwa navyo vyote ni muhimu zaidi, lakini ikibidi, kwa uzoefu wangu, unaweza kuanza na vifaa vipi bila kuathiri mafunzo yako.Ukiwa na vifaa saba (7) unaweza kufanya vizuri.

Vifaa hivi ni
  1. BP Machine;
  2. Stethoscope;
  3. Thermometer;
  4. Tape measure;
  5. Theatre goggles;
  6. Patella hammer
  7. Pen torch

Kama kawaida nitafurahi ukinipatia maoni yako. Ni rafiki yako,
Dr. Adinan J.
CEO AFYATech
 
Back
Top Bottom