Nassari: Mungu aibariki Tanzania!

Nassari: Mungu aibariki Tanzania!

Make it, Bring the changes Nassari; lets experience the difference.
 
Kucheka sio dalili ya wema, kama kweli mtu unaichukia harufu ya choo kwa nini ung'ang'anie chooni,ni dhahir kuwa ccm hawafai kwa lolote,
so huyu jamaa ni mnafiki na hafai kabisa na magamba wenzake,
 
William najua uwezo wa kuwa Mbunge unao,ila ninavyojua ccm itakupa Ubunge si kwa uwezo wako kama mpambanaji bali kwa ajili ya kupata mtetezi huku JF na kuwasaidia kuwashawishi vijana kuipenda ccm.Kwa maoni yangu ccm imechelewa sana na tena sana ila kazi unayo kaka kwa maana ulaji utapata ila heshima ya sisi vijana kama mpambanaji hiyo sahau kaka. nakutakia ulaji mwema huku ccm chama cha mafisadi hahahhahhahhhaaaaaaa .hongera
 
Mie nipo CCM ila ushindi wa nassari ni jambo jema kwa vijana na wapenda maendeleo wa nchi hii.
wakati wa uchaguzi ni vyema kumchagua CDM kijana kuliko CCM mwenzangu mzee.
Wakati wa vijana ni sasa.
OTIS
 
Tuwape vijana nafasi. Sijaona vijana wakidai utaifa wao wa leo. Naona wazee ndio taifa la leo: Angalia Kamati ya Katiba, Wataka Urais, Watunga sera wengi, nk. Kijana akijitokeza tu anasakamwa!

Mkuu kweli vijana wapewe nafasi za uongozi. Vunja mifupa wakati meno bado ipo. Lakini vijana wasipewe tuu nafasi hizo kwa sababu eti ni vijana. Wapewe nafasi kwa sababu wana uwezo wa kufanya yale wanayotaka kuifanyia jamii. Vingenevyo, itakuwa kama viti maalumu vya ubunge kwa wanawake.

Sasa hivi ukiangalia vijana wengi wameanza kujitumbukiza kwenye siasa kitu ambacho ni kizuri. Lakini wengi hawa vijana hawana ufahamu mpana, utashi wa kujifunza, usikivu, unyenyekevu, ari ya kujituma, uchapa kazi hodari na mengine mengi. Wengi wanajitumbukiza kwenye siasa kwa sababu inaonekana ni rahisi kutimiza haja zao binafsi. Wengine wanajitumbikisa kwenye siasa kupitia migongo ya wazazi wao ambao nao walikuwa wanasiasa.

Lakini dhahiri ya uongozi si ujana tuu. Uongozi ni mkusanyiko wa mambo mengi yakiwemo uwezo wa kuongoza, kipaji na uadilifu, nk. Haya yote yanahitajika na ni muhimu sana kwa mtu yeyote anayetaka kuongoza wengine whether kijana or not.
 
Tukiwa na tofauti ya kimawazo na watu tusitukane familia na watu ambao hawahusiki katika mijadala.Tujifunze utu na heshima kwa familia za watu

Ben,
Sasa kama hizo familia zimekuwa ndizo chanzo cha umaskini wetu tufanyeje? Ben uwe unafikiria vizuri. Huyu Williama Malecela anatumia mgongo wa Nassari kutafuta kura za CHADEMA wakati kila siku amekuwa akimtukana Mbowe na Slaa hapa JF alafu leo anaanza kusifu kazi zao za kukuza vijana na kuwaingiza Bungeni. This is BOGUS IDEA. Lazima tujibu mashambulizi. Funguka!

 
- Wameniomba CV kwanza na wengine wote wagombea, ninawaheshimu sana CDM kama ninavyoheshimu CCM, siamini CDM wana utaratibu wa kutoa kura kwa kupitia mitandao!


William.

Kama umeombwa CV na CDM hesabu umeshaliwa. Hatupigii kura Division IV! Wewe kwanza umekuwa ukimtukana Mbowa na Slaa humu JF mara kadhaa kwa ajili ya kutetea magamba. Leo unaanza kujibaraguza kupitia kwa Nassari. Foolish!

 
Malecela mawazo yako yako kiukombozi lakini uko katika chama kinachoendeleza ukoloni mamboleo katika nchi ya watanganyika. Kama kweli una nia ya dhati ya kuwasaidia watu wako huko uliko hakukufai hata kidogo hamia Chadema ndoto zako zitatimia ama sivyo utakluwa unafanya usanii. Usiogope kuondoka kwa magamba kwa sababu baba yako ni gamba, wewe hutakuwa wa kwanza kufanya hivyo, amka kijana hujachelewa!

Hii ndio hoja ya msingi. Yeye kama anataka kweli kuikomboa nchi aingie kwenye jeshi letu la ukombozi la CDM. Siyo anajiita mpiganaji wakati yupo ndani ya jeshi la adui.
 
Ben,
Sasa kama hizo familia zimekuwa ndizo chanzo cha umaskini wetu tufanyeje? Ben uwe unafikiria vizuri. Huyu Williama Malecela anatumia mgongo wa Nassari kutafuta kura za CHADEMA wakati kila siku amekuwa akimtukana Mbowe na Slaa hapa JF alafu leo anaanza kusifu kazi yao ya kukuza vijana na kuwaingiza Bungeni. This is BOGUS IDEA. Lazima tujibu mashambulizi. Funguka!


Hata mie nimeshangaa sana. Ni huyu huyu William alikuwa anawatukana akina Mbowe na Dr Slaa hapa JF kama hana akili nzuri vile. Lakini ndiye huyu huyu Mbowe aliyesema kwenye mazishi ya Regia Mtema (RIP) kuwa serikali isiwakwaze vijana wanapojihusisha na siasa. Ndio hawa hawa akina Mbowe na Dr Slaa wamediriki kuwapa nafasi hao ambao William anawasifia sasa.

Unafiki ni kitu kibaya sana.
 
Ni wakati wa vijana nao kuonyesha kua nao ni sehemu au chachu kubwa katika kuleta maendeleo ya nchi yetu regardless ni wa chama gani. Lingine ambalo mimi naona halistahili sana ni ili la kuwahukumu watu kwa kua baba zao walikua watu fulani. Sioni kama lina tija sana, kikubwa tuangalie hao vijana tunaowahukumu je ni wasafi na wazalendo wa dhati kulitumikia taifa, hawana kashfa za kushirikiana na baba zao kuliibia taifa letu? Je wana vigezo vya kupewa nafasi wanazo omba kulinganisha na Watanzania wengine? Ni mtazamo wangu tu lakini!

Ingawa umejihami kwamba ni mtazamo wako lakini mimi nakuchallenge. Wewe unasema ni wakati wa vijana regardless ni wa chama gani. Mimi kwa hili nakupinga rafiki yangu. Kijana akishapata uongozi kupitia CCM anaharibika ubongo. Mfano mzuri ni Lusinde. Tunataka vijana tuwape uongozi lakini ni kwa kupitia Upinzani!

Pili wewe hutaki tuwakumu watu kwa kuwa Baba zao walikuwa watu flani hata kama wanavigezo. Kwa hili nakuchallenge. Mtu kama William Malecela amekimbia nchi na kukaa nje kwa zaidi ya miaka Ishirini alafu leo anatua Airport anakaa two months anatangaza nia ya kugombea Ubunge! Hivi mtu kama huyo unahisi ana nia ya dhati ya kuwakomboa wananchi au kaja tu kutafuta Ubunge kwa maslahi yake?

Obvious hata shida zetu hazijui na kama anazijua atakuwa ameambiwa, au amekariri kama alivyoziacha miaka ishirini iliyopita. Pili hawa watoto wanabebwa na Baba zao at the expense of others ambao Baba zao hawajawai kuwa Vigogo ndani ya Chama na Serikali. Naomba nikuulize, hivi kulikuwa na Sababu yoyote ya kulikata jina la James Ole Millya na kuliacha la William Malecela?

Kati ya James Ole Millya na William Malecela (Ingawa wote ni Magamba na hatuwataki) ni nani anarekodi nzuri ya kiungozi?
 
Usiwe mnafiki mbona Wiliamu kasema CDM kuna baba na wakwe zao bungeni hapo hajaingilia familia, punguza unafiki.

EasyFit,
Ben kama anampigia kampeni William aseme ila sisi hatupo tayari kuona Wabunge wetu 48 wanampa kura Willy. Amekuwa akitutukana sisi na Viongozi wetu hasa Mbowe na Slaa. Leo asijidai anamsifia Nassari kumbe analake jambo. Aende zake huko huko kwa kina Lusinde akaombe Kura. Atuache sisi na umaskini wetu, arudi zake tu Marekani.

 
- Well, heshima mbele sana wakuu wote JF, nipo Dodoma toka majuzi kwenye ukingo wa mbio za Ubunge wa EAC, jana usiku Royal Hotel nilifanikiwa kukutana uso kwa uso na Mbunge Mpya wa Chadema Kamanda Nassari, na leo tena Bungeni nimeshuhudia kuapishwa kwake na pia kupata muda wa kuongea naye na kupiga sana picha naye, I was glad kujua kwamba ni M-JF!

- HOWEVER: Ninasema hivi in Ubunge wa Nassari, ni ushindi kwa Vijana I mean the kid is just 26 years old, and here he is leading, hebu look back ulipokuwa 26 years old then ulikuwa wapi na unafanya nini? ndio utaelewa kwamba sasa ni wakati wa Vijana, sasa hii dhana ya Vijana iende kwenye kona zote za Taifa, it does not matter Nassari anatoka chama gani, it is the message ya the big picture hapa TAIFA KWANZA!

- MUCH RESPECT CDM, SALUTE NASSARI! NA MUNGU AIBARIKI TANZANIA!

William.

Kiukweli kama unayosema yanatoka moyoni, basi unaujasiri wa ajabu ambao wengi hawana,so nkutakie kila lakheri katika harakati zako mdau.
 
William,wawili hawawezi ambatana isipokuwa wamepatana.Sasa iweje wewe unayeunga sera za ukombozi wa Taifa la Tz na at the sametime unakula sahani moja CCMafisadi.Naomba usiwe mnafiki kwa nafsi yako mwenyewe.Vijena wa leo ni waelevu sana.
 
- Kabla ya uchaguzi nilikutana na Sioi na nikasema kwamba ni great guy na very kool

William.

Mnaona jamani. Akikutana na Sioi anampamba ni Great Guy leo kakutana na Nassari wetu nae pia anampamba. Jamani huyu si mwenzetu! Ni mnafiki tu! Aende huko kwa kina Sioi Sumari, Zainabu Kawawa, Vita Kawawa, Adam Malima, Hussein Mwinyi, nk wampe kura za Afrika Mashariki. Yeye kama anaona CDM inafaa ajiunge nasi mbona mwenzake Rachel Mashashanga yupo nasi licha ya kuwa Baba yake alikuwa kigogo wa CCM.

Yani hawa kina Willy ni Wapuuzi sana. Wamekariri tu Baba akiwa CCM basi lazima na yeye awe CCM! Huu ni ujinga wa akili unaowasumbua hawa watoto na ndio maana tunawapinga na tutaendela kuwapinga hata kama wakishinda kwa kubebwa!
 
Mimi siwezi ku-entertain ujinga kwa sababu ya itikadi za kisiasa. Hapa ni ustaarabu na utu siyo political ideology. Siangalii kama ni mwana-CCM au mwana-CHADEMA.

Kwa hiyo matusi ya William Malecela kwa Mbowe na Slaa kwako ni Ustaarabu? Au unajifanya hujui? Acha ujuha Ben. We ni Mchadema mwenzetu inapofika hatua adui yetu aliyekuwa anawakashifu Viongozi wetu leo anajirudi lazima tumkatae kama ukoma. Vinginevyo aombe radhi na ajiunge na jeshi letu. Sio anajidai Ooooh Nassari is great wakati kumbe anataka atuwin!
 
- Classic ndio tatizo letu Tanzania, tumechanagnywa sana na wanasiasa mpaka tumefikia mahali ni vigumu kuamini anything!

William.

So you are not politician???? Unajikanyaga kweli....kama wanasiasa hawaaminiki, nani unataka akuamini????
 
Good Message kamanda.Kila la kheri.Narudia tena kukuomba mwaka 2015 nenda Mtera kamtoe yule mhuni anayejiita Mbunge Lusinde.Anaidhalilisha sana Mtera na anawafanya vijana wote wapuuzwe kwa sababu ya maneno yake ya kipumbavu.William nenda Mtera na tutakuunga mkono NO matter unatokea chama gani.Read my words ana I mean it!

Lakini ili ushinde kirahisi.....Vua magamba, vaa magwanda!! Maana cdm nao wataweka mgombea, na operesheni ya Lema itafika mtera kumwaga sumu. Ni ushauri tu.
 
Back
Top Bottom