Nassari: Lowassa anahusika kunipiga

Nassari: Lowassa anahusika kunipiga

Pole sana kamanda Nasari!...tunajua unyama na uovu wa ccm. Jana tumesikia kauli ya waziri mkuu akiidhinisha uvunjaji wa katiba kwa kuwapa policcm idhini ya kuwapiga watuhumiwa kabla ya kuthibitika kuwa wakosaji. Serikali hii inaendeshwa na genge la mafia, wananchi inabidi tujitafutie mifumo yetu ya kienyeji ili kujihami na dola lililogeuka tishio kwa siha na ustawi wa taifa.
MUNGU anaona, na ushindi hauko mbali.
 
Kwahiyo watu walimuona tu Nassari yule wakaenda kumpiga virungu? basi hao kwa hakika watakuwa ni wendawazimu.
 
Hv upigwe mpaka upelekwe hosp halafu uhamushiwe Moi bila hata ya maumivu au kuvunjika popote , kweli alipigwa au alikimbizwa? Mtoto ana kauli na dharau mbaya sana hata kwa viongozi wenzake huyu , mdom wake utamghalimu.
 
Nasari jiuguze utulie dogo umeanza siasa mwaka jana lowasa ni master wa siasa utaumia muulze sta,mwakyembe na kna sumaye!Dogo usikmbze upepo wenzko kna mbowe wanaenda kwa step na wanamjua EL ni mafia wa siasa toka ktmbo ata nyerere alkua anamuita kjana mjeur..lowasa almuonyeshea nyerere ujeur uwe wewe utaumia kijana
 
usdanganywe na maadui wa lowasa ksiasa utaumia ata akna nyalandu alyekusndkza airpot si kwmb anakutakia mema nyalandu ni kampen meneja wa membe ktk kutafta urais 2015 wanakudanganya unaropoka kwa sababu ni maadui wa lowasa ksiasa na amewazd kete kila idara kuanzia ndan ya ccm ad nje!take kea Nasari lowasa ni hatar dogo
 
haka kajamaa kalitoroka jkt visingizio eti kapata taarifa usalama wa taifa watamwua.

hospitali ya dini nako wanataka kumwua. bado anakimbilia muhimbili hospital tena ya serikali. usalama wavaa koti nyeupe hawako muhimbili.

huyu kijana ni toto jinga. yuko kwenye movie.
 
Cheap popularity + Cheap politics/ = Nassari.

Sent from my BlackBerry 9900 using JamiiForums
 
Tanzania politics at its best.

Mpaka kufikia 2015 tutakuwa tumeona na kusikia mengi.

Politically, Today is Mh. Lowassa accusation day.

Kuna mkono wa Mh. Lowassa katika dhoruba hii ya kisiasa na kidini, This is according to Mh. Nassari. Is this true or is just a filthy insinuation?.

This is very serious allegation lakini wakati huo huo na yeye Mh. Nassari anapigwa dongo kama ni "mwigizaji" na hata hospitali ya Selian ilikuwa na angalizo tofauti ukilinganisha na kile Mh. Nassari alikuwa akikisema. Mgonjwa na dakitali wake wamepishana katika kujaza hospital exit form.

Who's telling the truth ?.

Wanasiasa watendeeni haki wananchi wenu. Tanzania kwa sasa inaweweseka kwa sababu ya wanasiasa na siasa uchwara.

Hii sentensi tata sijui ina maana gani. Kwa kifupi tu tunaweza kuiweka kwa jinsi tunavyotaka na ikaleta maana.


Mh. Nassari ana maanisha kama viongozi wa CCM hawajakumbwa na dhuruba hii ya kisiasa na kidini ina maana wao ndiyo watengenezaji. Really?.

Lakini pia anasahau kuna wengine tunasikia wanajiteka na kudai wametekwa kama ilivyotokea hapa JF, Zanzibar na Tanzania bara (Ludovick). Hawa nao sijui tuwaweke katika kundi lipi wakati vile vile hata yeye anadaiwa ni mgonjwa magumashi (FAKER).

Siasa za Tanzania ni vituko tupu.

Wanasiasa wengi wanadhani kusema uongo ndio kujiimarisha kisiasa kumbe ni kujichimbia kaburi. Mnyika anasema hivi mara nassari akanushe yaliyosemwa na mnyika. ninachoona wao wanaongozwa zaidi na hisia zao badala ya uhalisia wa mambo.
 
Sikubaliani na Nassari...halafu kwa kauli zake hizi naamini amepunguza credibility.
Kwamba kwa sababu alimshinda mkwe wa Lowasa basi Lowasa anahusika...!
Kingine...,na kinachochekesha zaidi ni kuwa Makinda nae anahusika...,kisa...! Hajampigia simu/kumtumia sms...!
Kwenye hili,anapunguza credibility yake,asitafute mchawi, kutaka sifa kwa kuropoka ndio mchawi wake.

CCM mmeshindwa kufanya siasa huru, mnapiga watu ovyo tu, mmefilisika kichwani!
 
haka kajamaa kalitoroka jkt visingizio eti kapata taarifa usalama wa taifa watamwua.

hospitali ya dini nako wanataka kumwua. bado anakimbilia muhimbili hospital tena ya serikali. usalama wavaa koti nyeupe hawako muhimbili.

huyu kijana ni toto jinga. yuko kwenye movie.
Jenifa mimi nilikuwepoe usumbufu ulikuwa mkubwa wardini kiasi cha madaktari wenyewe kushauri aondolewe, nyie mnadhani ni ushabiki wa kisiasa tu kwa kila kitu..
 
Last edited by a moderator:
mi hata sielewi tena bhana maana nimechoka kuelewa
 
Ni kweli, Lowasa ni mtu wa kulipiza visasi sana ila anasahau waliomuhujumu Arumeru ni haohao CCM
 
Mbunge wa Arumeru Mashariki (Chadema), Joshua Nassari amemtuhumu Mbunge wa Monduli Edward Lowassa kwamba anahusika na kipigo alichokipata kutokana na chuki aliyonayo kwake.

Aidha amemtuhumu Spika wa Bunge, Anne Makinda kwamba naye ni miongoni mwa watu wanaomchukia pamoja na viongozi wengine wa Bunge, kwa kuwa hakuna kati yao aliyempigia simu au kumtumia ujumbe wa kumjulia hali kutokana na kipigo alichopata ambacho kimemsababishia maumivu makali.

Akizungumza jana akiwa kwenye chumba alicholazwa katika Taasisi ya Tiba ya Magonjwa ya Mifupa na Ufahamu Muhimbili (Moi), Nassari alidai Lowassa ambaye amewahi kuwa waziri mkuu kabla ya kujiuzulu, amemchukia tangu alipomshinda mkwewe Sioi Sumari, kwenye uchaguzi mdogo wa ubunge uliofanyika Aprili mwaka jana.

Nassari aliyekuwa amelazwa katika Hospitali ya Selian ya jijini Arusha kabla ya kuhamishiwa MOI, alidai kupigwa na kuchaniwa nguo na Green Guard wakati alipokuwa katika jitihada zake za kuhesabu kura kwenye uchaguzi wa udiwani wa Kata ya Makuyuni-Monduli.

“Kipigo nilichopata Lowassa anahusika ananichukia, anataka urais lakini hawezi kuupata kwa kuuumiza watu kama hivi, alifikiri kwamba nitakufa sitakufa hadi kwa mapenzi ya Mungu,” alisema.

Alisema kuna jambo ambalo wananchi wanapaswa kulifikiria ni jinsi ambavyo kumekuwa na matukio ya kutekwa na kuvamiwa, lakini hakuna yanayohusisha kiongozi wa CCM, badala yake ni raia wa kawaida na viongozi wa dini na siasa. Nassari alidai akiwa kama wakala mkuu wa Chadema katika kata hiyo, alikumbana na mambo kadhaa yaliyomshangaza, ikiwa ni pamoja na kufanyiwa jaribio la kutekwa mara mbili, kabla ya kushambuliwa kwa kipigo.

Alisema pia anashukuru kwamba askari wawili waliokuwepo katika eneo hilo walijitahidi kutaka kumnusuru, lakini walizidiwa nguvu na vijana hao, hasa kutokana na kutokuwa na bunduki, ambapo yeye alipofanikiwa kuchoropoka alikimbilia bastola yake na kuwanyoshea vijana hao bila kufyatua.

Akizungumzia kuhusu hali yake, Nassari alisema amepimwa kipimo cha X-ray ambapo imeonyesha kuwa pingili za mgongo wake zipo sawa, lakini daktari ameshauri afanyiwe kipimo kingine kiitwacho MRI ili kuangalia hali ya mishipa kutokana na maumivu makali anayoendelea kuyapata.

Aidha alitumia fursa hiyo kumshukuru Mbunge wa Kuteuliwa, Joseph Mbatia kuwa ndiye aliyemsaidia kufanya mipango kuwasiliana na uongozi wa Bunge na kumwezesha kuhamishiwa Moi, baada ya wabunge wote wa Chadema kwenda Arusha kushughulikia waliofariki kwa bomu.

Hata hivyo, Lowassa alipotafutwa kuhusiana na tuhuma hizo alikataa kuzungumzia suala hilo na kusema hilo aulizwe Msimamizi wa Uchaguzi, Paulo Kitaleki.

Mwananchi ilimtafuta Kitaleki ambaye pia ni katibu tarafa, alikanusha kuhusika kwa Lowassa akielezea kuwa siku ya tukio hilo alikuwa Geita.

“Huyu Nassari ni mwigizaji na anafaa kuwa msanii kwa kuwa anaigiza tu hata hakupigwa, bali yeye ndiyo aliyempiga Wakala wa CCM, Hussein Osama ambaye ni mlemavu, kisha akatimua mbio baada ya vijana kutaka kumkamata, nashangaa kumwona yupo hospitali akidai kupigwa, siyo kweli,” alisema Kitaleki.

Habari kwa hisani ya Mwananchi.

Photo taken from Selian to Muhimbili hospital bed.
Hata kama Nassari ni muongo lakini mbona madaktari wanaendelea kumutibu ,
1.je wanamtibi nini kama hakupigwa???
2.Kama Nasary kapigwa je kapigwa na chadema???
3.Wote humu tumukubaliana kuwa waliotembeza kipigo kwa washabiki wa chadema na wabunge ni CCM sasa Lowasa sio CCM???
4.Lowassa ndiye mfadhali mkubwa wa makundi ya CCM na ndiye anataka kugombea urais na upo ukweli bila shaka kuwa Arumeru Nasary ana nguvu kuliko Lowassa sasa hapa hakuna ushahidi ??


MIMI NINGESHAULI TUCHANGIE KWA HOJA KWA KUWA NASSARY AMETOA HOJA ; TUSICHANGIE KWA MTAZAMO WA KUMUONA LOWASSA KAMA CCM NA SI CHADEMA!!!
 
Back
Top Bottom