Nasra na Kassimu: Mapenzi ya kweli ingawa hayakudumu! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nasra na Kassimu: Mapenzi ya kweli ingawa hayakudumu!

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Dark City, Apr 4, 2012.

 1. Dark City

  Dark City JF-Expert Member

  #1
  Apr 4, 2012
  Joined: Oct 18, 2008
  Messages: 16,277
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160
  Binafsi najikuta mara nyingi nikipata shida kuamini kama kweli kuna kitu kinachoitwa mapenzi ya kweli katika ndoa zetu. Hata hivyo, siku ya Jumapili (1 Aprili 2012) kulikuwa na story kwenye kipindi cha Njia Panda katika Clouds Radio ambacho kimedhihirisha kuwa inawezekana kabisa kukawepo na mapenzi ya kweli. Ingawa nimechelewa kipindi kwa karibia dakika 30, hata hivyo nimeweza kupata undani wa story iliyokuwa inaongelewa.

  Story yenyewe inamhusu Bwana Kassimu, ambaye ni dereva wa pikipiki (boda boda) anayeishi eneo la Mabibo jijini Dar. Kassimu alienda siku moja kwenye bar moja ambayo hakuitaja, iliyoko jirani na kwenye kijiwe chake, ili kupata mchemsho wa kuku. Alihudumiwa na msichana aliyeitwa Nasra ambaye alitokea kuvutiwa naye. Jamaa alimwomba wakae wote katika meza aliyokuwa ameketi na wakapata chakula pamoja. Baada ya hapo, Kassimu alihisi mvuto wa ajabu na alirudi kwenye ile bar jioni, wakala chakula cha jioni pamoja.

  Ingawa alijaribu kujizuia kwenda kwenye ile bar mara kwa mara, alijikuta anashindwa na kulazimika kwenda. Siku moja akiwa kwenye ile ba na amekaa na Nasra, ulitokea ugomvi kati ya Nasra na boss wake (meneja wa bar) hadi ikambidi Kassimu kuingilia kati. Alimwomba Meneja amwache Nasra kwa kuwa ni mpenzi wake. Baada ya ugomvi kuisha, Nasra alimweleza Kassimu kuwa Meneja alikuwa anamlazimisha kwenda kufanya ngono na mwanamume ambaye Nasra mwenyewe hamfahamu na wala hakuongea naye. Ilielezwa kwamba huyo meneja alikuwa na tabia ya kuwauza wafanyakazi kwa wanaume na malipo kupokea yeye. Wale waliokubali kufanya ngono na wanaume waliotafutwa na Boss wao, hawakulipwa chochote kwani ilichukuliwa kama sehemu ya kazi yao. Kutokana na ugomvi huo, Nasra alifukuzwa kazi na Kassimu alipokuja tena pale kwenye bar hakumkuta.

  Kassimu aliwauliza wenzake Nasra ambao walimpa msaada hadi akampata. Bila kusita, alimwomba Nasra aende kwake wakaishi pamoja. Nasra alikubali na walipanga kutafuta pesa ili wakafanye taratibu za ndoa, ikiwemo kwenda kwa wazazi wa Nasra huko Sengerema. Hata hivyo, Nasra alipata mimba na ikawabidi kuahirisha mipango ya ndoa. Ilipofika wakati wa kujifungua, Nasra alipelekwa katika hospitali ya Mwananyamala kwa ajili kupata huduma. Alikaa pale hadi siku ya pili alipojifungua mtoto wa kiume (amepewa jina la Kudra) ila mama hali yake haikuwa nzuri na akapelekwa Muhimbili kwenye kitengo cha wagonjwa mahututi (ICU). Baada ya jitihada za madaktari kushindikana, Nasra alifariki dunia kwa kile kilichoelezwa kuwa ni pulmonary edema (kujaa maji kwenye mapafu) na kuzikwa maeneo ya Mabibo . Hata hivyo, Kassimu bado hawajui ndugu zake ikiwa ni pamoja na familia ambapo Nasra alifikia na kufanya kazi za nyumbani.

  Kutoka na ukata, Kassimu ameshindwa kumlea mtoto wake ambaye ana umri wa mwezi mmoja na nusu, na sasa anasaidiwa na jirani yake ambaye ameamua kumchukua mtoto na kuishi naye. Hata hivyo msaada zaidi kwa ajili ya kununua maziwa ya mtoto na mavazi unahitajika. Kassimu anapatikana kwa namba 0713 540 760.  Karibuni tena kwenye jukwaa letu tukufu la MMU, na naamini kwamba matokeo ya Arumeru na kwingine yanatupa nguvu ya kusonga mbele !!

  Babu DC!!
   
 2. Smile

  Smile JF-Expert Member

  #2
  Apr 4, 2012
  Joined: Jul 18, 2011
  Messages: 15,431
  Likes Received: 194
  Trophy Points: 160
  dah kisicho riziki hakiliki jamani
   
 3. Bishanga

  Bishanga JF-Expert Member

  #3
  Apr 4, 2012
  Joined: Jun 29, 2008
  Messages: 15,347
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 0
  A sad story,historia inatufundisha kuwa ex bar maids can make very good wives.Ila kassimnaye ngoja tumseme,juu ya nini unaishi na mtoto wa watu bila kujua kwao? Anyway ngoja nimrushie tigo pesa.
   
 4. MadameX

  MadameX JF-Expert Member

  #4
  Apr 4, 2012
  Joined: Dec 27, 2009
  Messages: 7,847
  Likes Received: 64
  Trophy Points: 145
  Duuh pole yake, mimi naona matatizo ni nani wa kumlea hako katoto kama mama but habari ya matumizi ya mtoto Kassimu alifkiria nini wakati walipoamua kuishi pamoja kuwa na family?
   
 5. YNNAH

  YNNAH JF-Expert Member

  #5
  Apr 4, 2012
  Joined: Dec 6, 2011
  Messages: 1,663
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 145
  Duh!! Very sad.
   
 6. Nicas Mtei

  Nicas Mtei JF-Expert Member

  #6
  Apr 4, 2012
  Joined: Dec 21, 2010
  Messages: 11,569
  Likes Received: 106
  Trophy Points: 160
  Nami pia nilihuzunishwa sana na story yake. Ilifikia mahali akawa hadi analia..
   
 7. Dark City

  Dark City JF-Expert Member

  #7
  Apr 4, 2012
  Joined: Oct 18, 2008
  Messages: 16,277
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160

  Kaka,

  Hii story ina mambo mengi sana....

  Binafsi nimejikuta nahangaika na kujaribu kubadili imani yangu. Naanza kuhisi kwamba, may be kuna mapenzi ya kweli duniani...Wakati Kassimu anahojiwa...ilionekana kwamba kweli hawa watu walipendana on first sighting!! It was so sweat to hear that!

  Kassimu hakuwa na pesa maskini ya Mungu ila hiyo haimuondolei hamu ya kuwa mume na baba...Wapo watu wengi sana wanaishi maisha ya namna hiyo ila Mungu anawanusuru na maswahibu mazito mazito ndiyo maana hatupati issues zao.

  Babu DC!!!
   
 8. Dark City

  Dark City JF-Expert Member

  #8
  Apr 4, 2012
  Joined: Oct 18, 2008
  Messages: 16,277
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160
  Ni swali zuri sana ila issue ya Kassimu na Nasra ina mambo mengi. Kwanza Nasra alikuwa amefukuzwa kazi na inawezekana Kassimu alichangia katika tatizo hilo. May be bila Kassimu, Nasra angeweza kukubali matakwa ya Boss wake na kuendelea na kazi. Kassimu kama binadamu yeyote (achana na mapenzi waliyokuwa nayo) ilikuwa ni busara atoe msaada kwa Nasra.

  Pili, zipo ndoa nyingi sana hapa nchini ambazo zinaishi maisha kama hayo. Ni kama maisha ya ndege. Hawana uhakika watakula nini na wakati mwingine hata pa kulala ni tatizo.

  Babu DC!!
   
 9. Edson

  Edson JF-Expert Member

  #9
  Apr 4, 2012
  Joined: Mar 7, 2009
  Messages: 9,200
  Likes Received: 714
  Trophy Points: 280
  nilikifatilia kisa hiki online kupita hiyo radio clouds pale nairobi.....huyo jamaa kapitia vikwanzo vingi sana kwanza alianza kuuza mkaa huko huko maeneo ya mabibo hadi akapewa jina la MASIZI na wateja wake....baada ya hapo jamaa alihama kwa tajiti wake baada ya kuona mshahara ni mdogo (elfu kumi) akaenda kwa mwajiri mwingine aliyekuwa anamlipa elfu 40 kwa mwezi kwa kazi hiyo hiyo ya kuuza mkaa...baadae yule tajiri yake alihamishwa kikazi na hivyo biashara yake ya kuuza mkaa ikafungwa...kwa kuwa alikuwa ameshafahamika sana pande za mabibo alipata tajiri mwingine...lakini safari hii huyu tajiti alikuwa na visa sana..alikuwa hamlipi pesa kwa wakati na pia manyanyaso mengi nasiku moja gafla alifika na kenta pale eneo la biashara na kuchukua mkaa wote na kuondoka nao...bwana masizi (kasim) alienda kito cha polisi na kulipoti tukio hilo lakini kwa kuwa jamaa alikuwa na pesa(tajiri) alimsingizia kuwa bwana kasimu amemuibia mkaa gunia 300...

  kasimu aliwekwa rumande na hivyo maana alikosa mtu wa kumdhamini...baadae akahamishiwa segerea....kule geto kwake alikuwa anaishi na masela wenzake ..wale masela baada ya kuona jamaa yuko ndani walluiza kila kitu cha kasimu (kitanda, godoro, redio,viatu na vitu vingine) wakasepa.... kuna mama mmoja ni mtu wa shighuli wa ccm alienda kule segerea na kuongea na wakuu wa gereza na hivyo kasimu kuachiwa huru....aliporudi uraiani jamaa hakuwa na pa kushika ...maana kila kitu kiliwa kimeuzwa....basi jamaa akaanza kuosha piki piki huku akijifunza kuendesha ndani ya mda mfupi akawa dreva mzuri na hivyo kupewa boda boda na jamaa mmoja..

  siku hiyo baada ya shughuli aliwekwenda kwenye hiyo baana kuagiza mchemsho wa kuku maana likuwa kaumisi mda mrefu...aliyemhudumia ni huyo NASRA..nalimuona kama ni mcheshi na mpole baadae alimwambia nasra nae ale chakula nasra akala na uhusiano wao ulianzia hapo....

  mimi niliishia hapo kusikiliza kisa hiki maana mda wa kupanda pipa ulikuwa umeshafika so nilizima ki laptop changu.....huko ulikoeleza mkuu babu DC sikusikiliza..kumbe nasra alifariki? ....ningekuwa najua jina la baba yake ningewatafuta wazazi wake.....maana huko sengerama napafahamu nimekulia huko na kusomea huko na ninakwenda huko pasaka hii.....ngoja nitumie namba hii ya kasimu(masizi) ili nijue kama ana detail zaidi za mahali nasra alitoka huko singer(sengerema)....tutamsaidia....
   
 10. toghocho

  toghocho JF-Expert Member

  #10
  Apr 4, 2012
  Joined: Mar 16, 2011
  Messages: 1,177
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  sorry kuna sehemu sijaelewa, jamaa kabaki mwenyewe, afu ni dereva wa bodaboda (ambayo ni biashara) sasa huo ukata wa hata kununua maziwa unatoka wapi? sorry nataka kujua tu
   
 11. Power to the People

  Power to the People JF-Expert Member

  #11
  Apr 4, 2012
  Joined: Jul 11, 2007
  Messages: 1,193
  Likes Received: 238
  Trophy Points: 160
  Kuna watu wengi sana wanakutana na wapenzi wao bila hata kujua majina ya pili ya hao watu wanaoanzisha mahusiano nao. Ninafanya kazi katika kampuni fulani kazi za kudeal na mahusiano ya watu na mwajiri. Wakati wa kujaza mikataba yao ya ajira umuulize mke wako anaitwa nani atakuambia mama fulani, na sio kwamba amepitiwa ni kweli kabisa hajui anachojua ni jina la kwanza tu kwa hiyo inabidi atoke nje kidogo afanye mawasiliano na mama fulani wake aje akupe jina kamili.

  Na mbaya kabisa logwa uulize tarehe ya kuzaliwa mbona atakushangaa sana why should he know the date of birth of his wife haoni umuhimu. wengi wao lakini ni wale ambao hawakubahatika kujiendeleza katika suala la elimu ingawa wako wengine walioenda shule kidogo ambao hawaoni umuhimu wa kujua tarehi za wenzi wao za kuzaliwa au hata watoto wao.
   
 12. Safina

  Safina JF-Expert Member

  #12
  Apr 4, 2012
  Joined: Jun 18, 2009
  Messages: 498
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Masikini pole yake, nadhani alikuwa anamlilia my wife wake, na si ugumu wa maisha.
   
 13. Dark City

  Dark City JF-Expert Member

  #13
  Apr 5, 2012
  Joined: Oct 18, 2008
  Messages: 16,277
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160

  Safina,

  Story ya Kassimu kama ambavyo Edson kaongezea, ilikuwa inagusa sana moyo wa kila binadamu. Siyo yeye tu aliyetoa machozi bali na wasikilizaji wengine tulijikuta tunamwaga machozi pia!

  Babu DC!!
   
Loading...