Nasikia kuna uchawi wa kumfunga mtu asipate kazi ya kuajiriwa baada ya kumaliza chuo, wala riziki katika biashara yake, hili swala lina ukweli?

Dah msoto kitu kibaya yani ukute na we ni kati ya graduates waliokosa kuajiriwa sasa unatafuta kisngizio. Mkuu pambana maisha siyo kuajiriwa tu unaweza pambana ukatoka aisee Mungu hutenda kwa wakati wake tena ulio sahihi ila juhudi zako na maombi ndiyo muhimu.
 
KAJINI KA KUDATISHA WATU,NOMA SANA WANDUGU.
USIOMBEE,(UTAVUTISHWA MIBANGE WE NA KUNYWESHWA MIPOMBE BILA KUJITAMBUE MPAKA UCHOMOLEWE NA NDG MWENYE UPENDO WA KWELI)
 

Kuna point umeingelea hapo kati naomba nisaidie kufahamu zaidi.

Kwamba “zinahitajika malighafi nyingi mchawi azipate ili kumroga mtu fulani na ili arogeke kisawasawa”.

Je ni malighafi gani hizo @ Mshana?

Awareness is empowering!


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu usimbeze kijana. Kuajiriwa ni haki yake, na kuwezeshwa kujiajiri ni haki yake pia.
Serikali yeyote iliyo makini moja ya mkakati wake wa msingi ni pamoja na hilo. Maana ukisema apambane na maisha bila kumuonyesha mpangilio, basi itakuwa bahati kama hataamua kufuata njia za kihalifu ambazo nazo pia sio za kubeza maana matajiri wengi zimewatoa na Leo wako nyumba za ibada na kutoa misaada kwa jamii.
Hivi kila wahitimu wa elimu za juu 50,000 kila mwaka wakaamua kujiajiri katika ujambazi baada ya muda mfupi hata Nigeria si tutawaacha mbali?
CCM waache kuwatumia vijana kwa maslahi yao bali wawatengenezee future yao, hilo ni bomu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ukiachana na uchawi ule wa zongo unaokaa machoni.. Huo mwingine lazima upate vitu visivyopungua vinne kisha uchanganye na madawa halafu ufanye manuizi
Jr
 
Umeelewa nilichokiandika? Mimi nimemjibu kwa mtazamo wake wa uchawi hayo mengine ume assume wewe
 
Ukiachana na uchawi ule wa zongo unaokaa machoni.. Huo mwingine lazima upate vitu visivyopungua vinne kisha uchanganye na madawa halafu ufanye manuizi

Jr


Alaa kumbe?!

Kumbe haina haja ya kuogopa wachawi ambao wako mbali nasi au siyo.

Sasa naomba nisaidie kufahamu hivyo vitu visivyopungua 4 vinavyochanganywa na madawa na kufanya manuizi ili mtu arogeke


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hakuna mambo ya kichawi ni hali yenyewe tuu.Japokuwa kuna watu ambao tunaenda mwaka wa 7 bado wanasugua benchi na Digrii zao safi tu.
 
#Akilinjema uchawi jambo la kipuuzi sana na wala haliitaji malighafi nyingi vile udhaniavyo!,mfano,chukua jina lako halisi liandike kwenye karatasi nyeupe,chukua buibui mweuzi muweke hapo,andika namba 3,5,7 na 9,popote tu kwenye hiyo karatasi fungasha vyote vifunge pamoja kwa uzi mweusi,ichomeke kwenye papai kaizike makaburini uone utakavyopandishwa vyeo.
 
Mkuu inaonekana ww ni muhanga wa tatizo la ajira.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hii itanifaa mimi maana toka jiwe aingie sijawa promoted

Sent using Jamii Forums mobile app
 
👊👊👊👊 I second you!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…