Nasikia kuna uchawi wa kumfunga mtu asipate kazi ya kuajiriwa baada ya kumaliza chuo, wala riziki katika biashara yake, hili swala lina ukweli?

AlphaMale

JF-Expert Member
Oct 26, 2019
617
1,000
Inasemekana kuwa tanzania haina nafasi za ajira za kutosha za kuwaajiri wasomi wote wanaohitimu vyuo vikuu, ila cha kushangaza nilisoma baadhi ya thread humu, kuna watu wali-comment kuwa walikosa kazi baada ya ku-graduate chuo, ila baada ya wao kwenda kwa waganga na kuogea madawa waliopewa na waganga, baada ya mda mfupi sana walipata kazi ya kuajiriwa yenye mshahara mzuri..waganga waliwaambia hao watu kuwa walifungwa kichawi ili wasipate kazi, sasa sielewi ina maana wote waliokosa kazi miaka mingi baada ya kumaliza chuo wamelogwa?

Tufundishane dalili za kufungwa kichawi usipate riziki kwenye biashara yako /au usipate kazi ya kuajiriwa..na kama kuna watu waliokutana na hivi visanga m-share experience zenu humu
 
tilmikha

JF-Expert Member
Feb 27, 2013
368
500
Uchawi wa kufungwa usipate kazi upo na dalili zake kama uchawi mwengine tu.Ila kuamini kuwa hujapata kazi sabab kuna mtu amekufanyiwa uchawi pia ni uchawi na utakua umejiroga mwenyewe. Nini cha kufanya? Usiende kwa waganga wala usiamini kuwa kutokupata kazi kwako sabab ni uchawi licha ya kuwa uchawi upo, bali kuwa patient, subir na endelea kupambana. Kinachowashinda wengi siku hizi ni subra (patience), muda mwengine mambo yanachelewa kutufikia ili tukiyapata tujue thamani yake.
Patience is most fitted.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
fazili

JF-Expert Member
Jun 10, 2011
7,363
2,000

Usisubiri tu kwani waweza kusubiri hadi mwisho wa dunia. Unachotakiwa kufanya ni maombi ya nguvu katika Jina la Yesu ukimwomba haja yako ambayo utaitaja kinagaubaga.

Pia fanya maombi ya vita au warfare prayer kuweza kuvunja nguvu za giza. Ila uwe vizuri kiroho kabla ya kupigana vita ya kiroho. Kama huna uzoefu au nguvu na pia ujuzi wa vita ya kiroho basi usifanye mwenyewe ila mtafute mtumishi wa kweli wa Yesu Kristo akusaidie nawe utakuwa huru na kuwa na maisha bora.

Watu wengi mno wanaibiwa mafanikio yao bila kujua na hata wakigundua huenda kwa waganga wa kienyeji. Hii ni sawa na kupeleka kesi ya mbuzi kwa fisi. Peleka haja zako kwa Yesu Kristo na sio kwa shetani.
 
tilmikha

JF-Expert Member
Feb 27, 2013
368
500
Kama hata Yesu anatoa hapo kwa hapo sidhani makanisa yangekuwepo, kila kitu kinahitaji patience
Usisubiri tu kwani waweza kusubiri hadi mwisho wa dunia. Unachotakiwa kufanya ni maombi ya nguvu katika Jina la Yesu ukimwomba haja yako ambayo utaitaja kinagaubaga.

Pia fanya maombi ya vita au warfare prayer kuweza kuvunja nguvu za giza. Ila uwe vizuri kiroho kabla ya kupigana vita ya kiroho. Kama huna uzoefu au nguvu na pia ujuzi wa vita ya kiroho basi usifanye mwenyewe ila mtafute mtumishi wa kweli wa Yesu Kristo akusaidie nawe utakuwa huru na kuwa na maisha bora.

Watu wengi mno wanaibiwa mafanikio yao bila kujua na hata wakigundua huenda kwa waganga wa kienyeji. Hii ni sawa na kupeleka kesi ya mbuzi kwa fisi. Peleka haja zako kwa Yesu Kristo na sio kwa shetani.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mshana Jr

Platinum Member
Aug 19, 2012
152,471
2,000
Tuna jukumu kubwa mno la kuilemisha jamii kuhusu uchawi... Si kila kitu ni uchawi... Swala la ajira ni kilio cha dunia.. Dunia haina uwezo wa kutoa ajira kwa wasomi wake wanaohitimu kila mwaka
Huyo unayedhani anakuroga naye ni mtafutaji kapuku tu kama wewe.. Yaani aache ishu zake aende kukuroga.
Zinahitajika malighafi nyingi mpaka kumroga mtu
Kingine ni wahitimu wengi kuchagua kazi na mazoea ya kutaka kuajiriwa kuliko kujiajiri.. Lakini pia kuna watu wana connection na wengine huhonga... Sasa watu kama hawa hawawezi kukwambia ukweli
Kuhusu hili la kupata kazi mara baada ya kwenda kwa mganga ni imani tuu.. Ingekuwa waganga wa kienyeji wana uwezo wa kukufanya upate ajira kungekuwa hakuna haja ya kusoma

Jr
 
Jokajeusi

JF-Expert Member
Jun 1, 2018
5,467

Nilikuwa nakusubiria hapa nione utakavyo changia.

Namshukuru Mungu umechangia kwa akili.
 
Chakaza

JF-Expert Member
Mar 10, 2007
36,470
2,000
Uchawi sio lazima kuloga kwa tunguli. Hata kuwa na nia mbaya tuu kwa wengine ni uchawi.
Serikali ya sasa ya CCM ni wachawi kwa wananchi wake, haiwatakii mema vijana wake ndio maana haijishughulishi kutafuta muafaka wa kupunguza tatizo la ajira na kufungua fursa za kujiajiri huku wao na watu wao wakijiwezesha.
Kwa vile dawa ya kutokomeza uchawi ni kumuondoa mchawi, vijana na wazazi wa vijana tushirikiane kumuondoa mchawi CCM bila kumuonea huruma SASA.
Vijana mkikubali mapambio ya wanasiasa wa CCM mjue mnawasindikiza watoto wao na mkija kushtuka mmekuwa wazee na bahasha zenu za kaki kwapani pia ndoto zenu za miradi kuwa za Alinacha.
Kwako Mshana Jr!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Liwagu

JF-Expert Member
Jan 25, 2017
2,130
2,000
Uchawi ni mambo ya kipuuzi tu yasiyo eleweka.
Na watu wavivu wa kufikiri ndio wanaangukia huko kwenye hayo mambo yasiyo eleweka.

There's nothing proves juu ya hicho kinachoitwa uchawi.
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mshana Jr

Platinum Member
Aug 19, 2012
152,471
2,000
Very well said....
Uchawi sio lazima kuloga kwa tunguli. Hata kuwa na nia mbaya tuu kwa wengine ni uchawi.
Serikali ya sasa ya CCM ni wachawi kwa wananchi wake, haiwatakii mema vijana wake ndio maana haijishughulishi kutafuta muafaka wa kupunguza tatizo la ajira na kufungua fursa za kujiajiri huku wao na watu wao wakijiwezesha.
Kwa vile dawa ya kutokomeza uchawi ni kumuondoa mchawi, vijana na wazazi wa vijana tushirikiane kumuondoa mchawi CCM bila kumuonea huruma SASA.
Vijana mkikubali mapambio ya wanasiasa wa CCM mjue mnawasindikiza watoto wao na mkija kushtuka mmekuwa wazee na bahasha zenu za kaki kwapani pia ndoto zenu za miradi kuwa za Alinacha.
Kwako Mshana Jr!

Sent using Jamii Forums mobile app

Jr
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom