Nashukuru sijakuufoo sarooo, kwa heri go with peace

Nashukuru sijakuufoo sarooo, kwa heri go with peace

hehehe "not permanent and pensionable".
Hii kitu haina formula asikufiche mtu! The principle is never stress and never put too much expectations!
 
Akili za hawa viumbe ni ndogo kwakweli (samahani wanawake). Hayo uliyomfanyia yote bado akili yake haijaamka? Usijali mkuu, na wala usiseme hutakuja kupenda tena hapana, mshukuru Mungu amekuonyesha tabia halisi ya huyo mwanamke, utapata tena utapata kaka utampata mwanamke bora kwako
Siyo wanawake wote wana tabia hiyo bwana.
 
Nashukuru wote mliocomment, nitazifanyia kazi hizo comments pamoja na pm. Mbarikiwe sana
 
Mi ndio maana nikipata chance ya kumuumiza mwanamke namuumiza sawa sawa... joke
 
Pole sana,ila kweli penye miti hakuna wajenzi,atakukumbuka one day!chukulia poa tu!
 
Where, in the bible did God allow us "to meet few wrong people" before meeting the right person? in other words, do you mean that God allowed fornication before marriage? au umemaanisha nini kusema hivyo??

nimequote shairi flani hivi na sio kutoka kwenye bible ndugu yangu
 
Pole sana mkuu. Ndio uume huo.
Achana nacho hicho kibweka, tafuta mwengine. Iko siku ataukumbuka wema wako.
 
Take it easy big boy.Fanya kama ulikuwa chuo cha mafunzo ya mapenzi na huo ni mtihani kama utaushinda utakuwa umefaulu.wengi yameshatukuta hayo na tumeyashinda.But time will tell atakuja kukupigia magoti.Kwahiyo fanya kazi zako kwa bidii.4give and 4get
 
Take it easy big boy.Fanya kama ulikuwa chuo cha mafunzo ya mapenzi na huo ni mtihani kama utaushinda utakuwa umefaulu.wengi yameshatukuta hayo na tumeyashinda.But time will tell atakuja kukupigia magoti.Kwahiyo fanya kazi zako kwa bidii.4give and 4get
 
Nitaandika story hii kwa urefu, lakini naomba jikaze uimalize kusoma mpaka mwisho kwani niko katika wakati mgumu sana, najisikia kuua kama sio kujeruhi au vinginevyo.

Nimekuwa nikisikia na kushuhudia watu wakiwaua wapenzi wao au kuwadhuru kwa sababu ya wivu au kutendwa, nikidhani kuwa wana matatizo (emotional problems) kwani nimekuwa muumini wa upole katika maisha yangu, nimekuwa nikiamini kuwa ninapotendwa napaswa nijiondokee zangu sitaki pressure napenda maisha ya amani na pia nimekuwa nikiamini wanawake ni wengi duniani, kwa nini nijihangaishe kwa ajili ya mmoja?. Ila kwa yaliyonitokea nimegundua sio kweli. Kwa yaliyonitokea ingekuwa mwingine nadhani angeshaua au kujeruhi.


Ni kuwa nina mpenzi wangu ambaye anakaa morogoro mimi niko Mbeya kikazi. Yeye ana mtoto mmoja ambaye ilikuwa bahati mbaya. Na baba wa huyo mtoto kwa sasa hata hafahamiki aliko na mtoto yuko la kwanza. Sikuparamia kumpenda binti huyu, nimemfahamu kwa muda na kujifunza tabia zake, nafahamiana na mama yake na hata wadogo zake. Baba yake alishafariki siku nyingi kwa ajali ya gari. Kwa kweli nilivyomfahamu niliridhika kuwa ameshajifunza kuwa maisha si lelemama kwani walikuwa wanapitia wakati mgumu sana. Mama yao hana kazi, na wao pia hawana kazi ya maana, ni ile kusogeza maisha kiugumuugumu tu.

Kabla mama yake hajagundua lolote kuhusu uhusiano wetu ilifika stage mama alikuwa ananipigia simu kuniomba kiasi cha hela kutatua matatizo (ukizingatia tulikuwa karibu sana kifamilia na nilikuwa nawatembelea kuwajulia hali). Wakati natoka unakuta mama ananiambia tufanye maombi, alafu mimi ndo naomba, mama ananiambia niwaombee, hapo anataja matatizo ambayo ninawaombea. Roho yangu ilikuwa inajawa huruma nikawa namsaidia mama kila ninapokuwa na vijihela.

Tulipoanza mahusiano binti alikuwa anakaa kwa ndugu zake Morogoro wakati mama akiwa Dar. Kadiri penzi letu lilivyonawiri, nilizidi kumpenda sana. Ikafika kipindi akapendekeza kuwa apange chumba chake mwenyewe ili tuwe huru kila ninapomtembelea. Nikamkubalia, nikalipa kodi ya chumba, kununua kitanda na mahitaji mengine. Mtoto akaanza shule nikalipa ada.

To make story short, kila ninapomtembelea huwa wakati mwingine nafanya surprize na kwa sababu anakuwa hajajiandaa kisaikolojia, nikifika wakati yeye anahangaika na maandalizi ya ugeni wangu mimi nilikuwa navinjari simu yake nikawa nanotice mawasiliano yenye kutilia shaka. Nikagundua kuwa hapendi mimi kushika simu yake.

KILICHONIFANYA NIANDIKE UZI HUU
Nilipata safari ya kikazi Arusha, nikampigia simu kuwa naenda Arusha ila nitalala Moro ili siku inayofuata nimalizie safari ya Arusha. Akaniambia kuna ndugu zake wamekuja hapo sasa itakuwaje kuhusu mahali pa kulala, pia akasema yuko mp. Nikasema poa isiwe tabu, mii nikanyoosha mpaka Arusha nikijua nitakapomaliza kazi zangu nikitoka Arusha nitapumzika Moro ili tuonane. Ajabu ni kuwa nilimpigia simu kuwa nakuja siku fulani, akasema pouwa. Nikiwa njiani akanitumia sms kuwa wale ndugu waliondoka ila kuna wengine wamekuja tena, akapendekeza tutafute lodge. Nikasema pouwa nikamtumia hela kwa M pesa.

Nilipofika Moro, hakutokea kunipokea, ila kwa kuwa sikuwa na mzigo mkubwa nikajiendea zangu mtaani nikapata lodge nzuri nikalipa 30,000 ya chumba japo nilishamtumia hela ya chumba. Nikiwa room akanitafuta nikamwelekeza. Kweli akaja. Baada ya kupiga mechi round ya kwanza akasema anaenda kumchukua mtoto ampeleke gheto kwake alafu atakuja. Nikasema pouwa. Ila akiwa bafuni anaoga nikashawishika kuishika simu yake nikagundua messages za mapenzi za wanaume wawili tofauti ambazo pasipo na shaka yoyote walikuwa wapenzi.

Alipotoka bafuni akawa mkali kama mbogo hataki nishike simu yake, kaniuliza nani kakuruhusu ushike simu yangu? Nilijikuta nimeshikwa na hasira za kutetemeka. Naye kwa haraka akachukua simu akavaa akaondoka.
Nikitegemea atarudi ndani ya lisaa limoja akawa hatokei kuanzia saa 12 jioni mpaka saa nne usiku, nikimtext anasema anakuja. Ilipofika saa nne akaanza kutoa sababu kibao zisizo na msingi za kusema kuwa hataweza kuja.
Aliniomba msamaha lakini sikumwelewa. Nikalala peke yangu chumbani nikiwa na majonzi. Asubuhi alikuja tena baada ya mimi kumtafuta. Nilichukia haijawahi tokea nikashindwa hata nifanye uamuzi gani. Alipokuja alinikuta nalia machozi kitandani hata leso zangu zililowa machozi, nilijisikia uchungu sana. Akanibembeleza, nilipotulia nikamwuliza kuhusu zle sms nilizokuta, badala ya kujitetea, alinijibu, "Kwanza unieleze huko uliko wewe huna wanawake? "

Sikumbuki vizuri kilichotokea baada ya hapo, ila ninachokumbuka ni kuwa nilijikuta nimefika stendi na kupanda gari. Njia nzima nilitafakari muda niliopoteza kwa huyu binti na kwa familia yake. Alipokuwa katika shida alikuwa anakosa hata 5000, leo hii nimemfikisha hapo alipo, namsomeshea mtoto nikijua tutakuwa mume na mke, namgharimikia kila kitu hata mavazi yake, mama yake namsaidia kwa mengi leo hii yeye yuko na wanaume wengine. Ni majuzi tu tulikuwa tunajadili nimfungulie bishara nimpe mtaji, kumbe mwenzangu ana lingine kichwani, bado utoto haujakutoka.

MY MESSAGE TO THIS LADY
Sawa, i am going off, kwa heri. Ila jua kuwa time is a good judge, Mungu hadhihakiwi.
Sitamwanini tena mwanamke.

Sijui mwana JF wenzangu yangekukuta haya ungefanyaje?

Love begins with a smile, grows with a kiss, and ends with a tear A sad thing in life is, you meet someone who means a lot to you, only to find out in the end that it was never meant to be, and you just have to let go.
 
ndugu yang hata mim yamenikuta kama yako..mim nimeshnwa kuvmilia nataman nimfanye muokota makopo kama itawezekana.
 
saa nyingine mungu anatukutanisha na watu sio ili tukipata watu ndio tuweze kushukuru kwa hilo,na mshukuru mungu unapomwaga chozi kwani unapata kupima umuhimu wa uyo mtu na vile unavyoaanza maisha mapya kisha unachapa lapa,pole sana broh,naweza kuhisi kiasi gani umeumizwa na uyo asiyejitambua
 
Back
Top Bottom