Mmoja kati ya hao wawili aliowakuta katika simu anaweza kua baba wa mtoto. "Damu nzito kuliko maji"
Lakini kusomesha siyo dili sana,mimi nilisomesha kwa mamilioni pia lakini kwa usamalia wema pasipo malipo yoyote na nikasepa kivyangu taratibu. Na mtu yuko serikalini anatumia elimu yake aliyoipata.
Wewe hukufika hata mbali,sasa fatilia vitu muhimu vinayohusu kazi,tena unaonekana unampenda Mungu.
Ingia katika maombi uvuke kikwazo hiki cha kitoto,utapata mwingine au yule yule atarudi kuomba msamaha.
Sasa akirudi ikatokea mumefunga ndoa lazima uwe tayari kukubali yafuatayo:
1.Mtoto wake ana baba mzazi,sasa kama yuko hai kuna siku atakuja kumtafuta mwanae
2.Mtoto huyu atakua na kuanza uliza baba yake yu wapi
3.Mama wa mtoto hata acha kuwasiliana na mzazi mwezie maadam wa namba ya kila mmoja
4.Uwe tayari kumtunza huyu malaika kama mwanao wa kumzaa
Pia usipende kuhesabu uliyomfanyia huyu dada,kwa sababu ndiyo inayokuongezea uchungu moyo mwako bure. Mfano mwingine atasema nimemnulia gari,nyumba,viwanja,shule nimelipa,duka nimemfungulia,alafu anafanya michepuko lazima nimkomeshe.
Pia usisahau hukumuoa bali umemfanya kama chombo cha starehe,wewe ulikua unapiga tu zeze muheshimiwa.
Yako mambo mengi wadau watakuletea humu utajifunza.
Kila lakheri