HAONI Kwa mujibu ya maelezo yako, inaonesha wewe sio mwaminifu ktk ndoa yako!!!
Kwanini ukimbie kupima na mkeo?
Umemuua bure mtoto wa watu!
...
Na ikiwa aliyosema watu8 (..mkeo anajua hali yake but anataka nawe ujijue...) then huyo mkeo hajakuonesha hali yoyote ya kuchukizwa na hayo matokeo, hapo iko namna!
...
My take:
Ongozana na mkeo mukapime tena, ili muanze kutumia dawa na kufuata miko/masharti ya matabibu! Ili muishi kwa matumaini!!!
Just mkapime bila kupoteza mda! Huwezjua pengine wewe and/or mkeo hamujaathirika!
Mkuu yaani out of nowhere aanze tu kutumia kondomu mind mkewe ni mjamzito....sasa hiyo kondomu sijui mkewe akiuliza kwa nini yavaliwa jamaa atajibu nini...
Suala la muhimu ni huyu jamaa kwa kuwa anajua hali yake, akae chini na mkewe na kumueleza. Kuwa na HIV sio ndio kwamba u marehemu...kila mtu ataonja mauti ni vile hakuna ajuaye ni namna gani roho yake itavyochukuliwa.
haya mambo ya ujauzito na vvu au ukimwi noma nilimpoteza dadangu hivihivi kidonda hakijapona.Kila akienda hospital anaambiwa apime harudi hospital ile tena clinic ya mtoto haendi kwenye kuzaa akaenda private sijui alihonga akazaa mtoto kinga hana kitoto kikafariki na yeye kuanza kuumwa hapo ndo tukakamata mchuma fasta kumfata alipo na kumpeleka hospital akaanza dawa na tukambeba kuja nae dar.Akasimama na nguvu akapata akarudi kama zamani.Akarudi mkoa anaokaa sijui ibilisi gani aliyemkumba na wakati dawa zinachululiwa dar mi mwenyewe namtumia na kuna dawa za asili za burundi alikuwa anatumiwa akaacha kumeza dawa sie kuja kupata taarifa kaacha na kuanza kuumwa ndani ya wiki kakonda,kavurugika,kukamata mchuma fasta kumfata mkoa i mi na ndugu yangu mwingine ili kumuangalia apate nafuu turudi nae dar ila haikuwa ridhiki baada ya wiki moja ya kuhangaika kumuokoa akaondoka. HAONI mchukue mkeo haraka sana mkapime hata kama kapima anahitaji support yako sana haijalishi kama majibu positive au negative ila anakuhutaji sana kipindi hiki