Kalumbesa
JF-Expert Member
- Nov 24, 2010
- 1,013
- 356
Kuna rafiki yangu mpenzi ameoa mwanzoni mwa mwaka jana...ni kipindi kirefu sasa amekuwa akiniomba ushauri juu ya mambo kadhaa kwani nami pia nimeoa...ameniambia amekuwa akivumilia sana katika ndoa yake ila kuna wakati huwa anakuwa karibu kufanya mambo ya ajabu kulingana na yale mwenza wake anayotaka...Anadai mke wake anapenda kuwa ana mcontrol ama kuwa na maamuzi juu ya mambo anayotaka kuyafanya...kwa mfano kama anataka kwenda mahali ama kuonana na marafiki zake au kwenda kufanya mazoezi mke wake huwa anakuwa against ama anakataa yeye kwenda kama hakumwambia muda mrefu kabla...yaani anapaswa kuwa alishamueleza mapema...huwa anajaribu kumweleza kuna ubaya gani nikienda kwenye mazoezi?lakini wapi mke huwa mbogo na kutoafiki yeye kwenda..wakati mwingine huwa anampuuza na kwenda ila ndiyo hivyo tena akirudi nyumbani kunawaka moto.ila hujifanya mjinga kuepusha shari...Na pia hata akipigiwa simu na rafiki waonane mke huwa mgumu kukubali hata kama rafiki yule naye anamfahamu..mke anaonekana kutokupenda mume aende mahali peke yake....Jamaa ananiuliza nifanye nini?mke wako anafanya hivi?napata tabu kumjibu maana nahofia kuwa m baya maana nachoweza kuongea kinaweza kumfanya akaharibu ndoa yake ama akanichukia mimi kama nitakuwa upande wa mkewe..nalazimika kumkwepa anapotaka kuniona kwa hili...Wadau nakaribisha mawazo yenu!hasa kwa wenye committed relationship au ndoa..kama bachelors chukulieni kama tatizo la mtu wa karibu siyo kujibu kirahisi kama vile, mwambie amuache...nk..Karibuni!!