Nashindwa kuendelea na masomo kwa sababu ya Aviator

Nashindwa kuendelea na masomo kwa sababu ya Aviator

Sun is Sun

JF-Expert Member
Joined
Mar 13, 2024
Posts
1,213
Reaction score
1,911
Ninaandika ujumbe huu kwa maumivu makubwa sana.

Inaonekana nitalazimika kukatisha masomo yangu kutokana na pesa za ada na matumizi kuishia kwenye mchezo wa AVIATOR.

Mwanzoni niliona kama ni njia rahisi ya kupata hela. Nilianza kwa bet ndogo ndogo, nikishinda mara chache nikajikuta naamini kwamba ninaweza kurejesha kila nilichopoteza.

Kadri siku zilivyokwenda, ndivyo nilivyozidi kuzama. Mwisho wa yote, hela iliyokuwa inategemewa kwa ajili ya elimu yangu imepotea.

Naandika hili sio kuomba huruma, bali iwe fundisho kwa vijana wengine. AVIATOR si mchezo wa kawaida kama wengi wanavyofikiria. Kwa namna nyingi ni aina ya utapeli unaocheza na akili na matumaini ya watu.

Wanakuonyesha ushindi mdogo ili uendelee kuweka hela nyingi zaidi, mwisho wake unapoteza kila kitu.

Kama wewe bado hujaingia kwenye hizi betting, tafadhali usianze. Na kama tayari umeanza, usisubiri mpaka upoteze kitu kikubwa kama elimu, biashara au mahusiano ndiyo uache.

Mwisho wa masomo umetimia.
 
Bro ulikuwa njia moja kuuelekea utajiri, the same njia ya kufata masomo, polee kwa matokeo ila hongera tena kwa ujasir

Jaribu tena katika njia hizo mbili ipo siku utafanikiwa tu

Big up
 
Back
Top Bottom