Nashindwa kuelewa utajiri wa Software developers

Nashindwa kuelewa utajiri wa Software developers

General Mangi

JF-Expert Member
Joined
Dec 21, 2013
Posts
15,316
Reaction score
23,178
Wakuu nashindwa kuelewa utajiri wa Bill gates, Zuckerbarg, mmiliki wa google (android),.
Ukiwatizama matajiri hawa unakuta wamewashinda wamiliki wa makampuni makubwa hapa dunini ambayo bidhaa zao nyingi ni tangible na zinaonekana kwa wingi mtaani mfano Samsung, Toyota, Suzuki, Sony, Air bus, Boeing, wauzaji mafuta , total.

Makampuni haya ni dhahiri kabisa unaziona bidhaa zao mtaani tangu zamani lakini unashangaa eti anapitwa na mtu ambaye kadevelop window ambayo kuinstall kwenye komputa ni kama 20000 tu na baada ya huipo hulipii tenaa. Mfano facebook unakuta hata kwa mwezi hutumii hata MB 500 lakini unaambiwa jamaa ndiye tajiri kuliko mmiliki wa Air Bus. Ukiniambia suala la matangazo sidhani kama ni hoja kuu kwani nashangaa hata wamiliki blogs wanalipwa na google kwa yeye kuweka matangazo yakee.

Naombeni kujua vyanzo vya mapato ambayo Bill gates anauza na kupata ela ambayo inamzidi mmikili wa Sansung au Apple.company. Android OS ni bure lkn google eti anaela kushinda mmiliki wa HTC au LG, hapa nashindwa kuelewaa kabisaa.
 
Hayo makampuni yote uliyoyataja, ya magari, ujenzi, viwanda nakadhalika, wanatumia software kuendesha shughuli zao na uzalishaji. Hakuna jinsi watakwepa kutumia huduma za hao software developers kwa njia moja ama nyingine. Dunia ya sasa inatulazimisha kutumia zaidi software ili kuongeza ufanisi na kuboresha utendaji wa kazi zetu.
 
Hata Facebook?
 
b5d45985296b399d5c07ec71ed23e1a6.jpg

Utajiri mara nyingi husaidiwa na u"unique" wa kitu. Bill Gates utajiri($78bill as of august) wake wote unatokana na Microsoft.. hajarithi wala nn ( he is a self-made billionaire)

Mark zuckerberg (54.5 bill usd)
620x434.jpg

Utajiri wake unatokana na facebook. Na yy ni self made billionea

Computer programming na internet entrepreneurship ndo mpango mzima..

Chukulia mfano Jack dorsey ,
BN-LU614_square_G_20151221105855.jpg

CEO wa twitter( 1.16 bill usd) anadeal na Programming. Japokuwa kulikuwa na tetesi kwamba anataka kuiuza kama yahoo alivofanya, maana revenue zinashuka mwaka hadi mwaka kama

Jamaa mwingine anaitwa Travis Kalanick
2Q==.jpg

founder ba CEO wa Uber. (6.2 bill usd as of august 2015 ) yy alitengeneza app inaitwa uber. Hii app dreva yeyote anaitumia kutafta wateja kwa wepesi ikamtajirisha japokuwa china pamemshinda..
Z.jpg

Elon Musk ( 11.6 bill usd)
9k=(2).jpg

CEO wa tesla motors.. na yy ni mambo ya software. Anahusika na utengenzaji wa magari yenye auto-pilot. kashauriwa mara kibao aachane na hiyo feature ya autopilot..lakini kagoma. anajua pesa na brand ya kampuni yake iko kwene hiyo software ya auto pilot model kama tesla model x( price usd 74,000-) na model S ( price yake inaanzia usd 66,000)za 2016.
9k=.jpg

9k=(1).jpg
 
Google kuna matangazo.

Facebook pia kuna matangazo.

Instagram pia kuna matangazo.

yote hayo unalipia

Haya matangazo unaweza kuona kama nikitu kidogo ila yana walipa kupita unavyofikiri.
 
pesa inaingiaje?
mfano mimi naweka bando la jero, kuanzia vodacom, tcra mpaka marck zuck google na wengineo hio hela wanaichukuaje?
 
pesa inaingiaje?
mfano mimi naweka bando la jero, kuanzia vodacom, tcra mpaka marck zuck google na wengineo hio hela wanaichukuaje?
Namimi pia mkuu ninahamu ya kujua jibu la swali lako..
 
umesahau mkuu hao wamiliki wa facebook, microsoft n.k pia wanamiliki na hardware mfano simu computer na biashara kibao, hawaja base kenye kitu kimoja tuu bali vingi. ila hakuna ubishi software inawalipa zaid,
siku hizi hila kitu kinakua operated by software hata magari sasa yanakua controled by software.
Makampuni mbali mbali yanategemea software kuhifadhi na ku share data mfano database, server, website, apps n.k
hakuna mtu anaehangaina tena na kubeba maboksi na madaftari kwa ajili ya kuhifadhi nyaraka. kwa sasa kila kitu kinakua saved in softcopy/software form na ni nia rahisi.
 
pesa inaingiaje?
mfano mimi naweka bando la jero, kuanzia vodacom, tcra mpaka marck zuck google na wengineo hio hela wanaichukuaje?
Wanaweka matangazo ndio wanolipa, namna mtandao unavyokua na watumiaji wengi duniani ndio namna wafanyabiashara wengi wanavyouhitaji kuweka matangazo yao
 
Wanaweka matangazo ndio wanolipa, namna mtandao unavyokua na watumiaji wengi duniani ndio namna wafanyabiashara wengi wanavyouhitaji kuweka matangazo yao
ila sitaki kuamini kua matangazo tuu yanawalipa, kuna kingine!
 
pesa inaingiaje?
mfano mimi naweka bando la jero, kuanzia vodacom, tcra mpaka marck zuck google na wengineo hio hela wanaichukuaje?
Revenue yao kwa upande mkubwa inatokana na matangazo. Unakuta anaeza pokea zaidi ya $ 1billion per quarter. Na hivo kupelekea value ya fb kuwa zaidi ya $100 billion.

Kuna ads zinaitwa targeting ads. Ziko based kwene information ulizoandika fb mfano unachopendelea kufanya, chakula n.k

Facebook ina spenders wakubwa kama;
- FORD
Hii kampuni inaamini kwamba mtu aki "like" kwene fb, inakuwa advocate wa iyo brand kwani watu wataona kwamba fulani ka"like" maybe gari jipya la ford.

-HSBC
hii ni bank na inatangazwa sana fb upande wa Asia na Europe

-ANHEUSER-BUSCH INBEV
mnamo mwaka 2010, Budweiser alotoa offer ya "bia za bure" kwa mtu yeyote aliekuwa anafikisha umri wa miaka 22

-MCDONALD'S
ina likes zaidi ya million 30 (survey data 2010)

-VISA
ilitumia pesa nyingi kujitangaza fb olympics 2012
Wengine ni pamoja na
-NIKE
-JPMORGAN CHASE
-STARBUCKS
-DISNEY
-DELL
-SAMSUNG
-NESTLE
-UNILEVER
-VERIZON
-GOOGLE
-WAL-MART
-GROUPON
-AMERICAN EXPRESS
-AT&T
-ELECTRONIC ARTS
-ZYNGA

HIZO KAMPUNI ZINALIPIA NN?
Japokuwa fb inakaribisha advertisers wa size yeyote, wote wako after the same thing, "likes and shares"
Gharama ya matangazo inarange kuanzia 5 cents to 5 dollars per click. ( yaani mtu anapo"like au kushare")
Gharama hupanda depending on targeting, bids na engagement

Sidebar ads
-ndo most common adds fb. cost yake ni about $1-$5

Sponsored stories
-hizi ni status updates za makampuni ambazo hugeuzwa kuwa ads. Cost yake ni 50cents per click

Promoted posts
Posts zilizowatajet fans and friends of fans. Cost ni $5 per every 1000 people targeted.

Source:
http://money.msn.com
Http://readwrite.com
Http://www.businessinsider.com
Http://ppbh.com
Http://www.techvibes.com
Http://www.marketwatch.com
And business-management-degree.net
 
Mimi jambo linalo nishangaza ni kampuni kama apple kuwa na ela nyingi kuliko makampuni kama Toyota, kampuni ya lambourgine kampuni hadi za kuunda ndege kisa hivi vilaptop na simu.
Wechat nasikia nayo inaingiza ela nyingi sana
 
Mabilionea wa Arusha nao vepeee?
Ina maana software ina utajiri zaidi Ya jiwe?
 
Wakuu nashindwa kuelewa utajiri wa Bill gates, Zuckerbarg, mmiliki wa google (android),.

Makampuni haya ni dhahiri kabisa unaziona bidhaa zao mtaani tangu zamani lakini unashangaa eti anapitwa na mtu ambaye kadevelop window ambayo kuinstall kwenye komputa ni kama 20000 tu na baada ya huipo hulipii tenaa. Mfano facebook unakuta hata kwa mwezi hutumii hata MB 500 lakini unaambiwa jamaa ndiye tajiri kuliko mmiliki wa Air Bus.
.
Nanikakudanganya ndugu, ushawahi nunua window OS mpya dukani???? achana na hizi za kuchakachua za buku 10!!! windows OS mpya ni zaidi ya laki moja, ukija kwenye microsoft office nayo ni zaidi ya laki!!! ila sema kwa kuwa sisi ni wabongo tunachakachua, sijui siku wakiamua kufungia windows zilizochakachuliwa itakuwaje?? nadhani utajifunza ubuntu bila kupenda!!!
 
Sio nje tu, angalia hii tender ya asasi moja ya kiserikali ilingia na oracle ndio utajua software ni ghali sana [HASHTAG]#GEPF[/HASHTAG]
Its about TSH 37,093,870,060 utajiri wa software knowledge ni zaidi ya mgodi wa gesi
 
Attachments

  • oracle.png
    oracle.png
    3.2 KB · Views: 44
Nanikakudanganya ndugu, ushawahi nunua window OS mpya dukani???? achana na hizi za kuchakachua za buku 10!!! windows OS mpya ni zaidi ya laki moja, ukija kwenye microsoft office nayo ni zaidi ya laki!!! ila sema kwa kuwa sisi ni wabongo tunachakachua, sijui siku wakiamua kufungia windows zilizochakachuliwa itakuwaje?? nadhani utajifunza ubuntu bila kupenda!!!
ndo kwanza najua hii.ila mbona kwenye official site ya microsooft wameweka bei halisi za window zao?
 
Mimi jambo linalo nishangaza ni kampuni kama apple kuwa na ela nyingi kuliko makampuni kama Toyota, kampuni ya lambourgine kampuni hadi za kuunda ndege kisa hivi vilaptop na simu.
Wechat nasikia nayo inaingiza ela nyingi sana
kimapato toyota, samsung na makampuni mengi yanaipita apple, kwenye faida ndio hawamfikii sababu apple hafanyi research, hafanyi sana matangazo na bidhaa zake zina specs ndogo na bei kubwa.

mapato ya toyota bilioni 252 za kimarekani
Apple mapato yake bilioni 233 za kimarekani
samsung mapato yake bilioni 305 za kimarekani

kwenye faida apple anapata hadi 25% ya mapato
 
Nanikakudanganya ndugu, ushawahi nunua window OS mpya dukani???? achana na hizi za kuchakachua za buku 10!!! windows OS mpya ni zaidi ya laki moja, ukija kwenye microsoft office nayo ni zaidi ya laki!!! ila sema kwa kuwa sisi ni wabongo tunachakachua, sijui siku wakiamua kufungia windows zilizochakachuliwa itakuwaje?? nadhani utajifunza ubuntu bila kupenda!!!
ukinunua laptop au desktop unalipia windows japo we hujui, labda ununue laptop ya dos au ubuntu. makampuni kama Lenovo, dell, hp etc humlipa microsoft kama dola 40 hivi kwa kila computer ya windows wanayouza. na ikiwa na windows kama pro, ultimate au enterprise bei huongezeka
 
Back
Top Bottom