Nashauri waziri Magufuli ashtakiwe

Nashauri waziri Magufuli ashtakiwe

Alifuata utaratibu ambao hautoi tija. Pesa ni mazungumzo yoote. Najua mahakama hebu fuatilia kwa makini wangapi hawana pesa wamekosa haki. Na je serikali itoe pesa ili ishinde kesi? Kwa serikali nani? Ni binadamu wanaiongoza wanahitaji dhamira na uzalendo.
 
Aliyeimba Nchi ya watu wadogo , Nchi ya kiyu kidogo ukitaka chai mama nunua katepa! Nadhani alituimbia watanzania na ka nchi ketu kakugikirika. Yaani Shamba la bibi.
 
Sidhani kama magufuli amefanya kosa!nafikiri mawakili na wanasheria Wa serikali waliosimamia hiyo kesi ndio wanaotakiwa wakamatwe.muacheni magufuli asimamie ujenzi Wa miundombinu ili mikiandamana muandamane kweny Lami!
 
Haiingii akilini kwa kesi yenye maslahi makubwa kwa serikali yetu kama hii ya samaki waliokamatwa kwenye meli iliyovua kweny bahari yetu bila kibali, kuambiwa kuwa serikali imeshindwa kesi na hivyo serikali yetu inadaiwa matilioni ya pesa.

Yaani mwizi atuibie harafu tumlipe matilioni na amekamatwa na kidhibiti. Kwangu naona kuna haja serikali ifanye uchunguzi wa wanasheria wake waliosimamia kesi hii isije ikawa tumehujumiwa ili kuiangusha serikali na wao wale cha juu.

Swali kwa wanasheria wa serikali: je kwa nn katk kesi nyng zinazoikutanisha serikali na watu binafsi, kwa asilimia kubwa watu binafsi wanashinda.

Je, serikali inaajiri incompetent lawyers ukilinganisha na mawakili binafsi? au serikali inawakwamisha katika kusimamia kesi.

Jamani tukumbuke na ile kesi ya Dowans kama siyo richmond tulivyoshndwa. Nakaribisha mchango naona kuna kitu hapa au labda ni uelewa wangu mdogo, naomba nifunguliwe macho.
 
Kama ulistaajabu ya Richmond, yaone ya "Samaki wa Magufuli" sasa.

Toka lini Mwanasheria wa Tanzania akasimamia maslahi ya Tanganyika na akashinda? Ndiyo maana sisi wananchi tunataka Tanganyika ili tusimamie rasilimali za nchi yetu wenyewe, tuna uchungu nazo.
 
tanzania haina wanasheria hao ni maboga tu. Haiwezekani kila kesi tunashindwa
 
Kama tumeshindwa kesi Mh Magofuli ajiuzulu kwani ndie waziri aliyekuwa na dhamana wakati meli inakamatwa. Huo ushahidi wa kusema meli haikuvua samaki kwenye eneo letu umetoka wapi? Kwanza hakimu na wanasheria walienda eneno la tukio? Wanasema walikuwa hawakuwa wameshusha nyavu baharini wakati wanakamatwa je walisema samaki waliwavua wapi? Wanasema kibali cha kuvua kwenye bahari ya Tanzania kilikuwa kimekwisha muda wake! Jamani tuache kulala usingizi tunapigwa bao na kitu kilicho wazi kabisa?

Uzembe wa meli kuzama ni wetu na hapo wahusika wawajibishwe.

Faini yenyewe hatuna uwezo wa kulipa matokeo yake tutaambiwa tuwape kibali cha kuvua kwenye maji yetu bila kikomo! TZ kweli shamba la bibi!
 
Hii ni fedheha kubwa sana kwa Taifa lakini ajabu ni kuwa inaonekana kuwa jambo sahihi, angalia Walimu wakienda Mahakamani kuiwekea Serikali pingamizi la kudai maslahi yao.

Hao wanasheria basi haraka utasikia utaratibu umekiukwa sasa kwenye hili la samaki sijui ndiyo wanaona sheria imechukua mkondo wake ila upo umuhimu wa "Kuwachunguza"!
 
tanzania haina wanasheria hao ni maboga tu. Haiwezekani kila kesi tunashindwa

Acha ulevi,mpaka kesi inamfikia mwanasheria,kuna mengi yametokea,wewe umeangalia mtiririko wa ushahidi? Kwa taarifa yako si kazi ya mwanasheria kupika ushahidi ila kazi yake ni kuisadia mahakama kufikia maamuzi ya haki, na wala sio kuilazimisha,na anayeamua kesi ni jaji sio mwanasheria. Kuna kesi ngapi tunazijua serikali inajenga shule eneo la mtu bila fidia ikienda mahakamani inashindwa? Hata hiyo ya samaki ni kesi za wanasiasa kulazimisha ziende mahakamani wakati mwingine bila kusikiliza ushauri wa wanasheria ili kufuta aibu. Kwa akili zenu serikali ikifungua kesi lazima ishinde? Ili nani ashindwe? Raia? Kama ni hivyo ni bora mahakama zisiwepo na iwe inashinda moja kwa moja. SERIKALI KUTOKANA NA MABAVU YAKE HUWA INAKUWA IMESHAHARIBU KILA KITU NA WAKILI WA SERIKALI HUWA AKIENDA MAHAKAMANI MARA NYINGI ANA MITIGATE TU,ANAPUNGUZA MAKALI YA MAAMUZI
 
Ni bora hata kuwanyongelea mbali vinginevyo ibinafsishwe,hapo kuna watu wameshavuta chao si unajua tena hili shamba la bibi,Nchi gani inaweza ruhusu upuuzi kama huu.
 
Acha ulevi,mpaka kesi inamfikia mwanasheria,kuna mengi yametokea,wewe umeangalia mtiririko wa ushahidi? Kwa taarifa yako si kazi ya mwanasheria kupika ushahidi ila kazi yake ni kuisadia mahakama kufikia maamuzi ya haki, na wala sio kuilazimisha,na anayeamua kesi ni jaji sio mwanasheria. Kuna kesi ngapi tunazijua serikali inajenga shule eneo la mtu bila fidia ikienda mahakamani inashindwa? Hata hiyo ya samaki ni kesi za wanasiasa kulazimisha ziende mahakamani wakati mwingine bila kusikiliza ushauri wa wanasheria ili kufuta aibu. Kwa akili zenu serikali ikifungua kesi lazima ishinde? Ili nani ashindwe? Raia? Kama ni hivyo ni bora mahakama zisiwepo na iwe inashinda moja kwa moja. SERIKALI KUTOKANA NA MABAVU YAKE HUWA INAKUWA IMESHAHARIBU KILA KITU NA WAKILI WA SERIKALI HUWA AKIENDA MAHAKAMANI MARA NYINGI ANA MITIGATE TU,ANAPUNGUZA MAKALI YA MAAMUZI

Wewe ni mburura wa mwisho kabisa usiyejua kitu,embu tuambie kesi gani yenye maslahi ya taifa hawa wanasheria wa serikali wamesimamia na wakashinda?
 
Wewe ni mburura wa mwisho kabisa usiyejua kitu,embu tuambie kesi gani yenye maslahi ya taifa hawa wanasheria wa serikali wamesimamia na wakashinda?

Mwanasheria makini anakupa ushauri wote,angle za kushindwa na kushindwa, na mwanasheria hana ubavu wa kubadili facts ambazo mwisho wa siku ndizo huamua kesi, na hasa mwanasheria wa serikali ambae anabanwa na sheria na kanuni awe muadilifu. Nenda kachukue hukumu na mwenendo wa kesi uumwage hapa tuuchambue kurasa kwa kurasa kuliko kuongea kama uko kwenye dimbwi la mlenda wa tabora
 
Haiingii akilini kwa kesi yenye maslahi makubwa kwa serikali yetu kama hii ya samaki waliokamatwa kwenye meli iliyovua kweny bahari yetu bila kibali, kuambiwa kuwa serikali imeshindwa kesi na hivyo serikali yetu inadaiwa matilioni ya pesa. Yaani mwizi atuibie harafu tumlipe matilioni na amekamatwa na kidhibiti. Kwangu naona kuna haja serikali ifanye uchunguzi wa wanasheria wake waliosimamia kesi hii isije ikawa tumehujumiwa ili kuiangusha serikali na wao wale cha juu. Swali kwa wanasheria wa serikali: je kwa nn katk kesi nyng zinazoikutanisha serikali na watu binafsi, kwa asilimia kubwa watu binafsi wanashinda. Je, serikali inaajiri incompetent lawyers ukilinganisha na mawakili binafsi? au serikali inawakwamisha katika kusimamia kesi. Jamani tukumbuke na ile kesi ya Dowans kama siyo richmond tulivyoshndwa. Nakaribisha mchango naona kuna kitu hapa au labda ni uelewa wangu mdogo, naomba nifunguliwe macho

Mara kwa mara mimi hukutwa na hali hii kwamba nawaza jambo Fulani nifanye kesho yake, nikiamka nakuta tayari kuna mtu kafanya vile nilivyowaza. Hakika ndivyo ilivyo kwa thread hii. Tanzania nchi yangu unahujumiwa na wananchi uliowaamini sana, haiingii akilini wizi ufanyike kwa ushahidi uliowazi halafu mtuhumiwa asikutwe na hatia. Mhimili wa mahakama unahujumu nchi, hili kamwe halikubaliki. Wanasheria mmeaminiwa kutetea nchi badala yake mnatetea wahalifu na uhalifu wao na kulitia hasara taifa kulipa deni kubwa kiasi hicho. Kamwe msidhani hili litaisha bila nyie kuwajibishwa.
 
Kama ulistaajabu ya Richmond, yaone ya "Samaki wa Magufuli" sasa.

Toka lini Mwanasheria wa Tanzania akasimamia maslahi ya Tanganyika na akashinda? Ndiyo maana sisi wananchi tunataka Tanganyika ili tusimamie rasilimali za nchi yetu wenyewe, tuna uchungu nazo.

Mkuu matatizo ya Watanzania, ni deal kwa viongozi (wa Serikali ya CCM)
 
Back
Top Bottom