Kimbunga
Platinum Member
- Oct 4, 2007
- 14,952
- 10,037
Habari kubwa kwenye media kwa sasa ni kushinda kesi kwa Wachina &WaVietnam waliokamatwa kwa kile kilichodaiwa uvuvi haramu, mwaka 2009 maarufu kama "samaki wa Magufuli"
Freemedia wanaripoti hivi;
" MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu imewaachia huru Wachina wa samaki wa Magufuli na kuamuru Jamhuri iwarejeshee vitu vyao ikiwemo meli ya Tawaliq 1.
Wachina hao Nahodha wa meli, Hsu Chin Tai na Wakala wa Meli ya Tawaliq 1, Zhao Hanquing waliachiwa kupitia hati ya Nole ya kuwaondolea mashitaka.
Hii ni mara ya pili kwa Wachina hao kuachiwa kwani mara ya kwanza waliachiwa na Mahakama ya Rufaa Machi 28 mwaka huu, walikamatwa tena na kushtakiwa upya kwa mashtaka hayo hayo yaliyofutwa.
Washtakiwa hao walikuwa wakikabiliwa na mashtaka ya uvuvi haramu katika Ukanda wa Uchumi wa Tanzania."
Ningekua Rais wa nchi hii ningemfukuza kazi Magufuli na kumshtaki mahakamani. Alichofanya ni ujinga wa kiwango cha juu kupata kutokea tangu enzi za Pontio Pilato.
Huwezi kufanya siasa kwenye mustakabali wa maisha ya watanzania ili tu upate umaarufu.
Alikuja na Mbwembwe za kukamata meli ya waVietnam, kuwapeleka mahakamani na kuwanyang'anywa samaki wao.
Matokeo yake ni kuwa mahakama imeshindwa kuwatia hatiani. Hivyo wameachiwa huru na Mahakama imeagiza tuwalipe meli yao na samaki zao, vyote vikikadiriwa kuwa jumla ya Tsh.Bil 27.
Meli yenyewe nasikia ilizama. Yaani baada ya kutafuna samaki tukazamisha meli.
Habari zinasema Kuzama kwa meli hiyo kunatokana na Serikali kupitia Wizara ya Mifugo na Uvuvi kushindwa kuitunza tangu ilipokamatwa Machi 8, 2009 ikiwa na tani 293 za samaki aina ya Jodari wanaodaiwa kuwavua katika Bahari ya Hindi ukanda wa kiuchumi wa Tanzania (EPZ).
Lakini hata hao samaki hatukuwafaidi maana waliishia kugawanywa hovyohovyo tu. Samaki hao wanaokadiriwa kuwa na thamani ya zaidi ya shilingi bilioni mbili wote waligawiwa katika taasisi mbalimbali baada ya Magufuli kudai kuwa Serikali haiwezi kufanya biashara.
Bili.27 tunazotakiwa kuwalipa hao WaVietnam ni fedha nyingi sana. Ni sawa na kulipia mikopo wanafunzi 57,446 (kwa semister moja) au kulipa madai yote ya waalimu nchi nzima.
Imeripotiwa kuwa mwaka huu wanafunzi zaidi ya 28,000 watakosa mikopo kwa sababu serikali imedai haina hela. Lakini hela hizi za kuwalipa wa-Vietnam zingetosha kuwalipia wanafunzi wote waliokosa mkopo mwaka huu na ikabaki chenchi ambayo ingetosha kulipia madai ya waalimu wote nchini.
.!
Mkuu pamoja na hoja zako nyingi lakini naona jazba imelitawala bandiko lako. Huenda ni kweli Magufuli alifanya siasa lakini yeye si mwanasheria. Sifahamu kama unajua mchakato wa kumshitaki mtu hasa kwenye makosa ya jinai.
Katika hili mimi nilitegemea lawama kubwa ingetupwa kwa DPP kwa sababu ndiye aliyekubali shauri hilo liende mahakamani na ndiye huyo huyo aliyetoa nolle prosequi hii ambayo imewaachia huru wachina. Hii hati mara nyingi hutolewa baada ya kuona ya kwamba huna ushahidi wa kutosha kuendelea na kesi.
Je wakati DPP anaipeleka kesi mahakamani hapo awali na serikali ikashindwa hakuangalia ushahidi kabla ya kuchukua uamuzi? Kama Magufuli alifanya siasa, je na DPP naye aliingia katika siasa na kuacha sheria?
Naona unamuonea bure Magufuli kwa kusema ati aliwapeleka wachina mahakamani! Magufuli hana uwezo kisheria kuwapeleka watuhumiwa wa jinai mahakamani hata kama angependa waende mahakamani lazima ruhusa itolewe na DPP baada ya kutathimini ushahidi wa shitaka husika.
DPP alitoa ruhusa kesi ikaenda mahakamani, prosecution side ikashindwa kutoa ushahidi pasipo na shaka kuishawishi mahakama kuwatia hatiani wahusika. Kisha huyo huyo DPP anatoa Nolle Prosequi kwamba haendelei na kesi!!
Hukuwafaidi samaki!!!!?