Red Giant
JF-Expert Member
- Mar 9, 2012
- 15,658
- 20,889
Wakuu baada ya kula ugali, nyanya chungu, bamia, dagaa, kabichi, maharage, nyama roast na kushushia pepsi big nimepata wazo.
Hili suala la mtoto kumshika mtu mzima wakati wa kusalimia naona kama halijakaa sawa. Naona kama linamjengea mtoto tabia ya kutojiamini, uoga na kumshusha thamani.
Pia ni usumbufu mtu kuanza kuinama usalimiwe.
Nasikia wenzetu wamasai huwa mkubwa ndiyo anasalimia kwa kumshika mdogo kichwani, hii kidogo imekaa poa. Hata baraka hutolewa kwa kushikwa kichwani sasa inakuwaje mtu mzima kupewa baraka na mdogo badala ya mkubwa ndiyo kumpa mdogo baraka?
Napendekeza tusalimiane na watoto kwa kushikana mikono au kwa kuwashika kichwani kama wanavyofanya wamasai. Au nakosea ndugu zangu?