Nashauri walimu wapewe kiapo ili kuongeza ufanisi zaidi

Askari Muoga

JF-Expert Member
Oct 22, 2015
6,113
4,655
Mimi nawalaumu sana walimu wa serikali na ninawajua asilimia kubwa ni wavivu na wanafundisha kama hawataki hivyo serikali iwape kiapo walimu waweze kuapa

Pia nashauri ifikie hatua muwafanyie interview au usaili, pia wakuu wa shule wabanwe sana waweze kuwasimamia
 
Kima cha chini ualimu kiwe 1.2m/- halafu mfumo mzima wa ualimu uwe overhauled; nafasi zitangazwe upya, wafanyiwe interview then watakao-qualify waajiriwe kwa mikataba ya miaka minne-minne (kwa case ya O-Level) ambayo itakuwa renewed based on performance.

Pili miundombinu iboroshwe - madarasa/mabweni/vyoo na kila shule iwe na maktaba na maabara zenye vifaa vinavyotakiwa. Wanafunzi wajengewe moralii ya kusoma - wale wa bweni - chai/mkate asubuhi; uji saa nne; ugali/wali/maharage/mboga za majani mchana; ugali/wali/makande/maharage/nyama/mboga za majani jioni.

Huo ndio "muujiza" unaotakiwa; utaona mabadiliko; otherwise tukienda kwa mazoea ya "matundu ya vyoo" ni kilio kila mwaka.
 
Wewe mtoa hoja kwa mshahara upi mpaka wapewe kiapo hata kama wakiapa hawezi kuongeza ufanisi
 
Mimi nawalaumu sana walimu wa serikali na Nina wajua asilimia kubwa ni wavivu na wanafundisha kama awataki ivyo serikali iwape kiapo walimu waweze kuapa pia nashauri ifikie hatua muwafanyie interview au usaili, pia wakuu wa shule wabanwe sana waweze kuwasimamia
unajua nn mkuu?..walimu wanaofundisha private na kutoa one nying wamesoma chuo kimoja na wanaofundisha serikalini na kutoa sifuri nyingi...tena cha kufurahisha hata quarification zao za kuingia chuo zinafanana(kuna watu wansema walimu wameferi)...swali linakuja sasa...kwa nini hawa wa serikali wanashindwa kufaurisha na wa private wanafaurisha?...apo ndipo utakapopata jibu kwamba elimu sio MWALIMU tu...inahusisha mambo mengi...
 
Mimi nawalaumu sana walimu wa serikali na Nina wajua asilimia kubwa ni wavivu na wanafundisha kama awataki ivyo serikali iwape kiapo walimu waweze kuapa pia nashauri ifikie hatua muwafanyie interview au usaili, pia wakuu wa shule wabanwe sana waweze kuwasimamia
walipeni madai yao, wapandishe madaraja kwa muda na usiwatese na kuwanyanyasa huko kwenye halmashauri zenu; kisha uwape kiapo cha kujituma zaidi.
 
Mimi nawalaumu sana walimu wa serikali na Nina wajua asilimia kubwa ni wavivu na wanafundisha kama awataki ivyo serikali iwape kiapo walimu waweze kuapa pia nashauri ifikie hatua muwafanyie interview au usaili, pia wakuu wa shule wabanwe sana waweze kuwasimamia
Unategemea ng'ombe ambaye haumpi matunzo bora akupe mazao bora!!
 
Mimi nawalaumu sana walimu wa serikali na Nina wajua asilimia kubwa ni wavivu na wanafundisha kama awataki ivyo serikali iwape kiapo walimu waweze kuapa pia nashauri ifikie hatua muwafanyie interview au usaili, pia wakuu wa shule wabanwe sana waweze kuwasimamia
Pia jaribu kuwianisha kiwango cha mshahara na mazingira ya kazi ya mwl wa kaizirege na feza ..na huo wa serikali yako. Halafu tegemea maajabu ya kiapo hivyohivyo
 
Hizi skuli za kata mkiani ni halali yao unategemea ulime magugu uvune mahindi? Kama nidhamu chafu katika skuli hizi inalindwa unategemea ufaulu utoke wapi?
 
Mimi nawalaumu sana walimu wa serikali na ninawajua asilimia kubwa ni wavivu na wanafundisha kama hawataki hivyo serikali iwape kiapo walimu waweze kuapa

Pia nashauri ifikie hatua muwafanyie interview au usaili, pia wakuu wa shule wabanwe sana waweze kuwasimamia
yaaani upo ubungo mataa unaenda Mwanza halafu mawazo yako hayajavuka hata jengo la Tanesco makao makuu
 
Afundishe kwa kujituma anayeshiriki mvinyo wa Taifa in terms of posho ila tusikuwa na haki ya kushiriki mvinyo tuendelee kuuza barafu na kashata kwa watoto.
 
Na wnafunzi waendelee kushinda whatsup, insta . Au na wao wakachukulie matokeo yao mahakamani
 
Wabunge wamekula viapo tena kwenye mavazi ya heshima, ndani ya jengo lenye heshima pale Dodoma lakini bado baadhi yao hawana ufanisi wowote na hata majimboni hawaonekani. Msifanye maisha yazidi kuwa magumu kwa walimu zaidi ya ilivo hivi sasa, kuna measures nyingne za kukuza elimu ila kwa kula kiapo sidhani kama its worth it.
 
Mimi nawalaumu sana walimu wa serikali na ninawajua asilimia kubwa ni wavivu na wanafundisha kama hawataki hivyo serikali iwape kiapo walimu waweze kuapa

Pia nashauri ifikie hatua muwafanyie interview au usaili, pia wakuu wa shule wabanwe sana waweze kuwasimamia
Je na wanafunzi waliojaa viburi wawafanyeje? Mi natamani viboko vingerudishwa tu. Mitoto imekuwa mbumbu, inaona bora kuwa teja la unga kuliko kusoma, inadhani manchester united ni muhimu zaidi ya masomo, inawajua marefa zaidi ya walimu wake.
 
Wapewe mshahara kama wa mbunge na walipwe kiinua mgongo kila baada ya miaka mitano,kusha anayetaka kuendelea kuwa mwalimu aombe miaka mingine mitano.
Mwalimu mmoja afundishe wanafunzi 45 darasani kila akiingia kwenye kipindi.
 
Back
Top Bottom