Nashauri vyeo hivi vifutwe!

MwanaFalsafa1

JF-Expert Member
Joined
Feb 26, 2008
Messages
5,566
Points
1,195

MwanaFalsafa1

JF-Expert Member
Joined Feb 26, 2008
5,566 1,195
Mimi naona imefika wakati tuamue moja na kufuta cheo kimoja kati ya makamo wa raisi au waziri mkuu. Sioni mantiki ya kuwa na vyeo vyote hivi kwa wakati mmoja. Naamini kabisa waziri mkuu anaweza akafanya kazi ya makamo wa raisi na makamo wa raisi anaweza akafanya kazi ya waziri mkuu. Sasa kuna maana gani kuwa na vyeo vyote hivi?

Nasema hivi kwa sababu mara nyingi vyeo vyote hivi viwili vikiwepo mara nyingi inaashiria nchi hiyo ina mgogoro fulani wa kisiasa na cheo kimoja kimewekwa ili mtu wa "upande wa pili" kupewa. Mfano ni Kenya kuanzisha cheo cha waziri mkuu baada ya uchaguzi wa 2007 ili Raila Odinga apewe nafasi hiyo na Zimbabwe ambapo alipewa Morgan Tsavangirai. Naweza kusahihishwa lakini kichwani hainijii nchi yoyote isiyo kuwa na mgogoro wa kisiasa ambapo vyeo vya makamo wa raisi na waziri mkuu vyote vipo.

Kwa Tanzania mimi naona bora cheo cha makamo wa raisi kifutwe kabisa kwani hamna la maana makamo wa raisi analo fanya zaidi ya kuwa kiongozi "ceremonial" anaeitwa kukata utepe na kuzindua vitu. Najua katiba inasema raisi akitoka upande mmoja wa muungano basi sharti makamo atoke upande wa pili. Hilo halina neno kwani tunaweza kusema raisi akitoka upande mmoja wa muungano basi waziri mkuu atoke upande wa pili.

Sababu ya pili nashauri nafasi ya makamo wa raisi ifutwe ni kwa sababu japo kiprotokali cheo cha makamo wa raisi ndicho cha pili kwa ukubwa kiutendaji waziri mkuu ana nguvu zaidi kuliko makamo wa raisi. Pia waziri mkuu kama mtendaji mkuu wa serikali ina maanisha ana nafasi nzuri zaidi ya kukaimu kiti cha uraisi endapo raisi hayupo au ana hali inayo mzuia kufanya shughuli zake.

Pili napenda kushauri nafasi za naibu waziri nazo tuzifutie mbali. Zina jaza tu ukubwa wa baraza wakati kazi ya naibu waziri inaweza ikafanywa vizuri tu na katibu mkuu wa wizara husika. Pale waziri ambapo hayupo nani anaefaa zaidi kuendesha shughuli za serikali kama si katibu mkuu wa wizara?

Mwisho ningependa pia kushauri nafasi za waziri wa nchi zifutwe kwani hazina matiki zozote. Naamini kabisa shughuli zinazo fanya na waziri wa nchi zinawezwa wekwa zikawa chini ya idara ya wizara kamili.

Nazani imefika wakati tupunguze hizi nafasi za "zawadi za kisiasa" na tubaki na zile ambazo kweli tuna zihitaji katika uendeshaji wa serikali yetu. Nawakilisha.
 
fikramakini

JF-Expert Member
Joined
Nov 27, 2010
Messages
247
Points
0

fikramakini

JF-Expert Member
Joined Nov 27, 2010
247 0
Nakuunga mkono mkuu.

Hivi majuzi nilishangaa kuona Waziri mkuu alishindwa kumchukulia hatua Jairo eti hadi awasiliane na Raisi. Hivi Raisi akisafiri anamwachia nchi nani kati ya makamu na waziri mkuu? Maana kama anamwachia waziri mkuu, basi mzee mzima pinda alikua ana mamlaka ya kumchukulia hatua jairo moja kwa moja ... ila kama anamwachia makamu wa rais, nilitegemea pinda awasiliane na makamu wa raisi ili hatua stahiki zichukuliwe.

Hii inanichanganya kiasi naona bora nafasi mojawapo ifutwe kweli ...
 
Mzee

JF-Expert Member
Joined
Feb 2, 2011
Messages
13,464
Points
2,000

Mzee

JF-Expert Member
Joined Feb 2, 2011
13,464 2,000
Kwa hapa kwetu naona waongeze makamu wa makamu wa rais. Rais anakuwa sana nje ya ofis (anazunguka dunia), cheo kikiwa k1 atakuwa overloaded. Tusubir had tukipata kiongoz mwajbkaj.
 
Muangila

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2010
Messages
1,910
Points
1,250

Muangila

JF-Expert Member
Joined Feb 24, 2010
1,910 1,250
U have a point mkuu...! Makamu wa rais yupo kama mfalme hana madaraka yoyote wala maamuzi kazi kuzunguka tu kufungu warsha kongamanos na seminars hii nafasi ipo kwa ajili ya kuwaridhisha waznz lkn kiuchumi inaiumiza zaidi bara.
 
Mvaa Tai

JF-Expert Member
Joined
Aug 11, 2009
Messages
6,175
Points
2,000

Mvaa Tai

JF-Expert Member
Joined Aug 11, 2009
6,175 2,000
Unachokisema ni kweli kabisa, ila itakuwa ngumu sana kufuta baadhi ya nafasi za uongozi kwasababu zipo kwa ajiri ya kugawana, hebu fikiria wanamtandao wanavyonyukana chini chini kukosa hizo nafasi za shukrani kwa kuchangia vizuri wkumuweka mtu madarakani. Kwa Tanzania hilo haliwezekani
 
ebrah

JF-Expert Member
Joined
Oct 9, 2010
Messages
397
Points
170

ebrah

JF-Expert Member
Joined Oct 9, 2010
397 170
naunga mkono, ila pale kwa wazirimkuu kutoka upande wa pili hapana kwani zanzibar kuna waziri kiongozi,katika hili eneo mawazo yangu iwe hivi "(a) kuwe na Raisi mmoja na mawaziri wakuu toka pande zote za muungano kusiwe na raisi zanzibar wala makamu huku bara.(b) Kuwe na Raisi wa tz,wa zanzibar awe makam katika muungano, then waziri mkuu.
 
ebrah

JF-Expert Member
Joined
Oct 9, 2010
Messages
397
Points
170

ebrah

JF-Expert Member
Joined Oct 9, 2010
397 170
naunga mkono, ila pale kwa wazirimkuu kutoka upande wa pili hapana kwani zanzibar kuna waziri kiongozi,katika hili eneo mawazo yangu iwe hivi "(a) kuwe na Raisi mmoja na mawaziri wakuu toka pande zote za muungano kusiwe na raisi zanzibar wala makamu huku bara.(b) Kuwe na Raisi wa tz,wa zanzibar awe makam katika muungano, then waziri mkuu.nawakilisha.
 
MwanaFalsafa1

JF-Expert Member
Joined
Feb 26, 2008
Messages
5,566
Points
1,195

MwanaFalsafa1

JF-Expert Member
Joined Feb 26, 2008
5,566 1,195
Nakuunga mkono mkuu.

Hivi majuzi nilishangaa kuona Waziri mkuu alishindwa kumchukulia hatua Jairo eti hadi awasiliane na Raisi. Hivi Raisi akisafiri anamwachia nchi nani kati ya makamu na waziri mkuu? Maana kama anamwachia waziri mkuu, basi mzee mzima pinda alikua ana mamlaka ya kumchukulia hatua jairo moja kwa moja ... ila kama anamwachia makamu wa rais, nilitegemea pinda awasiliane na makamu wa raisi ili hatua stahiki zichukuliwe.

Hii inanichanganya kiasi naona bora nafasi mojawapo ifutwe kweli ...

Mkuu ndiyo maana kwa Tanzania makamo wa raisi hana maana yoyote. Ukiacha vijukumu ambavyo kapewa kwenye katiba kazo zake zote zingine zina tegemea na raisi atampa nini. Kwa hiyo kama JK hakumuachia Bilal majukumu ya kushughulikia swala kama la Jairo ina maana asingeweza kufanya kitu. Yani ni cheo hakina maana yoyote ile.

Tukiangalia Shein alipo kuwa makamo wa raisi na sasa Bilala huwezi kuona kazi yoyote ya maana waliyo fanya au uamuzi wowote waliotoa kwa sababu hawana nguvu hiyo.
 
MwanaFalsafa1

JF-Expert Member
Joined
Feb 26, 2008
Messages
5,566
Points
1,195

MwanaFalsafa1

JF-Expert Member
Joined Feb 26, 2008
5,566 1,195
U have a point mkuu...! Makamu wa rais yupo kama mfalme hana madaraka yoyote wala maamuzi kazi kuzunguka tu kufungu warsha kongamanos na seminars hii nafasi ipo kwa ajili ya kuwaridhisha waznz lkn kiuchumi inaiumiza zaidi bara.
Ni kweli mkuu hiki cheo kipo kama political token. Kwa mfano Bilal alikua na nguvu sana Zanzibar kwa hiyo baada ya kumnyima wakaamua wampoze na cheo ambacho kwenye karatasi ni kikubwa (wa pili toka kwa raisi) lakini kiutendaji hamna kitu kabisa.
 
MwanaFalsafa1

JF-Expert Member
Joined
Feb 26, 2008
Messages
5,566
Points
1,195

MwanaFalsafa1

JF-Expert Member
Joined Feb 26, 2008
5,566 1,195
naunga mkono, ila pale kwa wazirimkuu kutoka upande wa pili hapana kwani zanzibar kuna waziri kiongozi,katika hili eneo mawazo yangu iwe hivi "(a) kuwe na Raisi mmoja na mawaziri wakuu toka pande zote za muungano kusiwe na raisi zanzibar wala makamu huku bara.(b) Kuwe na Raisi wa tz,wa zanzibar awe makam katika muungano, then waziri mkuu.
Au kinyume na hapo tuwe na makamu wa raisi wawili toka pande zote za muungano na cheo cha waziri mkuu kifutwe kabisa. Maana sisi Tanzania tumechanganya parliamentary system na presidential system na japo kuna nchi zingine zimefanya hivyo mfano India iau Ethiopia unakuta kwenye hizi nchi raisi ni ceremonial (head of state) na waziri mkuu ndiyo mtendaji mkuu (head of government) sasa sisi tuna raisi (head of state and government) na waziri mkuu ( head of government).
 
Felixonfellix

JF-Expert Member
Joined
Feb 16, 2010
Messages
1,670
Points
1,195

Felixonfellix

JF-Expert Member
Joined Feb 16, 2010
1,670 1,195
Kuna vyeo vingi tu havina maana, tunahitaji kuwa realistic katika kuangalia upya mambo haya. tumejitwisha mzigo mkubwa ambao hatuwezi kuubeba tena.
Kwa hapa kwetu naona waongeze makamu wa makamu wa rais. Rais anakuwa sana nje ya ofis (anazunguka dunia), cheo kikiwa k1 atakuwa overloaded. Tusubir had tukipata kiongoz mwajbkaj.
 
Tata

JF-Expert Member
Joined
Dec 3, 2009
Messages
5,594
Points
2,000

Tata

JF-Expert Member
Joined Dec 3, 2009
5,594 2,000
Mimi naona imefika wakati tuamue moja na kufuta cheo kimoja kati ya makamo wa raisi au waziri mkuu. Sioni mantiki ya kuwa na vyeo vyote hivi kwa wakati mmoja. Naamini kabisa waziri mkuu anaweza akafanya kazi ya makamo wa raisi na makamo wa raisi anaweza akafanya kazi ya waziri mkuu. Sasa kuna maana gani kuwa na vyeo vyote hivi?

Nasema hivi kwa sababu mara nyingi vyeo vyote hivi viwili vikiwepo mara nyingi inaashiria nchi hiyo ina mgogoro fulani wa kisiasa na cheo kimoja kimewekwa ili mtu wa "upande wa pili" kupewa. Mfano ni Kenya kuanzisha cheo cha waziri mkuu baada ya uchaguzi wa 2007 ili Raila Odinga apewe nafasi hiyo na Zimbabwe ambapo alipewa Morgan Tsavangirai. Naweza kusahihishwa lakini kichwani hainijii nchi yoyote isiyo kuwa na mgogoro wa kisiasa ambapo vyeo vya makamo wa raisi na waziri mkuu vyote vipo.

Kwa Tanzania mimi naona bora cheo cha makamo wa raisi kifutwe kabisa kwani hamna la maana makamo wa raisi analo fanya zaidi ya kuwa kiongozi "ceremonial" anaeitwa kukata utepe na kuzindua vitu. Najua katiba inasema raisi akitoka upande mmoja wa muungano basi sharti makamo atoke upande wa pili. Hilo halina neno kwani tunaweza kusema raisi akitoka upande mmoja wa muungano basi waziri mkuu atoke upande wa pili.

Sababu ya pili nashauri nafasi ya makamo wa raisi ifutwe ni kwa sababu japo kiprotokali cheo cha makamo wa raisi ndicho cha pili kwa ukubwa kiutendaji waziri mkuu ana nguvu zaidi kuliko makamo wa raisi. Pia waziri mkuu kama mtendaji mkuu wa serikali ina maanisha ana nafasi nzuri zaidi ya kukaimu kiti cha uraisi endapo raisi hayupo au ana hali inayo mzuia kufanya shughuli zake.

Pili napenda kushauri nafasi za naibu waziri nazo tuzifutie mbali. Zina jaza tu ukubwa wa baraza wakati kazi ya naibu waziri inaweza ikafanywa vizuri tu na katibu mkuu wa wizara husika. Pale waziri ambapo hayupo nani anaefaa zaidi kuendesha shughuli za serikali kama si katibu mkuu wa wizara?

Mwisho ningependa pia kushauri nafasi za waziri wa nchi zifutwe kwani hazina matiki zozote. Naamini kabisa shughuli zinazo fanya na waziri wa nchi zinawezwa wekwa zikawa chini ya idara ya wizara kamili.

Nazani imefika wakati tupunguze hizi nafasi za "zawadi za kisiasa" na tubaki na zile ambazo kweli tuna zihitaji katika uendeshaji wa serikali yetu. Nawakilisha.
True!! hawa jamaa wanaongeza tu idadi ya vyeo serikalini na foleni barabarani kwa sababu ya misafara yao isiyokuwa na tija. Kiutendaji Waziri Mkuu na Makamu wa Rais ni vibogoyo tu (au Nyoka wa Kibisa) wasioweza kufanya maamuzi yoyote ya maana kwa nchi kama ambavyo tumeshuhudia Pinda akitoa majibu yasiyokuwa na kichwa wala miguu.
 
Tata

JF-Expert Member
Joined
Dec 3, 2009
Messages
5,594
Points
2,000

Tata

JF-Expert Member
Joined Dec 3, 2009
5,594 2,000
Au kinyume na hapo tuwe na makamu wa raisi wawili toka pande zote za muungano na cheo cha waziri mkuu kifutwe kabisa. Maana sisi Tanzania tumechanganya parliamentary system na presidential system na japo kuna nchi zingine zimefanya hivyo mfano India iau Ethiopia unakuta kwenye hizi nchi raisi ni ceremonial (head of state) na waziri mkuu ndiyo mtendaji mkuu (head of government) sasa sisi tuna raisi (head of state and government) na waziri mkuu ( head of government).
Ukweli ni kuwa waziri mkuu ni Head of a MINISTRY not Government kama ulivyoeleza hapo juu. Wizara yake inaitwa TAMISEMI. Hana tofauti na waziri mwingine yeyote.
 
Tata

JF-Expert Member
Joined
Dec 3, 2009
Messages
5,594
Points
2,000

Tata

JF-Expert Member
Joined Dec 3, 2009
5,594 2,000
naunga mkono, ila pale kwa wazirimkuu kutoka upande wa pili hapana kwani zanzibar kuna waziri kiongozi,katika hili eneo mawazo yangu iwe hivi "(a) kuwe na Raisi mmoja na mawaziri wakuu toka pande zote za muungano kusiwe na raisi zanzibar wala makamu huku bara.(b) Kuwe na Raisi wa tz,wa zanzibar awe makam katika muungano, then waziri mkuu.nawakilisha.
Wewe sasa unataka kuwachokoza wazanzibari. Zanzibar hakuna waziri kiongozi bali kuna makamu wawili wa rais.
 
GeniusBrain

JF-Expert Member
Joined
Nov 3, 2010
Messages
4,321
Points
1,195

GeniusBrain

JF-Expert Member
Joined Nov 3, 2010
4,321 1,195
Mimi naona imefika wakati tuamue moja na kufuta cheo kimoja kati ya makamo wa raisi au waziri mkuu. Sioni mantiki ya kuwa na vyeo vyote hivi kwa wakati mmoja. Naamini kabisa waziri mkuu anaweza akafanya kazi ya makamo wa raisi na makamo wa raisi anaweza akafanya kazi ya waziri mkuu. Sasa kuna maana gani kuwa na vyeo vyote hivi?

Nasema hivi kwa sababu mara nyingi vyeo vyote hivi viwili vikiwepo mara nyingi inaashiria nchi hiyo ina mgogoro fulani wa kisiasa na cheo kimoja kimewekwa ili mtu wa "upande wa pili" kupewa. Mfano ni Kenya kuanzisha cheo cha waziri mkuu baada ya uchaguzi wa 2007 ili Raila Odinga apewe nafasi hiyo na Zimbabwe ambapo alipewa Morgan Tsavangirai. Naweza kusahihishwa lakini kichwani hainijii nchi yoyote isiyo kuwa na mgogoro wa kisiasa ambapo vyeo vya makamo wa raisi na waziri mkuu vyote vipo.

Kwa Tanzania mimi naona bora cheo cha makamo wa raisi kifutwe kabisa kwani hamna la maana makamo wa raisi analo fanya zaidi ya kuwa kiongozi "ceremonial" anaeitwa kukata utepe na kuzindua vitu. Najua katiba inasema raisi akitoka upande mmoja wa muungano basi sharti makamo atoke upande wa pili. Hilo halina neno kwani tunaweza kusema raisi akitoka upande mmoja wa muungano basi waziri mkuu atoke upande wa pili.

Sababu ya pili nashauri nafasi ya makamo wa raisi ifutwe ni kwa sababu japo kiprotokali cheo cha makamo wa raisi ndicho cha pili kwa ukubwa kiutendaji waziri mkuu ana nguvu zaidi kuliko makamo wa raisi. Pia waziri mkuu kama mtendaji mkuu wa serikali ina maanisha ana nafasi nzuri zaidi ya kukaimu kiti cha uraisi endapo raisi hayupo au ana hali inayo mzuia kufanya shughuli zake.

Pili napenda kushauri nafasi za naibu waziri nazo tuzifutie mbali. Zina jaza tu ukubwa wa baraza wakati kazi ya naibu waziri inaweza ikafanywa vizuri tu na katibu mkuu wa wizara husika. Pale waziri ambapo hayupo nani anaefaa zaidi kuendesha shughuli za serikali kama si katibu mkuu wa wizara?

Mwisho ningependa pia kushauri nafasi za waziri wa nchi zifutwe kwani hazina matiki zozote. Naamini kabisa shughuli zinazo fanya na waziri wa nchi zinawezwa wekwa zikawa chini ya idara ya wizara kamili.

Nazani imefika wakati tupunguze hizi nafasi za "zawadi za kisiasa" na tubaki na zile ambazo kweli tuna zihitaji katika uendeshaji wa serikali yetu. Nawakilisha.
Yawasilishe mawazo yako mfu kwenye jukwaa la katiba !
 
Najijua

JF-Expert Member
Joined
Nov 5, 2010
Messages
1,037
Points
1,195

Najijua

JF-Expert Member
Joined Nov 5, 2010
1,037 1,195
Naunga mkono hoja, naongeza na hivi vyeo vifutwe kibaki kimoja kati ya hivyo coz kodi zetu zina chomwa bila sababu

1. DAS, Mkurugenzi wa halmashauri na M/Kiti au meya wa halmashauri
2. RAS, Meya wa jiji, Mkurugenzi wa jiji
3. Mkurugenzi wizarani, kamishina wa kitengo na mkuu wa idara

na vingine nimesahau ongezeni
 
Forum statistics

Threads 1,353,394
Members 518,294
Posts 33,076,459
Top