Hakika Uwaziri mkuu wa Watanzania ni vyema ufutwe,manake imekuwa kama kichocheo,kuyumbisha shughuri za maendeleo,manake kwa walio wengi waliopata kuwa mawaziri wakuu wa Tanzania ni mmoja tu ndiyea laiyefanikiwa kuwa Rais wa Tanzania na mwingine japo angeweza kuwa Rais lakini hakungangania na angekuwa kinganganizi angeweza lakini kwa kujua urais ni nini akamludishia Rais mhusika.
Waliobaki wali wengi wao wamekuwa ving'ang'anizi wa kutaka wawe Marais bila kujali kanuni na mpangilio mzima.Wanapoingia kwenye cheo hicho hawaangaiki na kuhudumia Wananchi kama ilivyokuwa kwa JK na RK.Wanachoshughurika nacho ni kuhangaika huku na kule ili wajenge mfumo [System] ya kuwasupport kuchukua Urais.
Kidogo JSW sikupata kusikia kuingia kwenye vuguvugu la kuwania Urais lakini waliosaria wengi wao walichaluka kama mbogo,kukitaka kiti cha enzi cha Watanzania.Waliokuwa na busara walikaa pembeni baada ya kukikosa wakatumia busara zao kujiengua,wasio na busara wamekuwa na kero mpaka inachefua.
Hakika Kama Mzee huyu JM akuhupata Urais wa Tanzania,basi hakika haitatokea Waziri mkuu mwingine yoyote kinganganizi awe na pesa asiwe na pesa kuweza kuwa Rais wa Nchi hii,bali ataingia kukubalika tu kama Wananchi watataka au wanampenda kuona anakuwa Rais wao.
Kuna jadi na kama utamaduni wa asilia [nature] na kama Mama Tanzania imekuwa kitu ambacho waliopata kuwa Mawaziri wakuu wa Tanzania, ambao wameshika nafsi hiyo ni JK tu ndiye aliyepata kuwa Rais,basi kwa utamaduni wa Mzee RK kukabidhi tena madaraka kwa aliyekuja kuwa Rais aliasisi jadi ya kufunga ufunguo wa mtu aliyepata kuwa Waziri mkuu kuwa Rais.
Japo wakiwa kwenye cheo hicho wanapumbazika na kamwe hawaioni jadi hiyo asilia [nature] wala hawajifunzi kwa kwa kuona wenzao walio watangulia.Na kwa kuwa hawana macho wala masikio basi wanabaki kupigana na vivuli vyao kila siku ya Mungu ili wawe Marais.
Kuna mmoja yeye inasemekana alipendwa na Mwalimu sana kiasi kuwa alitamani kumuona kawa Rais wa Watanzania lakini Mwalimu akupata kutimiza ndoto yake hiyo na hivyo kudhibitishiwa na kanuni asilia ambayo walio wengi ukiizungumia awawezi kujua unazungumzia nini.
Hivyo kuendele kuwa na cheo hiki kinachoshabikia mbinu na mikakati ya kuangalia nafasi ya Urais na si kusimamia shughuri za maendeleo na Taifa kwa ujumla ni mzigo mkubwa kwa Taifa letu.Na pamoja na mbinu zote na michakato na matumizi ya rasimali ya umma yote na bado wasichukue Urais,inakuwa ni kuyumbisha Taifa na watu wake.
Na mchezo mwingine umezaliwa kwenye Wizara ya mambo Nchi za Nje, kuanza kuhalalishwa kuwa ni kituo cha kumuandaa Rais mtarajiwa.Upofu huu wa kinasaba ya kimfumo ni hatarishi sana kwa usalama wa Taifa.Tusifike sehemu Watanzania wajue Rais anaweza kutoka sehemu yoyote ile ndani ya Serikali au Nje ya Serikali ili tu awe na uwezo na mfumo [system] unajua ni mzalendo na atasimamia kujenga na kulinda Nchi kwa kadri ya maono yake na kukubalika kwake kwa jamii.