Nashauri: Viongozi msishindane na Mbowe kwenye kuongea

Kamundu

Platinum Member
Nov 22, 2006
6,605
8,744
Mimi naona hawa viongozi wanajaribu kushindana na Mbowe kwenye kuongea hawawezi kushinda na sio mbinu nzuri sana. Kila binadamu ana kipaji chake na Mbowe bahati yake Mungu kampa kipaji cha sauti nzuri, kujua kuongea na kusikilizika. Wengine wamepewa vipaji vya akili, wengine vipaji vya usimamiaji. Lakini ukiangalia vizuri kitu kimoja ambacho kimemsaidia Mbowe kwa miaka yote kwenye jamii ambayo inathamini sana wasomi kuliko watu wengine ni kipaji chake cha mawasiliano. Sasa spika hata kama anaongea mazuri hata fanikiwa kushindana na kipaji maana kipaji ni kitu ambacho unapewa na Mungu. Hivyo sio sawa kulinganisha hotuba za Magu au spika na Mbowe. Mbowe ni kama Obama USA kwenye kuongea huwezi kushindana naye.

Magu kwa akili za kipaji anapitwa na Nyerere tu kwenye Maraisi waliopita lakini kwenye kipaji cha mawasiliano ni wa mwisho kabisa sio muuongeaji mzuri.

Mfano kwenye Corona Magu ameweka majibizano mengi sana yasiyo ya msingi kumbe angeweza kueleza kwa kirahisi sana watu wakamwelewa kabisa.

Magu angeleza hivi: Ni kweli lockdown ingesaidia kupunguza maambukizina vifo kwa Watanzania wenzetu. Na katika mazingira ya kawaida tungefanya lockdown. Lakini ukweli Watanzania wenzangu nchi yetu bado ni masikini sana, uchumi wetu ni wa siku kwa siku. Kwa misingi hiyo hatuna uwezo kama nchi wa kufanya lockdown.

Badala yake washauri wanamwambia aanze kupinga ukweli kama vile lockdown isingepunguza maambukizi, mara vipimo vibovu ambavyo ni serikali ndiyo imeleta, mara kubadilisha waziri na kumweka mbunge ambaye amekutetea bungeni.... kuna mambo mengi ya mawasiliano hayaendi vizuri. Kwa kipaji cha Magu kidogo kwenye mawasiliano wangejaribu kutoa ujumbe mfupi ambao haupingani na ukweli. Hakuna mtu angelaumu maana huu ni ugojwa wa Dunia nzima.

Wakati wa Lissu nao ni hivyo hiyo wangeweza kabisa kukubali makosa ya usalama wa taifa ambao uko wazi na kusema ukweli badala ya kujaribu kushindana na watu wenye kipaji zaidi na ukweli uko upande wao.

Ni lazima viongozi na washauri wajue mapungufu ya viongozi wao na uongozi huu ni mawasiliano. Mwana Ilboru mwenzangu Mwigulu naye ataishia kufukuzwa maana anashinda kwenye mitandao kubishana na Mbowe badala ya kufanya kazi mpya ya uwaziri wa sheria. Tena hii wizara hutakiwi kuongea ovyo.
 
Mkuu ,hivi mtu mwenye kipaji cha akili kiasi Cha kuwazidi wote waliomtangulia,hata Kama presentation skills zake sio nzuri,yaani anashindwa hata kuona kile alichoandikiwa au kushauriwa kuwa ni upuuzi?I believe umempaka mafuta kwa mgongo wa chupa
 
Acheni kumperemba Mbowe, hana kipaji chochote cha kuongea sema anaongea vitu ambavyo Watanzania wengi mnapenda kusikia. Rais Magufuli yeye anaongea ambavyo hampendi kusikia ambavyo kimsingi ndiyo ukweli wenyewe wa mambo.
 
Acheni kumperemba Mbowe, hana kipaji chochote cha kuongea sema anaongea vitu ambavyo Watanzania wengi mnapenda kusikia. Rais Magufuli yeye anaongea ambavyo hampendi kusikia ambavyo kimsingi ndiyo ukweli wenyewe wa mambo.
Ninachoamini ni kwamba ukweli utabaki kuwa ukweli hata angeongea shetani. Unapenda kuusikia au hupendi kuusikia haubadiliki, unabaki kama ulivyo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Acheni kumperemba Mbowe, hana kipaji chochote cha kuongea sema anaongea vitu ambavyo Watanzania wengi mnapenda kusikia. Rais Magufuli yeye anaongea ambavyo hampendi kusikia ambavyo kimsingi ndiyo ukweli wenyewe wa mambo.
Usishindane na aliyejaaliwa utapasuka msamba

FB_IMG_1589397986327.jpg
 
mbowe hakuna kitu pale ni tapeli wa kisiasa tu,kwa mapoyoyo wenzake watamwona muongeaji mzuri Ila pumba nyingi sana utapeli tu ndio maana hataki kuachia uenyekiti
 
Nashangaa hata huyu mbwa anashindana na kamanda wa anga MBOWE
 

Attachments

  • 2361894_images.jpeg
    2361894_images.jpeg
    31.4 KB · Views: 1
mbowe hakuna kitu pale ni tapeli wa kisiasa tu,kwa mapoyoyo wenzake watamwona muongeaji mzuri Ila pumba nyingi sana utapeli tu ndio maana hataki kuachia uenyekiti

Sasa jiulize imekuwaje amekuwa na Chama kikubwa na kukaa zaidi ya miaka 20! tena upinzani ni lazima kuna kitu anacho. Swamba lake lilibomolewa, jengo lake la bilkanas walivunja jiulize inawezekana vipi akawa hapo. Mimi nataka kumsadia Magu maana hata akiwa na nia nzui bado anajichanganya mwenyewe
 
Back
Top Bottom