Nashauri siku ya wajinga tarehe 01/04 ifutwe kabisa

Nashauri siku ya wajinga tarehe 01/04 ifutwe kabisa

Antony Abel

JF-Expert Member
Joined
Dec 18, 2017
Posts
264
Reaction score
142
Kama uwezekano upo basi ningeomba siku kama ya leo 01/04 ifutwe kabisa.

Leo mida ya saa 1asubihi nikiwa nyumbani nilisikia simu ikiita kuangalia kaka yangu kanipigia akaniambia kuwa baba mdogo amefariki saa 10 usiku kwa hivo nifanye haraka kwa ajil ya kusafirisha maiti.

Nikatoka huku nilipo hadi kufika mjini, cha ajabu nimemkuta baba mdogo akiwa kwenye shughuli zake tukasalimiana vizuri huku akisema yupo salama kabisa.

Ndipo nilipo kwenda kwa kaka na kumuuliza, kulikoni kuchuriana? Akanijibu kwani wewe hujui kama leo ni tarehe 01/04 sikukuu ya wajinga!

Ukweli nilikasirika sana lakini sikuwa na jinsi ya kufanya.
 
hahha ,siku ya wajinga nilidakwaga Mara moja tu ,niliambiwa nimefukuzwa Shule nikachukue barua kwa Mkuu wa Shule.kufika tu Mkuu wa Shule alikua anajua kinachoendelea akaniacha nje ya ofisi akaondoka .badae akaja akaniambia nipotee its fools day
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Back
Top Bottom