Nashauri salamu ya "Shikamoo" ifutwe

Kwa roho zetu hizi za kiswahili mwingine ukimsalimia ukamshika miguu yeye anaweza kukushika kichwa lakini huku moyoni mwake anakulaani badala ya kukubariki. CHEZEA ROHO MBAYA YA KISWAHILI WEWE!
 
Utakuja kushika mapepo
 
Ww ndo akili zako makamasi vijana wanaleta mabadiliko ya kweli, shikamoo utumwa na nyerere aliendeleza utumwa
 
Acha kupotosha watu maana ya shikamoo ni kuwa chini ya miguu ya mhusika, halafu ukitaka kujua kiundani hakuna shikamoo uarabuni. Ilikuwa Salam ya utumwa.
 

Nakubaliana na wewe kwamba ifutwe, ila sababu nayoiona mimi ni sababu salamu ya SHIKAMOO ni zao la biashara ya utumwa. Ukiangalia hata kwenye makabila yetu hakuna salamu ambayo ni ya upande mmoja(yaani lazima itoke kwa mdogo kwenda kwa mkubwa).

Sababu nyingine ni kuwa hivi kwa salamu ya upande mmoja (unidirectional) utajuaje kwamba huyu unayetaka kumsalimia ni mkubwa kuliko wewe ikitokea hufahamu umri wake (sura inaweza danganya)?
 
Mkuu acha tu kutoa shikamoo haujalazimishwa
 
Lol! huo muda unatoka wapi basi hii salaam imepitwa na wakati
 
Uko sahihi mkuu. Asante kwa kuliona hilo kama pia kikwazo cha maendeleo yetu.
 
Acha uzushi wewe. Shikamoo ni tradition mbaya sana ambayo waarabu walio wasulubu mababu na mabibi zetu wametuachia. Nafikiri mababu zetu walio shuhudia mateso yao hao waarabu wakituona jinsi gani tuna lishangilia hili neno watatushangaa sana.

Shikamoo ni neno ambalo wazee wetu walilitumia kuwaomba radhi watesaji walio wachukua utumwa wakifanya kosa wasiwapige mpaka kufa.

Walilitunia hilo neno kuwaambia watesaji kuwa "niko chini ya miguu yako" kama ishira ya kumtukuza mtesaji na kumwonyesha kuwa yeye ana power huu yake na lolote lile atakalo fanya yeye ndiye master.

Ni heshima mbovu sana ya kudhalilishana. Kwa nini umwambie binadam mwenzako niko chini ya miguu yako. Ridiculous!
 
Na sisi wana wa wakama ,watemi, na wami: tusalimieje ili kulindi hadhi yetu?
 
Na sisi wana wa wakama ,watemi, na wami: tusalimieje ili kulinda hadhi yetu?
 
Utashangaa toto halina adabu midharau kibao ila kila siku shikamoo pambaf shikamoo mama yako
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…