Nashauri Rais awekwe mbali au apunguziwe access na mitandao ya kijamii

Stroke

JF-Expert Member
Feb 17, 2012
34,668
40,916
Kwa mtazamo wangu ili kumuwezesha kufanya maamuzi akiwa na fikra huru wampunguzie access au kumuweka mbali na mitandao ya kijamii.

Lisipofanyika hilo utendaji wake utaathirika pakubwa kwani maamuzi yake yanaweza athiriwa na opinions za watu ambazo kwa namna moja au nyingine zinaweza zisiwe sahihi.

Kwa siku hizi chache hilo ni jambo ambalo nimeona ni muhimu kufanyika na wasaizidi wake.

My few cents.
 
Wacheni Mama apangue apange timu itakayoendana na Kasi yake ya ukweli

Halafu achukue na ushauri wa Kigogo 14 kuhusu akina Ole Sabaya na wenzake
Huu ni ushauri tu kamanda, nadhani wahusika watauzingatia.
 
Magufuli was good mitandaoni alikuwa anapita mwenyewe na kufahamu mambo mengi na ikawa ngumu kwa wasaidizi wake kumdanganya.

Mama amerithi utamaduni huo na anashiriki kwa kutweet kabisa.

Huu ni utamaduni mzuri,unamuwezesha kuwa karibu na raia na kupata feedback ya kinachoendelea ground.

Naamini kabisa wasiotaka Rais na wasaidizi wake wa karibu kutumia mitandao wana nia mbaya ya kumweka Rais viganjani wamwendeshe wanavyotaka wao,wamwaminishe yale wanayotaka wao na kumshauri mnayotaka nyinyi.

Acheni mama ajivinjari mitandaoni,msimpangie.

La jana limewaumizeni sana mataga,mnataka kumcontrol Rais,haiwezekani.Acha awe huru.
 
Magufuli was good mitandaoni alikuwa anapita mwenyewe na kufahamu mambo mengi na ikawa ngumu kwa wasaidizi wake kumdanganya.
Mama amerithi utamaduni huo na anashiriki kwa kutweet kabisa...
Unaweza ukaliweka hivyo na ukaeleweka na baadhi ya watu ila lengo langu ni kumpa muda wa kuwa na maamuzi binafsi yasiyotokana na influence nyingine hasa wakati huu anapoanza kufanya kazi.

Huko mbeleni haina shida ila kwa sasa itamfanya asiwe na misimamo yake binafsi na watu watashindwa kuielewa misimamo yake yeye mwenyewe.
 
Kweli kabisa mkuu, mitandao sio mizuri sana nahisi ndio iliyochangia kuukuza ugonjwa wa moyo wa mzee wetu mpaka katutoka tungari tunamuhitaji sana hasa wakati huu wa forced vaccination & vita za magaidi kule Mozambique
 
Dunia ya leo Kumzuia au Kumpunguzia Rais access ya Mitandao ni Kitendo cha Kipumbavu na Kisichovumilika na pia Kinakera kama kikitoka kwa Great Thinker wa JamiiForums.

Yaani mnataka Rais Mama Samia Suluhu Hassan asiwabadilishe au asiwaondoe hao Manyang'au yenu ili yaendelee Kuharibu na Kuwalinda Kiuchumi kwa Gharama ya Kuwafisadi Watanzania Wanyonge?

Tena sasa nakuambia hakuna Rais ambaye kama akiwa anapenda Kuipitia Mitandao ya Kijamii na hasa huu huu wa JamiiForums ataongoza nchi vizuri mno kama Mheshimiwa Mama Samia Suluhu Hassan.

Katika dunia ya leo kamwe huwezi Kushindana na Nguvu ya Mtandao hasa katika Suala zima la Ushawishi ndani ya nchi yoyote ile. Mbona Marais wengine wakubwa tu duniani akina Biden, Putin na Kagame wapo mno Mitandaoni tena 24/7 na nchi zao zinapiga hatua za Kimaendeleo?

Huyo Rais Mheshimiwa Mama Samia Suluhu Hassan amekuambia huwa anakesha fully humu Mitandaoni? Acha Kumpangia cha Kufanya na kama haya Mabadiliko yamekugusa pole sana anza Kujiandaa Kisaikolojia na tambua kuwa kutesa ni kwa zamu na sasa Rais ni SSH na siyo tena Hayati JPM.
 
Mmeanza nyie Lumumba FC. Mwacheni Mama afanye kazi.
Opinions nyingi za mitandaoni zinatolewa kwa malengo ya vukundi flani,

Ukifuatilia sana mambo ya mitandaoni itakua ngumu kufanya maamuzi binafsi, tutakua tunaongozwa na opinions za watu badala ya maamuzi ya kitaasisi,

Nimeandika kwa lengo jema tu, ushauri huu unaweza usizingatiwe pia.
 
Unaweza ukaliweka hivyo na ukaeleweka na baadhi ya watu ila lengo langu ni kumpa muda wa kuwa na maamuzi binafsi yasiyotokana na influence nyingine hasa wakati huu anapoanza kufanya kazi.

Huko mbeleni haina shida ila kwa sasa itamfanya asiwe na misimamo yake binafsi na watu watashindwa kuielewa misimamo yake yeye mwenyewe.
Mimi sidhani kama anaweza kusoma kitu mtandaoni halafu akakibeba hivyo hivyo.
Lazima atafanya uchunguzi wake kujiridhisha.

Na sio kwamba ndio anategemea mtandao as a main source.Naamini hii ni mojawapo tu kati ya njia zake nyingi kupata taarifa na kushauriwa.

Inawezekana pia haya ni maamuzi ya system yake na wanamsaidia kuhakikisha anapata anachotaka na sio kwamba ni yeye mwenyewe yuko mtandaoni full time au kwamba yeye personally ndio anaendesha zile accounts zake.

Inawezekana pia uwepo wake mitandaoni unaleta mtazamo fulani kwa jamii ambao in turn unaipa system feedback fulani wanayoitaka kirahisi tofauti na kama wangejificha na kutokuwa public.

Pia pre emptying ni mojawapo ya faida inayoweza kupata system ya mama kwa wao kuzoeleka mitandaoni kama hivi.(kama una idea ya intelijensia utanielewa hapo).

System inabadilisha mbinu kila wakati kulingana na mahitaji ya wakati kwa namna wao wanavyotaka kuendesha nchi.

Hivyo hata baadhi ya tabia kiongozi anafundishwa kuziadopt ili awe na taswira fulani katika jamii kwa wakati fulani na sababu fulani.

Nikudokeze tu kwamba sio mama pekee aliyeingia mtandaoni,viongozi wa serikali ya awamu ya sita wengi wameanza kuwa very active mitandaoni.

So nadhani this is planned na system iko aware na huenda ndio architecture wa hili kwa sababu wajuazo wao.
 
Opinions nyingi za mitandaoni zinatolewa kwa malengo ya vukundi flani,

Ukifuatilia sana mambo ya mitandaoni itakua ngumu kufanya maamuzi binafsi, tutakua tunaongozwa na opinions za watu badala ya maamuzi ya kitaasisi,

Nimeandika kwa lengo jema tu, ushauri huu unaweza usizingatiwe pia.
Maoni gani aliyafuata toka mtandaoni toka ashike madaraka?
 
Mimi sidhani kama anaweza kusoma kitu mtandaoni halafu akakibeba hivyo hivyo.
Lazima atafanya uchunguzi wake kujiridhisha...
Umeshindwa kuelewa point yangu ndogo sana kwamba ,

Pressure ya mitandaoni ni kubwa sana,

Kila mtu anataka jambo lake lifanyike kama anavyotaka yeye Rais bado hajaizoea office, kumpa access ya mitandaoni muda huu ni kumnyima peace of mind wakati wa kutimiza majukumu yake.

Kwa sasa tumpe muda kwanza once atakapokuwa settled anaweza fanya atakalo, na itakua vizuri kwani atakuwa anaangalia reaction ya her own decisions.
 
Back
Top Bottom