Nashauri Mrisho Gambo agombee ubunge 2020 Arusha mjini

Nashauri Mrisho Gambo agombee ubunge 2020 Arusha mjini

Mimi ninachojua ni kwamba kiongozi yeyote anayejua kero za wananchi na akajaribu kutatua kwa kuwashirikisha ipasavyo na wakatambua kweli mtu huyu yupo kwa ajili yao atakuwa kiongozi wa watu hao kwa muda mrefu lakini ukaweka kisogo interest zao na mtu mwingine akaja kuzifanyia kazi huyo ndiye watakaye kuwa na imani naye. Kwa mawazo yangu mimi yeye anatimiza wajibu wake kama kiongozi katika mkoa huo kwa sababu serikali hii lengo lake ni kutatua kero za watu na kuleta maendeleo. Uongozi thabiti ni ule wenye malengo ya kutatua kero za wananchi wake. Watu watapima kwa kuwatumikia
Swadakta mkuu upo sahihi sana.natumaini wanasiasa watajifunza ulichokizungumza katika post hii
 
Ana uwezo huo sana. Anajiamini sana kama Lema alivo. Wakisimamishwa Kwenye Debate Lema anaweza kosa points.
Ngoja tusubirie asee lakini kwa imani yangu ARUSHA kwenda kwa Ccm ni kichekesho kipya hiki ..upinzani wame take over
 
Hivi unaamini kuwa uongozi wa rais wa sasa ni mbovu sana na 2020 anapigwa chini?
Ni vigumu kuamini. Kama Lowassa alishwandwa wakati ule ndio 2020?
 
Arusha mnaijua mnaisikia

hata aje Mungu kwa Mgongo wa CCM hapewi kura
 
Mh. Gambo wakomboe wana wa Arusha kutoka kwa wapiga dili.......
 
Wala ww siyo cdm ni ccm ni sisi watu wa kaskazin hatututakaa tuichague ccm kamwe hata kama ccm itatawala hii nchi milele
 
Lema kapwaya sana arusha na anatuangusha chadema bora arudi TLP akaungane na Mrema kudili na wafungwa!!! Chyaa...mbunge hana programu yoyote ya maendelea zaidi ya madongo na maandamano!!! Asee Lema, pita ivi chalangu!
 
Nizamu ya kumpoteza huyo mropokaji,
Cdm imeoza pale ni Viroba tu hakuna jipya.
Gambo kiboko ya wapuuzi
Mungu mpatie nguvu na afya tele kijana
Wetu
 
Endelea na mawazo yako ya kusadikika. Kwa taarifa yako hakuna yeyote ndani ya CCM atakayelichukua jimbo hilo toka kwa Godbless Lema.


Mimi ni mpenzi wa CHADEMA kwa muda mrefu sasa hapa mkoani Arusha lakini kasi ya huyu kijana Mh. Mrisho Gambo ni kubwa sana na mbunge wetu Lema asipogutuka mapema atakuta mwenzake yupo mbali sana.

Tangu awe Mkuu wa Mkoa amefanya vitu vingi na sensitive sana.

Kukutana na walimu wote, kukutana na waandishi wa habari, kujadili kuhusu utalii na changamoto zake mkoani Arusha, suluhisho la mgogoro wa murieti na ujenzi wa Kituo cha Polisi Kwa Morombo ni baadhi ya mambo machache tu na yanayotia hamasa na kazidi kumjengea umaarufu na imani kwa wana arusha wote.

Yule Mh. Lema ninayemjua sijui yuko wapi kwa sasa. Juzi tu Mh. Gambo kaagiza pesa zilizookolewa kutokana na madiwani kujizidishia zitumiwe kulipia madeni ya walimu. Kama ni hivi CHADEMA itasalimika kweli?

Mrisho Gambo gombea ubunge 2020 ili wapinzani wa jifunze na kurudisha ule ushindani uliopotea kwa muda mrefu.

Arusha tunataka maendeleo sio vurugu tena.

Wasalaam,
 
Back
Top Bottom