Nashauri Manispaa ya Moshi itangazwe kuwa jiji 2022. Mashamba makubwa yaruhusiwe ndani ya mipango miji

Vigezo vinakidhi ?
 
Nani anataka kujenga huko Moshi. Kaeni na vihampa vyenu fursa ziko kibao nchi hii.
 
Moshi hakuna Ardhi ya kuuza ndomana wachagga wamekimbilia kushika ardhi ktk mikoa mingine na ardhi hurithishwa vizazi kwa vizazi, mchagga na udongo ni kaka na baba
 
Unavijua vigezo vya manispaa kuwa jiji au unajisemea tu ?
Usichojua Ni kwamba ilikuwa moshi iwe jiji tangu enzi za JK lkn kuna mambo machache na yameshafanyiwa kazi.Unadhani kelele zenu zitazuia mchakato huo.

Moshi mji una vigezo vyote.
 
Unavijua vigezo vya manispaa kuwa jiji au unajisemea tu ?
Unabishana bila kujitambua.Katika michango yangu nimeshataja 3.Hutaweza kujua coz hujui ,Ni ushabiki

Na km ni vigezo Dodoma isingestahili kuwa jiji. Nitajie hata kimoja ambacho Dodoma ilikidhi tofauti na ukubwa wa eneo.
 
Ndugu zetu kule wakiacha ubahili na ubinafsi tutalifanya jiji mapema mno, haiwezekani mji matajiri ni wale wale miaka nenda rudi na kuziba mianya ya wageni kupanuka kibiashara kwa kuwapiga vita baridi na fitina 😁!

Siku wakiheshimu VYASAKA tutalifanya jiji!
 
Achana nae huyo chuki imemjaa
 
Unabishana bila kujitambua.Katika michango yangu nimeshataja 3.Hutaweza kujua coz hujui ,Ni ushabiki

Na km ni vigezo Dodoma isingestahili kuwa jiji. Nitajie hata kimoja ambacho Dodoma ilikidhi tofauti na ukubwa wa eneo.
Usilinganishe Moshi na Dodoma. Dodoma ni makao makuu ya nchi.
 
Mkuu

Mji wa Moshi ni ngumu kuwa ni jiji maana ni eneo dogo mno kubeba mahitaji ya uduma zote ukizingatia ardhi na udongo wa hapo hauruhusu kujenga majengo marefu kutokana na mfumo wa kijiolojia wa miamba ya volkano.
Labda uitwe mji wa utalii, mazingira na viwanda maalum bora lakini sio kwa shughuli mbalimbali za kiuchumi kama biashara nk maana zinaweza kuhatarisha uhai wa mlima Kilimanjaro na mazingira kwa ujumla.
 
Tatizo lako hujui maana ya ardhi ya kuweka rasilimali, Viwanda, recreation (Burudani) Hospital na vinginevyo.
Huko kote ulikokutaja ni viwanja vya watu, na wewe unafikiri Jiji linajengwa kwenye viwanja hivyo, fungukeni muoneshe ardhi sio huko Mabogini.
Wenzako waliotoka Moshi unakosema wamekimbilia kwa warangi ndio sasa matajiri,
kwa Wagogo pia matajiri ndio hao waliotokea Moshi.
Uchoyo umewajaa mtabaki kubrush viatu mabarabarani na kuuza simu
Mimi nimezaliwa hapo, nimesoma mpaka Chuo hapo Moshi mitaa na tabia za hapo hunifichi ndio maana tumewakimbia kwa ajili ki-Mji kuwa dormant hakiwezi kuwa Jiji kwani hakuna ARDHI
 
Na km ni vigezo Dodoma isingestahili kuwa jiji. Nitajie hata kimoja ambacho Dodoma ilikidhi tofauti na ukubwa wa eneo.
Jibu hapo Mkuu ni Ukubwa wa Eneo, Wakazi na wageni walijichukulia ardhi ovyo na wengine wakidai ni za Mababu wakapewa Sheria na wakaziachia
Rais ana uwezo wa kuchukua Ardhi yoyote kwa Amri au kwa fidia na sisi ni tofauti na Kenya
48. Allocation of land acquired Ord. No. 14 of 1961 s. 19 (1) Subject to the provisions of subsection (2) of this section, the President may allocate any land acquired compulsorily pursuant to the provisions of this Act to the local government authority, any public utility company or corporation or any religious, educational, charitable, cultural or social institution or organisation or to any person on such terms and conditions as he shall consider necessary to secure its use in the manner provided in the scheme applicable thereto within a reasonable period after the coming into effect of the scheme.
Kwa hiyo hao wenzako wanaosema Ardhi haitolewi waache UTOPOLO kigezo ni kuwa Ardhi Moshi hakuna ya kuwekeza Jiji hapo
WAKULUNGWA ARDHI YA MOSHI NA KILIMANJARO HAIUZWI KWA WAKUJA!!!!!! Tuna taratibu zetu Na ardhi wala hatujaomba msaada.
 
Achana nae huyo chuki imemjaa
Wanjiru labda ungetafuta Sheria za uanzishaji hii Miji na Majiji chwa kwanza ni Ardhi
Huo Mji eneo gani utaendeleza na limesha jaa, nimetoka huko Kibosho Mkombole mpaka Old Moshi Mahoma makaburi wametafukuwa na kuweka vitu vingine, leo utwagusa si uanataka wakulilie, haya huko tambarare kwenye mipunga ndipo utajenga Ofisi za umma? au mnaamini kujijengea nyumba kwenye robo eka ndio kuwa Jiji, Miji inaanza na Ardhi, hao ndugu zangu ni wabinafsi (selfish) hawana ushirikiano kabisa kwa kila kitu na sio leo angalia Histori ya Mareale kwenda UN hadi leo kisiasa
soma hapo chini usije na majibu ya kijiweni
5.0 VIGEZO VYA KUANZISHA HALMASHAURI ZA MIJI, MANISPAA NA JIJI:
5.1 Vigezo vya ujumla
i. Jiografia ambayo inafanya utoaji huduma kwa Wananchi kuwa mgumu kwa sababu ya milima, mito, misitu, mabonde au Visiwa.
ii. Kuwepo kwa miundombinu inayohitajika kwa eneo la utawala kuanzishwa,
iii. Kuwepo kwa mtandao wa barabara za uhakika kuunganisha Makao Makuu ya eneo la utawala lililoanzishwa na maeneo mengine yenye kuhitaji kuhudumiwa na Makao Makuu,
iv. Uwezo wa Serikali wa kuanzisha eneo jipya la utawala,
v. Utayari wa Wananchi kuchangia uanzishaji wa eneo la utawala.
Aidha, ili maeneo hayo yaweze kuanzishwa/ kupandishwa hadhi vimewekwa vigezo kwa mujibu wa Sheria ya Mipango Miji Na 8 ya mwaka 2007 (The Urban Planning Act No 8 of 2007) Kipengele cha Tano cha Jedwali la Tano (Item number 5 of the Fifth Schedule) kama ifuatavyo:-
 
Magufuli asikusikie ukizungumzia maendeleo ya Kilimanjaro.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…