Nashauri Manispaa ya Moshi itangazwe kuwa jiji 2022. Mashamba makubwa yaruhusiwe ndani ya mipango miji

Usichojua Ni kwamba Moshi Kama mji siyo kwa ajili ya wachaga.Tatizo mentality za ukabila na chuki zimewajaa.Kwako wewe dodoma kwa ajili ya wagogo na warangi.

Mbona hampigi kelele Iringa,Lindi au Songea kuwa majiji kwa sababu wenyeji wanaachia ardhi yao kirahisi. Mchaga siyo mgogoe, mzaramo mpaka akuuzie ardhi kirahisi wanajua thamaniy ya kipande cha ardhi alicho nacho.

Na si kwamba moshi ardhi ya kununua haipo. Ipo bali hutafika Bei kwasabab wauzaji wanajua thamani yake.
Wanaowekeza ktk viwanda mbona hawakosi ardhi.Nyie mnaotaka viwanja vya kujenga room mbili na Bei hamfiki ndiyo mnapiga kelele humu.

MOSHI ITAKUWA JIJI KABLA MAGUFULI HAJAONDOKA MADARAKANI. HUU UTOPOLO WENU NA VICHUKI VYA KIKE HAVITAZUIA HILO.
Vigezo vinakidhi ?
 
Na moshi siyo apo send tu,kuna mashamba na viwanja vingi tu shabaha, MABOGINI, KAHE. Huko hamtaki nyie moshi Ni shan't, Soweto kcmc wakat huna hela. Walioko siriaz viwanja vipo vingi tu mjohoron, sango, kawawa, mbokomu kote uko vipo.

Tatizo wenye hivyo viwanja si wazaramo au wagogo, Ni watu wanaojua thamani ya kipande cha ardhi. Wanajua value of money.
Nani anataka kujenga huko Moshi. Kaeni na vihampa vyenu fursa ziko kibao nchi hii.
 
Moshi hakuna Ardhi ya kuuza ndomana wachagga wamekimbilia kushika ardhi ktk mikoa mingine na ardhi hurithishwa vizazi kwa vizazi, mchagga na udongo ni kaka na baba
Miji inayokua kwa kasi sasa hiivi ni le ambayo sio michoyo kuuza ardhi kwa wageni yenye mchanganyiko wa makabila mbalimbai

Moshi mjini wanataka jiji lenye mashamba makubwa!!!! la ardhi isiyoendelezwa!!!

Ukabila utaua Moshi mji sababu wazee hawauzi maeneo yao wala nyumba zao zivunjwe wawekezaji wapya wafanye yao!!

matokeo vijana wa kichaga wengi wamejenga na kuwekeza sana mikoa mingine Moshi mjini wametelekezea wazee wabaki nao na ardhi yao ndio maana haukui wala kuwa na sura mpya ya maana.

Moshi mbeleni waweza shushwa hata hadhi kutoka manispaa na kuwa mji wakiendelea na hiyo tabia sababu mji ni kama hauna generational success plan ya kuufanya uende juu
 
Unavijua vigezo vya manispaa kuwa jiji au unajisemea tu ?
Usichojua Ni kwamba ilikuwa moshi iwe jiji tangu enzi za JK lkn kuna mambo machache na yameshafanyiwa kazi.Unadhani kelele zenu zitazuia mchakato huo.

Moshi mji una vigezo vyote.
 
Unavijua vigezo vya manispaa kuwa jiji au unajisemea tu ?
Unabishana bila kujitambua.Katika michango yangu nimeshataja 3.Hutaweza kujua coz hujui ,Ni ushabiki

Na km ni vigezo Dodoma isingestahili kuwa jiji. Nitajie hata kimoja ambacho Dodoma ilikidhi tofauti na ukubwa wa eneo.
 
Ndugu zetu kule wakiacha ubahili na ubinafsi tutalifanya jiji mapema mno, haiwezekani mji matajiri ni wale wale miaka nenda rudi na kuziba mianya ya wageni kupanuka kibiashara kwa kuwapiga vita baridi na fitina 😁!

Siku wakiheshimu VYASAKA tutalifanya jiji!
 
Mbona ndiyo mji pekee unaosubiria kupewa hadhi hiyo.Jikaze tu kifua kisipasuke kwa chuki. Eti majengo mengi ni dizaini ya zamani,kwahiyo mji hauwezi kuwa jiji kwa sababu hiyo.

Nb:
Kajiridhishe kwanza vigezo vinavyotumika kuipa manispaa /mji hadhi ya kuwa jiji, halafu urudi.
Achana nae huyo chuki imemjaa
 
Unabishana bila kujitambua.Katika michango yangu nimeshataja 3.Hutaweza kujua coz hujui ,Ni ushabiki

Na km ni vigezo Dodoma isingestahili kuwa jiji. Nitajie hata kimoja ambacho Dodoma ilikidhi tofauti na ukubwa wa eneo.
Usilinganishe Moshi na Dodoma. Dodoma ni makao makuu ya nchi.
 
Nashauri Manispaa ya Moshi itangazwe kuwa jiji in 2022.

1) Mji upanuliwe kusini mwa barabara ya Moshi-Arusha, this is very important. Kamwe mji usipanuliwe Kaskazini mwa barabara ya Moshi-Arusha.

2) Sehemu ya kata za wilaya ya Hai na Moshi Vijijini, zinazopakana na Manispaa ya Moshi na zilizoko kusini mwa barabara ya Moshi-Arusha, zihamishiwe kwenye Manispaa ya Moshi.

3) Katika eneo litakalohamishwa, contribution ya Moshi vijijini iwe kubwa kuliko contribution ya Hai, kwasababu Wilaya ya Moshi Vijijini ni kubwa (kieneo) kuliko Wilaya ya Hai.

4) Mipango miji ya Manispaa isiwabague watu wa kipato cha chini.

5) Mipango miji ya Manispaa isiwabague wazawa wenyeji.

6) Mipango miji ya Manispaa iruhusu mashamba makubwa na viwanja vikubwa sana kuendelea kuwepo ndani ya Manispaa.

7) Mipango miji ya Manispaa isilazimishe majengo marefu ndani ya Manispaa.

8) Mipango miji ya Manispaa isifute hati za kimila ndani ya Manispaa.

9) Kuwe na maeneo ya viwanja vya low density. Ambayo yata mimic Oysterbay na Masaki.

10) Maeneo ya makaburi ya waafrika yazungushiwe ukuta mfupi (wa futi 2). Na kuwe na gaps pana kwenye pande mbali mbali zitakazoruhusu magari mapana na watu wengi kuingia na kutoka kwa rahisi sana.

11) Serikali kuu ipeleke fungu kubwa la pesa litakalo boresha miundombinu ya Jiji hilo la Moshi.

12) Eneo la Mji wa Himo lipanuliwe (kwa upande wa kusini mwa barabara ya Moshi-Arusha-Holili, unaopakana na barabara ya kwenda Dar es Salaam) na Miji wa Himo upewe hadhi ya Manispaa ya mji. Kanuni za mipango miji ya Himo zifanane na hizo hapo juu nilizoshauri kuhusu mipango miji ya Manispaa ya Moshi.

13) Kiwanja kidogo cha ndege cha Moshi mjini kihamishiwe Uchira (Kusini mwa Barabara ya Moshi-Arusha). Na kiwe na runway ya lami ya 3.3 kms.

14) Mipango miji mingine yeyote ya maeneo ya mkoa wa Kilimanjaro ifuate kanuni za mipango miji nilizoshauri hapo juu. E.g. Mipango miji ya makao makuu ya wilaya mbalimbali za Mkoa wa Kilimanjaro. Pia barabara za makao makuu ya wilaya zisile sana viwanja na mashamba ya watu.

NB: Mikoa mingine ya Tanzania (ambayo sio makao makuu ya nchi kama Dodoma na Dar es Salaam) inaweza kuiga kanuni hizi za mipango miji.

Asante sana.
Mkuu

Mji wa Moshi ni ngumu kuwa ni jiji maana ni eneo dogo mno kubeba mahitaji ya uduma zote ukizingatia ardhi na udongo wa hapo hauruhusu kujenga majengo marefu kutokana na mfumo wa kijiolojia wa miamba ya volkano.
Labda uitwe mji wa utalii, mazingira na viwanda maalum bora lakini sio kwa shughuli mbalimbali za kiuchumi kama biashara nk maana zinaweza kuhatarisha uhai wa mlima Kilimanjaro na mazingira kwa ujumla.
 
Na moshi siyo apo send tu,kuna mashamba na viwanja vingi tu shabaha, MABOGINI, KAHE. Huko hamtaki nyie moshi Ni shan't, Soweto kcmc wakat huna hela. Walioko siriaz viwanja vipo vingi tu mjohoron, sango, kawawa, mbokomu kote uko vipo.

Tatizo wenye hivyo viwanja si wazaramo au wagogo, Ni watu wanaojua thamani ya kipande cha ardhi. Wanajua value of money.
Tatizo lako hujui maana ya ardhi ya kuweka rasilimali, Viwanda, recreation (Burudani) Hospital na vinginevyo.
Huko kote ulikokutaja ni viwanja vya watu, na wewe unafikiri Jiji linajengwa kwenye viwanja hivyo, fungukeni muoneshe ardhi sio huko Mabogini.
Wenzako waliotoka Moshi unakosema wamekimbilia kwa warangi ndio sasa matajiri,
kwa Wagogo pia matajiri ndio hao waliotokea Moshi.
Uchoyo umewajaa mtabaki kubrush viatu mabarabarani na kuuza simu
Mimi nimezaliwa hapo, nimesoma mpaka Chuo hapo Moshi mitaa na tabia za hapo hunifichi ndio maana tumewakimbia kwa ajili ki-Mji kuwa dormant hakiwezi kuwa Jiji kwani hakuna ARDHI
 
Na km ni vigezo Dodoma isingestahili kuwa jiji. Nitajie hata kimoja ambacho Dodoma ilikidhi tofauti na ukubwa wa eneo.
Jibu hapo Mkuu ni Ukubwa wa Eneo, Wakazi na wageni walijichukulia ardhi ovyo na wengine wakidai ni za Mababu wakapewa Sheria na wakaziachia
Rais ana uwezo wa kuchukua Ardhi yoyote kwa Amri au kwa fidia na sisi ni tofauti na Kenya
48. Allocation of land acquired Ord. No. 14 of 1961 s. 19 (1) Subject to the provisions of subsection (2) of this section, the President may allocate any land acquired compulsorily pursuant to the provisions of this Act to the local government authority, any public utility company or corporation or any religious, educational, charitable, cultural or social institution or organisation or to any person on such terms and conditions as he shall consider necessary to secure its use in the manner provided in the scheme applicable thereto within a reasonable period after the coming into effect of the scheme.
Kwa hiyo hao wenzako wanaosema Ardhi haitolewi waache UTOPOLO kigezo ni kuwa Ardhi Moshi hakuna ya kuwekeza Jiji hapo
WAKULUNGWA ARDHI YA MOSHI NA KILIMANJARO HAIUZWI KWA WAKUJA!!!!!! Tuna taratibu zetu Na ardhi wala hatujaomba msaada.
 
Achana nae huyo chuki imemjaa
Wanjiru labda ungetafuta Sheria za uanzishaji hii Miji na Majiji chwa kwanza ni Ardhi
Huo Mji eneo gani utaendeleza na limesha jaa, nimetoka huko Kibosho Mkombole mpaka Old Moshi Mahoma makaburi wametafukuwa na kuweka vitu vingine, leo utwagusa si uanataka wakulilie, haya huko tambarare kwenye mipunga ndipo utajenga Ofisi za umma? au mnaamini kujijengea nyumba kwenye robo eka ndio kuwa Jiji, Miji inaanza na Ardhi, hao ndugu zangu ni wabinafsi (selfish) hawana ushirikiano kabisa kwa kila kitu na sio leo angalia Histori ya Mareale kwenda UN hadi leo kisiasa
soma hapo chini usije na majibu ya kijiweni
5.0 VIGEZO VYA KUANZISHA HALMASHAURI ZA MIJI, MANISPAA NA JIJI:
5.1 Vigezo vya ujumla
i. Jiografia ambayo inafanya utoaji huduma kwa Wananchi kuwa mgumu kwa sababu ya milima, mito, misitu, mabonde au Visiwa.
ii. Kuwepo kwa miundombinu inayohitajika kwa eneo la utawala kuanzishwa,
iii. Kuwepo kwa mtandao wa barabara za uhakika kuunganisha Makao Makuu ya eneo la utawala lililoanzishwa na maeneo mengine yenye kuhitaji kuhudumiwa na Makao Makuu,
iv. Uwezo wa Serikali wa kuanzisha eneo jipya la utawala,
v. Utayari wa Wananchi kuchangia uanzishaji wa eneo la utawala.
Aidha, ili maeneo hayo yaweze kuanzishwa/ kupandishwa hadhi vimewekwa vigezo kwa mujibu wa Sheria ya Mipango Miji Na 8 ya mwaka 2007 (The Urban Planning Act No 8 of 2007) Kipengele cha Tano cha Jedwali la Tano (Item number 5 of the Fifth Schedule) kama ifuatavyo:-
 
Nashauri Manispaa ya Moshi itangazwe kuwa jiji in 2022.

1) Mji upanuliwe kusini mwa barabara ya Moshi-Arusha, this is very important. Kamwe mji usipanuliwe Kaskazini mwa barabara ya Moshi-Arusha.

2) Sehemu ya kata za wilaya ya Hai na Moshi Vijijini, zinazopakana na Manispaa ya Moshi na zilizoko kusini mwa barabara ya Moshi-Arusha, zihamishiwe kwenye Manispaa ya Moshi.

3) Katika eneo litakalohamishwa, contribution ya Moshi vijijini iwe kubwa kuliko contribution ya Hai, kwasababu Wilaya ya Moshi Vijijini ni kubwa (kieneo) kuliko Wilaya ya Hai.

4) Mipango miji ya Manispaa isiwabague watu wa kipato cha chini.

5) Mipango miji ya Manispaa isiwabague wazawa wenyeji.

6) Mipango miji ya Manispaa iruhusu mashamba makubwa na viwanja vikubwa sana kuendelea kuwepo ndani ya Manispaa.

7) Mipango miji ya Manispaa isilazimishe majengo marefu ndani ya Manispaa.

8) Mipango miji ya Manispaa isifute hati za kimila ndani ya Manispaa.

9) Kuwe na maeneo ya viwanja vya low density. Ambayo yata mimic Oysterbay na Masaki.

10) Maeneo ya makaburi ya waafrika yazungushiwe ukuta mfupi (wa futi 2). Na kuwe na gaps pana kwenye pande mbali mbali zitakazoruhusu magari mapana na watu wengi kuingia na kutoka kwa rahisi sana.

11) Serikali kuu ipeleke fungu kubwa la pesa litakalo boresha miundombinu ya Jiji hilo la Moshi.

12) Eneo la Mji wa Himo lipanuliwe (kwa upande wa kusini mwa barabara ya Moshi-Arusha-Holili, unaopakana na barabara ya kwenda Dar es Salaam) na Miji wa Himo upewe hadhi ya Manispaa ya mji. Kanuni za mipango miji ya Himo zifanane na hizo hapo juu nilizoshauri kuhusu mipango miji ya Manispaa ya Moshi.

13) Kiwanja kidogo cha ndege cha Moshi mjini kihamishiwe Uchira (Kusini mwa Barabara ya Moshi-Arusha). Na kiwe na runway ya lami ya 3.3 kms.

14) Mipango miji mingine yeyote ya maeneo ya mkoa wa Kilimanjaro ifuate kanuni za mipango miji nilizoshauri hapo juu. E.g. Mipango miji ya makao makuu ya wilaya mbalimbali za Mkoa wa Kilimanjaro. Pia barabara za makao makuu ya wilaya zisile sana viwanja na mashamba ya watu.

NB: Mikoa mingine ya Tanzania (ambayo sio makao makuu ya nchi kama Dodoma na Dar es Salaam) inaweza kuiga kanuni hizi za mipango miji.

Asante sana.
Magufuli asikusikie ukizungumzia maendeleo ya Kilimanjaro.
 
13 Reactions
Reply
Back
Top Bottom