Nashauri kuwa na Afya Counseling kwa Madereva

Kiokotee

JF-Expert Member
Mar 21, 2022
1,675
2,194
Imefika mahali hizi Ajali sio bahati mbaya tena ni Uzembe wa mtu mmoja unaweza ondoa maisha ya familia za watu wasiopungua 60 ndani ya basi ndani ya nusu saa tu!

Hii sio sawa...kwa nini tukubali kuwa kama kuku mtu mmoja Atuchinje kwa Akili yake tu bila sababu hivi hakuna njia mbadala ya kudeal na huyu mtu kabla ya kumkabidhi roho zetu azisafirishe tukiwa hai.

Mi sio mtaalam wa Afya ya akili ila nafahamu kuna Councelling huwa inafanyika kumfahamu mtu kabla ya kumkabidhi jukumu zito kama marubani wa ndege na kama hayuko sawa siku hiyo anaweza pewa mwingine

Kama watu wengine, madereva wa vyombo vya moto wanaweza kuwa na matatizo au changamoto ambazo kwa namna moja au nyingine zinaweza kufanya apoteze concentration na hatimaye kusababisha ajali

Kufanya vipimo vya mara kwa mara, au counselling kunaweza kupunguza madhara yanayoweza kusababishwa na dereva kutokuwa na afya njema ya mwili na akili, mamlaka zitafute namna ya kucheki mara kwa mara afya za mwili na akili za madereva ili kutunusuru.

Inauma sana familia nzima inateketea kwa Uzembe wa mtu mmoja.
 
Mada nzuri ila imewakilishwa visivyo ila ni vema tukawa tunasoma to understand sio kuuliza maswali, accident it's someone fault na sio bahati mbaya au kazi ya Mungu, kuna mengi ya kujiuliza including mfumo wetu wa utoaji leseni, ni muhimu tuongeze kipengele cha PDP kwenye leseni,

barabara zetu bado ni mbovu mno na hazijawekwa alama za kuonya madereva, alama zinatakiwa zionekane vema sio kama hizi tulizokua nazo, yellow line hakuna kabisa kwenye hizi freeways zetu, tuondoe uchafu wa matuta na tuweke speed cameras, bodaboda, baiskeli, pedestrians hawatakiwi kisheria kutumia hizi freeways!
 
Imefika mahali hizi Ajali sio bahati mbaya tena ni Uzembe wa mtu mmoja unaweza ondoa maisha ya familia za watu wasiopungua 60 ndani ya basi ndani ya nusu saa tu!! Hii sio sawa...kwa nn tukubali kuwa km km kuku mtu mmoja Atuchinje kwa Akili yake tu bila sababu hivi hakuna soln mbadala ya kudeal na huyu mtu kabla ya kumkabidhi roho zetu azisafirishe tukiwa hai
Kabla ya kuongelea madereva tuongelee Mamlaka simamizi, nyingi zinakula rushwa na ndiyo maana madereva hawadhibitiki hata iweje
 
Mkuu hao madereva wanafanya kazi katika mazingira magumu sana, long hours, ujira mdogo, leo areport afanyiwe counselling, familia yake itakula wapi ndio maana wengine wanajilipua tu hata kama wamejua siku hio hawajisikii vizuri...lol.
 
Una mawazo mazuri ila uandishi wako ni wa hovyo, unafupisha maneno kiajabu ajabu tu mpaka unapoteza maana ya sentesnsi.

Na sio lazima uandike heading kwa kiingereza mkuu.
 
Kweli kabisa long hours ni sababu kubwa na pia wenye magari wengi ni wabaguzi kama hawawezi kufanya service magari yao Kwanini waendelee na biashara hii

Unakuta matairi kipara, break zimeisha hata spring ziko hoi
Sasa hapo ni ajali lazima

Kingine dereva anakimbiza kama kichaa na wasafiri wamekaa kimya tu kwanini wasipaze sauti na kusema punguza speed au tunashuka wote
Hata kuongea hawajui utafikiri kabeba Ng’ombe

Traffic anapiga mkono anawaaga hawasemi kitu
 
Yaani unamaanisha watakuwa wa tatizo la kisaikolojia

Likiwezekana hilo na viongozi wanaoongiza watu zaidi mil60 nchini wafanyiwe hivyo maana wengine matamko yao sio salama
 
Mkuu hao madereva wanafanya kazi katika mazingira magumu sana, long hours, ujira mdogo, leo areport afanyiwe counselling, familia yake itakula wapi ndio maana wengine wanajilipua tu hata kama wamejua siku hio hawajisikii vizuri...lol.
Tunafanyaje sasa au tukubali kupoteza familia kimasihara.
 
Yaani unamaanisha watakuwa wa tatizo la kisaikolojia

Likiwezekana hilo na viongozi wanaoongiza watu zaidi mil60 nchini wafanyiwe hivyo maana wengine matamko yao sio salama
Sorry! Sio kila uzi lazima uwe wa siasa..
 
Una mawazo mazuri ila uandishi wako ni wa hovyo, unafupisha maneno kiajabu ajabu tu mpaka unapoteza maana ya sentesnsi.

Na sio lazima uandike heading kwa kiingereza mkuu.
Ahsante mkuu,Ila hilo neno nasikiaga tu Madaktari wanalitamka halafu mi mwenyewe sijasoma kiviile labda unisaidie hilo neno kwa kiswahili silijui lengo langu ilikuwa kufikisha Ujumbe,Utanisamehe kwa uandishi wangu.
 
Ungetumia ushauri wa kitaalam.

Lakini yote kwa yote ujumbe umefika mkuu.
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom