Nashangaa wanawasonga tu hawa 19 yule mmoja wamemgwaya? Alisema Spika Ndugai

Masi Lambo

JF-Expert Member
Apr 8, 2020
532
360
Akizungumza baada ya kuwaapisha wabunge wateule, Spika Ndugai amekemea vikali watu wanaodharau shughuli zinazofanywa na Bunge la Tanzania.

"Wako rafiki zetu ambao hivi karibuni wamejipambanua kwa kukejeli shughuli za bunge, niwatahadharishe na kuwakumbusha labda wamesahau kuwa ni jambo lisilokubalika kwa mtu yoyote, kudharau shughuli za bunge, kudhalilisha bunge, kudhalilisha uongozi wa bunge na hata kudhalilisha wabunge waliokwisha kuapishwa.

Amesema maboresho ya kanuni inayosimamia kiapo yanamuwezesha mbunge mpya kutekeleza kazi za kibunge na kuwajibika kwa wananchi mara tu baada ya kuchaguliwa kwake au kuteuliwa kwake.

Kwa hiyo wabunge wote wa bunge la 12 tuliowaapisha tunaendelea kuwatambua kuwa wabunge kamili wakiwemo 20 wa chama cha Chadema, 19 wa kuteuliwa na mmoja wa kuchaguliwa, Aida Kenani.

''Nashangaa wanawasonga tu hawa 19 yule mmoja wamemgwaya? Wakiweza wamfukuze basi, lakini sisi tumeshamwapisha na tunamtambua kwamba ni mbunge, hayo yanayoendelea huko ni ya kwao'', alisema Spika Ndugai. Ndugai amewatoa wasiwasi waliokuwa wakifikiri kuwa wabunge 19 wateule si halali, akisema kuwa wale ni wabunge kamili.

''Na niwakumbushe wanahabari kuwa kila mnapotamka majina yao muanze kwa jina 'Mheshimiwa' kwa kuwa ni kanuni ya Bunge.''

'Ukandamizaji dhidi ya wanawake'
Spika Ndugai amewasihi Watanzania kukataa na kupiga vita ukandamizaji dhidi ya wanawake kwa kisingizio chochote kile.
Kiongozi huyo amekemea kitendo cha Mwenyekiti wa chama cha Chadema Freeman Mbowe kusimama hadharani na kuwatukana wabunge wanawake.

''Kwa mtu mzima na mwanaume wa Kitanzania uliyefundwa ni aibu kubwa kutukana wanawake hadharani, ningependa kuchukua nafasi hii kumuonya na kumkanya mwenzangu asione sifa jambo hili, wanawake ni mama zetu, dada zetu, shangazi zetu na hata kama wamekosea namna gani tuwatafute na kukaa nao ili kupata maelezo yao, na si kuwafukuza kama vibaka na kuona fahari katika kufanya hivyo''

Pia amemuonya mbunge wa zamani wa chama hicho kwa kitendo chake cha kuwatukana wanawake wenzake akiwaita 'Covid-19'.

''Yeye mwenyewe ni mwanamke anatukana wenzake namna hii, inasononesha unaona kweli safari ya wanawake bado ni ndefu kufikia mnakotaka kufika, hamjui nyinyi wale 19 wamepitia mapito gani, hamjui kwa nini imekuwa ilivyokuwa, ni ngumu, yako mambo hatuwezi kusema humu.

''Viko vyama ni kampuni ya mtu, mtu ni mungu mtu bila yeye hakiwezekani chochote na kwa masharti yoyote atakayoweka''.

Spika Ndugai amesema wabunge 19 ni wabunge kamili labda wao wenyewe waamue kwa kutumia utaratibu wa kikatiba kujiuzulu.

''Lakini kwa yeye na Mnyika wake, wale ni wabunge...hawawezi wao na genge lao la wanaume wakaweza kufanya hivyo kwa dada zetu hata tuwe vyama tofauti hata kabila , rangi tofauti lakini ubaguzi wa aina hii wa kijinsia unatakiwa upigwe vita na Watanzania wote.''

Hivi kweli rafiki yangu Freeman Mbowe, umesahau, Mh Halima alivyovunjika mkono kwa sababu ya kukufuata Magereza umesahau? Esther Bulaya alipopigwa akazimia na kupelekwa Aga Khan hajitambui kwa ajili yako? Esther Matiko amelazwa Segerea mara ngapi kwa ajili yako? Ningeweza kumtaja kila mmoja jinsi walivyosota kwa ajili ya wewe Mbowe, mshahara wao ni kufukuzwa hadharani kwa utaratibu ule usiokuwa wa ki utu? Haiwezekani!.Alisema Spika Ndugai.

1606761245952.png
 
Hivi kweli rafiki yangu Freeman Mbowe, umesahau, Mh Halima alivyovunjika mkono kwa sababu ya kukufuata Magereza umesahau? Esther Bulaya alipopigwa akazimia na kupelekwa Aga Khan hajitambui kwa ajili yako? Esther Matiko amelazwa Segerea mara ngapi kwa ajili yako? Ningeweza kumtaja kila mmoja jinsi walivyosota kwa ajili ya wewe Mbowe, mshahara wao ni kufukuzwa hadharani kwa utaratibu ule usiokuwa wa ki utu? Haiwezekani!.Alisema Spika Ndugai.
View attachment 1638653

Hayahayahayaaaaaaaaaa, wameanza kujianika wenyewe. Huu ukatili dhidi ya wanawake hawa ulipokuwa ukifanyika mlikuwa wapi wakati huo? Hamkuona maumivu waliyopitia? Akili ni zawadi kutoka kwa Mola wetu, Upumbavu ni zawadi kwa wasiotumia akili vyema.
 
Yaani leo Ndugai ndiyo anajua kuwa Wabunge wetu wanapaswa kuheshimiwa....!!?

Hivi wakati wanadhalilishwa, kupingwa na kufungwa alikuwa hayaoni yote hayo.

Design ya watu kama Hawa inabidi wafutwe kwenye historia ya nchi. Maana mtoto kufundishwa history inayomuhusisha huyu bwana nafikiri Siyo sahihi.
 
Ila hapo kwa mbunge wa Nkasi kama kuna ukweli flan, CDM ilibidi ianze na yule kipindi kile anaapishwa, sidhani kama wengine wangeenda kuapishwa baada ya kuona yule mwenzao adhabu ambayo angeipata
 
Then akasema, rafiki yake amewahi kushindwa ubunge mara mbili, hivyo eti ana uzoefu wa kushindwa...teh
Huyu mzee ana maneno sana...😂😂
 
Huyu Spika ni janga kwa Tanzania.

Haeleweki anapohoji kuhusu uhalali wa Mbunge wa kuchaguliwa Mhe. Kenani!

Kama Spika anashindwa kutofautisha kati ya mbunge wa Viti Maalumu na Mbunge wa Kuchaguliwa basi kuna something very wrong in his brain!
 
Back
Top Bottom