1. Issue sio uyahudi wao bali ni Ukristo wetu kwa maana ya kutii maandiko ya Biblia.
2. Mji wa Yerusalemu katika Israeli ni mji pendwa wa Mungu & umeshaharibiwa mara nyingi na kujengwa tena. Mungu ameahidi kupigana na mataifa yatakayotaka kuuharibu tena.
"Tena itakuwa siku hiyo, nitafanya Yerusalemu kuwa jiwe la kuwalemea watu wa kabila zote; wote watakaojitwika jiwe hilo watapata jeraha nyingi; na mataifa yote ya dunia watakusanyika pamoja juu yake. Hata itakuwa siku hiyo, ya kwamba nitatafuta kuwaangamiza mataifa yote watakaokuja kupigana na Yerusalemu." - Zekaria 12:3,9
3. Mungu anasema hao wayahudi ipo siku atawapa Roho ya utambuzi na Wataamini kupitia Yesu Kristo. That day is just near, kuna kitu anakiplot Mungu (Asomaye na afahamu).
"Nami nitawamwagia watu wa nyumba ya Daudi, na wenyeji wa Yerusalemu, roho ya neema na kuomba; nao watamtazama yeye ambaye walimchoma; nao watamwombolezea, kama vile mtu amwombolezeavyo mwanawe wa pekee; nao wataona uchungu kwa ajili yake, kama vile mtu aonavyo uchungu kwa ajili ya mzaliwa wake wa kwanza." - Zekaria 12:10
4. Israeli na mji wake pendwa Yerusalemu umechaguliwa na Mungu kuwa lango la baraka na Udhihirisho wa Mungu kwa mataifa mengine. Ukiwa nao utabarikiwa & kinyume chake ni laana.
"Tena itakuwa, ya kwamba mtu awaye yote wa jamaa zote zilizomo duniani, asiyekwea kwenda Yerusalemu ili kumwabudu Mfalme, Bwana wa majeshi, mvua haitanyesha kwao." - Zekaria 14:17
Nina mengi ya kuelezea, ngoja niishie hapa kwa sasa. Next time nitakuja kuwaeleza "KWA NINI NI MUHIMU KUIOMBEA AMANI ISRAELI/YERUSALEMU" kama ilivyoamriwa kwenye MAANDIKO.