Sijui nianze vipi, lakini kwa ufupi kama kichwa cha habari kinavyojieleza hapo juu sisi wanawake wa tanzania nasema kwa niaba ya wengi tumechoka na mfumo dume.
Kila mahali unaenda unakuta midume imejitutumuaaaaaa, mara miruzi mara weweeeeeeeee tumechoka aaaaaaaaah.
Haya tuanze na majumbani mwetu, kila kitu kipaumbele anapewa mwanaume. Shule yeye, urithi yeye, nyumba yeye.
Tukija makazini hivyo hivyo, tunafanywa kama vitu, hupati kazi mpaka utangulize kitu. jamani tumechoka.
Tukija katika uchumi, tunadhalisha sana lakini hatuthaminiwi juzi shangazi yangu karudi nyumani kakuta mjomba kauza mazao yote aliyolima.
Tumejaribu tumeshaweza kuwa na benki yetu, maana nyungine zimekuwa zikitunyanyapa hazijui mahitaji yetu. Kutokana na malaamiko yaliyomo vyuoni tunataka chuo chetu kikuuu tusinyanyaswe kijinsia na mijibaba mikware yenye kutoka udenda ionapo mwanamwali.
Bado kwenye nafasi za uongozi za nchi hii tumesahauliwa tunadharauliwa sana. Historia ambayo imepindishwa kuhusu uhuru wa nchi hiii ni budi sasa iandikwe upya, sisi tulishiriki kwa hali na mali zaidi tena zaidi kupigania uhuru wa nchi hii, tulikuwa wahamasishaji wakubwa mikoani kuanzia usangi mpaka uyole. Mtwara mpaka Ngara. Kama si wanawake wa nchi hii usingepatikana.
Kwa kumalizia ni haki katika nchi hii, sisi kinamama wa nchi hii mifumo ya mahakama imejaa mfumo dume tunaonewa mahakamani hatupati haki, ni wakati sasa na sisi wanawake tupate mahakama zetu. Mashauri yote ya kinamama na yanausisha wanawake yapelekwe kwenye mahama hizo, natena nasema na sisi ni rahia wa nchi hii.