Ivi uko timamu kabisa?Kuna wakati tunapaswa kumshukuru sana mungu, we unalalamika huna viatu wenzio hawana miguu
Jaribu kuwaza wenzio uliomaliza nao chuo hawajaajiliwa na hawana ramani na hakuna wa kumkopa ili kusogeza mbele gurudumu la maisha kwa matumaini ya kulipa hata mwisho wa mwezi?. Mimi nakushauri acha kazi uwape nafasi wahitaji ambao wako tayari kuvumilia hali hiyo.
Usijari leo kwako kesho kwanguShukrani Sana kaka kwa mchango wako najua Mungu atakuzidishia ulipotoa umenisave sana
Mungu akubarikiUko Wilaya gani? Pole sana
Weka namba ya simu pia atakaeguswa akusaidie
Ila pambana andika barua fuata taratibu zinazohusika kutoa malalamiko, omba appointment na wakubwa ukikwama kabisa tafuta shughuli nyingine ya kufanya.
Pole, Mungu atafanya njia
Sent from my SM-G955F using JamiiForums mobile app
utazunguka na mavyombo nchi nzima 😅Ni shughuli gani unayofanya yenye pesa nje nje?
Sawa Mkuu utanisamehe kwa majibu ya hasra, lkn inaumiza sana kwa mtu kuwekwa ugenini kwa 4 month bila chochote!shukrani sana ndugu yangu. nimepata ujumbe wako.
Jamaa hajui maana ya njaa. Aisee bora ulemavu kama unapata nanuhakika wa kula kuliko NJAA Jamaa analalamika ana njaa kisha jinga moja linamwambia awaze kuhusu walemavu! Hivi amewahi kupigwa njaa sawasawa kweli!Ww jamaangu unaakili fupi sana, afadhali ukose ramani ukiwa mazingira uliyozoea kulko ugenini, pili uvumilivu gani unataka kama yy kakaa mwezi Wa 4 huu kwa kupewa 10 na shule, ungekuwa wewe na akili hiyo ushakufa muda sana!
Mkuu huwezi mlaaumu mwalimu mkuu kwa kushindwa kumpa 30,000, jua kwamba hela wanayopewa ya madaraka wengi unakuta wamekopa hiyo ndiyo inamtoa.Mkuu wa shule ni mshenzi sana, pesa ya madaraka anashindwa kukupatia hata elfu 30,000 kwa mwezi?
Nadhani pia hata serikali hawakuwa wamejiandaa na hizo ajira, huku nilipo ndio wanaandaa pesa za kujikimu, inasikitisha sana
Sent from my Infinix X652 using JamiiForums mobile app
Tangu 2016 ulikuwa unaishi vipi? Uko kwenye ajira, kuwa na natumaini na subira kuwa muda si mrefu utakuwa na kipato.Kwa kuanza kabisa Mimi ni mwalimu wa primary ajira mpya kwa hii intake ya Desemba!
Nakiri wazi kuwa tangu nimalize chuo mwaka 2016 ndo nimebahatika kupata ajira mwaka jana lakini Hali yangu kimwili, na kiakili kwa Sasa haijakaa sawa kutokana na changamoto ninazopitia.
Kwanza naomba niweke wazi kuwa tangu mwezi desemba nipo kituoni (kazini) na sijawahi pewa mshahara hata mmoja maana kila nikifuatilia halmashauri naambiwa kuwa nisubiri uhakiki wa vyeti bado unaendelea na huu mwezi sina hakika ya kulipwa yaani hapa nilipo nadaiwa na watu hata kupokea simu naogopa, na mbaya zaidi kila siku naishi kwa mikopo na siku nikikosa kabisa nalala njaa kabisa, nilijaribu kumueleza mkuu wa shule lakini katika bajeti yao walinipa sh 10000 tu wakidai kuwa chalk na vifaa vingine vya shule havijanunuliwa na wakizidisha bajeti itawalemea.
Yaani sikuwahi jua kuwa mtu unaweza ikafika hatua ukaishi kwa mateso hivi.
Yaani inafika kipindi napika ugali naweka chumvi kisa sina mboga.
Muda mwingine nakoroga uji natia chumvi.
Huku kwetu maji tunanunua siku nikikosa hela ya kununulia maji nanawa maji niliyooshea vyombo.
Yaani Mambo mengi magumu ambayo nayapitia na mpaka saivi nimedhoofu mwili hasa, sina amani kabisa yaani.
Na kingine nikiweke wazi na hii shida sijui nimeirithi wapi maana ni Toka utoto mfano kama hapa nateseka Sana lakini kutoka hapa na kwenda kwa majirani nikaombe chakula nashindwa kabisa maana naweza kaa hata siku mbili sijaonja kitu lakini kuomba chakula kwa mtu nashindwa kabisa.
Na saivi hakuna mtu hata wa kumkopa maana asilimia kubwa nimewakopa na wengine wananidai maana nikiwaambia bado sijaanza kupokea mshahara wanahisi nawadanganya.
Ila nateseka sana Tena Sana kibaya zaidi naishi kwenye nyumba ya kupanga ambapo mwenye nyumba ananidai kodi Toka januari na analalamika nimlipe Kodi yake au nihame.
Naombeni ushauri jamani maana wazo lililopo kichwani ni kutoenda shule Hadi mshahara utakapo ingia ili hizi siku nitumie hata kufanya vibarua. Je, naweza achishwa kazi kwa kosa la kutoenda shule.
Bado sijaipataNenda halmashauri, mwalimu mkuu, rudi home mpka utakapoingiziwa salary, mm binafsi nilipitia kipindi kama chako in take ya 2018, miezi tatu bila salary, afu huku ninafamilia. Acha kabisa. Ila check number umepata? , Pole
Upo hakmashauri gani ndugu?Bado sijaipata
Kwa unavyoona anaweza kuwa anadanganya ili apate kiki eeeeh??Kama ni kweli, pole
Swala siyo kupendana ni bajeti tuu imekaa vibaya, hivyo mtu anafikiria bajeti yake mwenyewe ya mawazo labda na mkopo kachukua sasa anawaza nimchukue mshikaji aingizwe kwenye payroll (4 to 6 months) may be zaidi anaona pazito. Wewe huoni mkuu wa shule kamchinjia baharini??Mimi huwa naamin walimu wengi hampendan tofaut na wafanyakazi wengine
Yan kweli kakosekana hata kjana mwenzako alie tangulia kwenye ajira ambae mamb yako vizur akajitolea akusaidie hadi mambo yakae vizuri uwe una kula chakula tu kwake? Kwani mkuu unamaliza kilo ngapi? Hata robo haumalizi.
Tatizo hampendani aise, wengine wakisikia kuna mgeni kafika muajiriwa mpya hata kama hawajuani wanahakikisha kwanza kapata sehemu ya kulala na kula
Kumbe hii ya kurudi nyumbani hadi salary isome iko kisheria siyo??Pole sana kwa unayopitia ila kwa utaratibu ni kuwa baada ya kuripoti kazini unarudi nyumbani mpaka mshahara utakapoingia ndio unaenda rasmi kufanya kazi, huyo mkuu wako hana msaada wowote kwako nenda kaonane na mwajiri wako/afisa utumishi ndiye anaweza kukusaidia..
... Hatujinyongiii hatunywi sumuuu CUF mbeleee kwa mbeleee [emoji445] [emoji445] [emoji126][emoji126][emoji1732][emoji1732]Mitano tena.
Ooops.
Unajua tatizo limeanzia kwa DEO na DED kwa sababu they know everything kuhusu kuchelewa mishahara ya hao walimu wapya... Walichotakiwa kufanya ni kuwapa posho ya kujikimu ya wiki mbili kama taratibu zilivyo na pia kuwaeleza utaratibu wote ikiwemo kuchelewa kwa mishahara yao.Pole!
Je upo halmashauri gani?
Nenda kwa DED directly!
DED ana mpaka fedha za zarura, kama ana hekima, atakupatia.
Wabongo ni waoga sana kujiajiri huko mtaani au kuajiriwa nje ya serikali..Kuajiriwa na serikali ni kujitafutia umasikin ..njoo huku tujiajiri pesa nje nje..