Napitia kipindi kigumu kuliko kawaida

Napitia kipindi kigumu kuliko kawaida

Niliongea naye kadai kuwa mtu ambaye hajalipwa mshahara sio ww tu na lingine alisema yy anaruhusiwa kutoa ruhusa ya siku mbili tu ndo maana nataka niamue kwa mawazo yangu nistop kwenda kazini kwa muda hata bila taarifa rasmi.
Pole sana mkuu, kwa kweli sijawahi kuona serikali ya ajabu kama hii. Mimi nilipoajiriwa miaka 20 iliyopita ile kuripoti kwenye kituo changu cha kazi nililipwa posho ya wiki mbili na kurudishiwa fedha za nauli niliyotumia. Mshahara ulichelewa miezi 2 wakati wa kuingiza data sheets but tulikuwa tunapata advance ili tuweze kujikimu. Sasa nashangaa sana kwa serikali ambayo makusanyo yamepanda mara dufu inamkopaje mtumishi anayeanza kazi?? Kwa nini sasa baada ya kuwaajiri hiyo Disemba kama fedha hakuna wasingewashauri wakae home mpaka pale mishahara itakapikuwepo? Ushauri wangu: kwa uzoefu wangu kwa walimu, hasa primary, wanavyosota due to inadequate salary, anza mapema kabisa kubuni shughuli mbadala for extra income (vibiashara kama uko mjini au kilimo kama uko vijijini).
 
Uko Wilaya gani?Pole sana
Weka namba ya simu pia atakaeguswa akusaidie
Ila pambana andika barua fuata taratibu zinazohusika kutoa malalamiko,,omba appointment na wakubwa ukikwama kabisa tafuta shuhuli nyingine ya kufanya.
Pole,Mungu atafanya njia

Sent from my SM-G955F using JamiiForums mobile app
Hivi wale CWT kazi yao ni nini hasa??
 
Kwa kuanza kabisa Mimi ni mwalimu wa primary ajira mpya kwa hii intake ya Desemba!

Nakiri wazi kuwa tangu nimalize chuo mwaka 2016 ndo nimebahatika kupata ajira mwaka jana lakini Hali yangu kimwili, na kiakili kwa Sasa haijakaa sawa kutokana na changamoto ninazopitia.

Kwanza naomba niweke wazi kuwa tangu mwezi desemba nipo kituoni (kazini) na sijawahi pewa mshahara hata mmoja maana kila nikifuatilia halmashauri naambiwa kuwa nisubiri uhakiki wa vyeti bado unaendelea na huu mwezi sina hakika ya kulipwa yaani hapa nilipo nadaiwa na watu hata kupokea simu naogopa, na mbaya zaidi kila siku naishi kwa mikopo na siku nikikosa kabisa nalala njaa kabisa, nilijaribu kumueleza mkuu wa shule lakini katika bajeti yao walinipa sh 10000 tu wakidai kuwa chalk na vifaa vingine vya shule havijanunuliwa na wakizidisha bajeti itawalemea.

Yaani sikuwahi jua kuwa mtu unaweza ikafika hatua ukaishi kwa mateso hivi.

Yaani inafika kipindi napika ugali naweka chumvi kisa sina mboga.

Muda mwingine nakoroga uji natia chumvi.

Huku kwetu maji tunanunua siku nikikosa hela ya kununulia maji nanawa maji niliyooshea vyombo.

Yaani Mambo mengi magumu ambayo nayapitia na mpaka saivi nimedhoofu mwili hasa, sina amani kabisa yaani.

Na kingine nikiweke wazi na hii shida sijui nimeirithi wapi maana ni Toka utoto mfano kama hapa nateseka Sana lakini kutoka hapa na kwenda kwa majirani nikaombe chakula nashindwa kabisa maana naweza kaa hata siku mbili sijaonja kitu lakini kuomba chakula kwa mtu nashindwa kabisa.

Na saivi hakuna mtu hata wa kumkopa maana asilimia kubwa nimewakopa na wengine wananidai maana nikiwaambia bado sijaanza kupokea mshahara wanahisi nawadanganya.

Ila nateseka sana Tena Sana kibaya zaidi naishi kwenye nyumba ya kupanga ambapo mwenye nyumba ananidai kodi Toka januari na analalamika nimlipe Kodi yake au nihame.

Naombeni ushauri jamani maana wazo lililopo kichwani ni kutoenda shule Hadi mshahara utakapo ingia ili hizi siku nitumie hata kufanya vibarua. Je, naweza achishwa kazi kwa kosa la kutoenda shule.
sio kuachidhwa tu bali ahata kunyang'anywa leseni.....ila nini umesema vyema sana kuwa unapita..... mimi nadhani fanya ukimbie ili upapite haraka apo unapopita....
 
Danganya upo maternity upewe ruhusa , mkuu wako anafel wap😆
 
Pole sana ndugu, jaribu tu kuvumilia maana nchi ina Rais mpya, labda yeye atakuwa na "huruma" kidogo na anaweza kuwakumbuka.

Usikimbilie kuacha kazi, vumilia tu, kumbuka ule msemo, "ukiona kiza kimezidi sana, basi fahamu karibia kutapambazuka".
 
Kuna wakati tunapaswa kumshukuru sana mungu, we unalalamika huna viatu wenzio hawana miguu
jaribu kuwaza wenzio uliomaliza nao chuo hawajaajiliwa na hawana ramani na hakuna wa kumkopa ili kusogeza mbele gurudumu la maisha kwa matumaini ya kulipa hata mwisho wa mwezi?. mi nakushauri acha kazi uwape nafasi wahitaji ambao wako tayari kuvumilia hali hiyo.
Wewe una matatizo ya akili

Sent from my Infinix X5515 using JamiiForums mobile app
 
Pole!
Je upo halmashauri gani?
Nenda kwa DED directly!
DED ana mpaka fedha za zarura, kama ana hekima, atakupatia.
Umemaliza USHAURI MZURI MIMI NILIAJIRIWA 2006 HATUKULIPWA MSHAHAR MIEZI 6 ILA TULIPATA MTU AKATUELEKEZA TWENDE KWA AFISA ELIMU TUKAWA TUNAKOPESHWA KILA MWEZ ANAKUKOPESHA NUSU YA MSHAHAR WAKO MPK TULIVYOLIPWA TUKAKATWA
 
Kwanza pole kwa changamoto hii.

Sikushangai kwa sababu kila mtu ana changamoto zake na mbinu tofauti za kuzitatua.

Ok

Sasa ushauri wangu ni kuwa ukitoka kufundisha jichanganye mtaani kwako,najua muda wa kutoka shule unatosha kukufanya uwe na masaa Kama matano au sita kabla ya kulala namaanisha muda wa kutoka shule mpaka muda wa kulala usiku.

Tumia huo muda vizuri,kwa mtu mwenye maamuzi magumu,na roho ya mapambano lisaa limoja Ni kubwa sana.

Anza hata kwa kuomba kumenya chips kwenye vibanda wanapokaanga Hapo huwezi kikosa za kula usiku,tafuta shughuli zozote za kujitolea fanya ukishachangamsha akiri na tumbo likiwa limeshiba utaona njia ya kutokea niamini Mimi.

Nobody can work with an empty stomach kwa hiyo pambania tumbo kwanza likikaa sawa kodi, mshahara nk vitakaa sawa tu.

Kila la kheri.
 
Kuajiriwa na serikali ni kujitafutia umasikin ..njoo huku tujiajiri pesa nje nje..
Kuna mwalimu yuko Geita vijiji vya ndan ndan sana....alipopatata ajira akaanza badilishana mpunga kwa hela...i thnk anakupa 5000 unampelekea debe 1...mwaka 2019 alikua ana machine za kukoboa mpunga alikua ana zaidi ya 600m bank narudia zaidi ya miliom mia sita benk...alinionesha nikahisi kupata kiharusi ..ukimuona unakataa...yaan anapelekewa mpunga balaa anaukoboa kitu kinaenda Rwanda na Congo! Ni mwalimu wa shule ya msingi tu!

Mwingine yupo Musoma...alipopelekwa vijijini akaanza kusanya mpunga anaweka kwake..akaona kwake kumejaa akaanza weka godown..yaan alikua anaukusanya kama kichaa ..mwaka jana ameuza akapata 8m! Na anakuambia hata 1m haikufika..maana wanafunzi wanampelekea anaupima ( ndoo unaiwekea petrol inatanuka)anawaambia haujfika debe analetewa 10kgs...nadhan wapima mpunga wanajua njia ile ya kuzungusha ndoo huku unaweka!
Wengine mikoa inayolima miti anawatumia wanafunzi kupanda miti..kwa mwaka anaweza panda miti hata 3000....imagine after yrs ana utajiri kias gani!
●Moral of the story wasibweteke tu huko mkifika vijijini... fursa kijijini had unadata..
 
Maisha ya mwanadam aliezaliwa na mwanamke ni mafupi na yamejaa misuko suko mingi pole sana chief
 
Kuna watu wanakaa kwa wakuu wa shule mpka sasa na washapata mshahara we unakwama wapi?
 
Back
Top Bottom