Napitia katika changamoto kubwa

bro Da'Vinci
 
haki ya Mungu ni mecheka. Si kwa hili jibu lako. Kwa hiyo hii bikira ina nifanya nakosa maamuzi mazuri. 😅😅
 
Hakuna limshindalo Mungu, wakati mwingine majaribu huja ili kututia nguvu, na kuna watu wamepitia makubwa kuliko wewe unayelilia ndoa. Kuna watu wana ndoa lakini wanatafuta mtoto mwaka wa 15+ na hawajapata, lakini Mungu aliyemkuu hujibu kwa wakati wake.
Tafakari na maandiko kutoka kitabu cha Ayubu 1:13-19
 
Asipokuelewa hapa basi, hasa hiyo namba 4 na 6.

Maandiko yanasema " Mungu hujibu kwa wakati wake (sio wako).

Waswahili wanasema "Ukiona kiza totoro ujue ndo kumekaribia kukucha".

Hakika umemshauri vyema.

Sent using Jamii Forums mobile app
Kumbe u mshauri mzuri, mi mbona hunishaurigi lakini?[emoji17]
 
Kama ni kwa ajili ya watu usisumbuke mana hutongozi bali unatongozwa wakikusema waambie wakuletee mume upo tayar
Ila kama ni maamuzi yako wanaume wapo wengi labda huyo umtakae ndo huwezi kumpata hadi unakufa kumbuka pia waeza olewa na mtoto usipate pia
 
Life is not fair at all, yaani kujitunza kote huko lakini bado unakosa wa kukuoa wakati makurumbembe yaloshindikana yanaolewa kila kukicha!

Pole mamy, usichoke kumtegemea Mungu yeye ni mweza wa yote. Usiharakie maisha kwa kuogopa maneno ya watu....ISHI UWEZAVYO, USIISHI WATAKAVYO!
 
Umri wako unaenda hapo utaishia kupata hao hao waume za watu na mwisho utafanyiwa kitu mbaya na wenye waume zao,na ukipata mwanaume asiye na mke atakuja kukupiga pesa na kusepa so take care utashangaa unazeeka tu kwa maelezo zaidi njoo PM
Wanampa moyo et umri bado.
yani aende leba na 40 siamini akisemacho huyo ni mchaguzi kama wachaguzi wengine ngoja Mungu amuonyeshe kua yeye hakosei
 
hapo kwenye nyekundu me nipo tayari naomba uwe mshenga wangu kwa huyu mrembo mkuu
 
N

Nashukuru ndugu. Niombee mpendwa maana huwa inafikia mpaka akosa cha kuomba wakati wa kusali.
Si kila muda unapoenda chumba cha faragha kuongea na Mungu wako lazima uombe dada. Kuna muda unahitaji kumsifu,kumwabudu Mungu na kumshukuru! Maana Mungu sio kwamba haoni unayoyapitia, anaona ila pengine muda wake bado na wakati wako haujafika! Na kikubwa omba mapenzi yake yatimizwe sio yako!!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nashukuru kwa mistari uliyonipa nimeipitia hapa na nitazidi kuisoma pake niombapo.asante sana.
Dad yangu biblia ni kitabu kigumu sana sio cha kutafsiri kirahisi kwa kusoma mstari mmoja au miwili.

Mimi nakushauri futa kabisa mawazo ya kuhama kanisa Katoliki kisa kuolewa. Pia jaribu kuwasiliana na chama cha kitume cha Karismatiki Katoliki katika parokia unayosali lazima kipo ili wakusaidie na kukuongoza katika kumuomba Mungu katika jambo hili.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…