Napitia katika changamoto kubwa

Napitia katika changamoto kubwa

Sasa hivi naona kama umri unaenda sana hivyo nahofia kukosa mtoto kabisa. Tatizo kubwa nililonalo ninapenda sana watoto na kwa sasa namhitaji kuliko ninavyoweza zungumza.
I understand your pain. Yupo mmoja alifanya kama wewe akaja kumpata mwanaume at 38 tena asiyeeleweka mpaka akaingia menopause. Mpaka kesho hana mume na hana mtoto.
 
Mungu anayo majibu ya maswali yako na shida zako.
Sisi hapa JF tunaongea kwa interest flan. Tafuta spiritual solution. U need to go deeper on God. All in all nakuombea,nna rafiki yangu ana issue kama yako...tulimwomba Mungu soon anaolewa.
 
Usillie Mungu amesikia kilio chako kanileta mimj niwe mkombozi wako..... Njoo pm mama come to papa
 
Aisee to be honest dada nineguswa na nyuzi yako hivyo nakuja pm kazi ni kwako

Mm sina rules wala nini
 
Sasa hivi naona kama umri unaenda sana hivyo nahofia kukosa mtoto kabisa. Tatizo kubwa nililonalo ninapenda sana watoto na kwa sasa namhitaji kuliko ninavyoweza zungumza.

Pole sana, kama ulichoeleza hapo juu ni sahihi (yaani hujatunga) nafahamu wakati unaopitia! Nimeshaona watu wa aina yako wanakuwa na wakati gani. Wakati naanza kazi kuna dada mmoja alikuwa na hali kama yako, ki ukweli kazi zilikuwa haiendi na alikuwa akiona mwanaume yuko single anahisi ndo Mungu kajibu ombi lake. Nakumbuka namna alivyoning'ang'ania lakini kila mara nikawa naishia kumpa moyo na kumshauri kwa sababu nisingeweza kufanya chochote kwake kwani alikuwa mkubwa kwangu na hakuwa aina ya ninayemuhitaji!
Kifupi nafahamu upweke ulionao kwa sababu nimeshawaona watu wa aina hiyo na mateso ya kisaikolojia na kihisia wanayo yapata!
Ushauri wangu kwako: Endelea kuvumilia tu na usijionyeshe saaana kwa watu (hasa wanawake ) kwamba unahitaji mwanaume kwa hali na mali! Vizuri umesoma naamini unajielewa na unaelewa madhara ya kuchukua maamuzi wa kukurupuka!

Tumia hekima iliyojaa uvumilivu kuhifadhi hisia zako kwa mwanaume hasa unapoongea na mwanamke mwenzio. Lakini unapokuwa na mwanaume, kama ni aina ya wanawake wenye maringo (maana wapo pia) jitahidi sana kuwachangamkia wanaume na akitokea wa kutaka kutoka na wewe, kwa vile shida yako kwa sasa ni mtoto na kukidhi hitaji lako la kihisia usikwepe kwepe sana!! kikubwa jihakikishie usalama wa afya yako kwanza...ukishapata mtoto faraja itakujaa tele na hutoona kama umepungukiwa chochote

Kwa ushauri zaidi waweza kuniona PM
 
Nashukuru kwa ushauri kaka angu. Wanadamu wanaweza kukupa jakamoyo. Na wazazi wangu japo hawajawahi niuliza direct lakini wanavyozungumuza mimi ni mtu mzima nawaelewa. Inafika sehemu nashidwa kabia. Na tatizo kubwa nililonalo ni kutojihusisha na mapenzi directly kitu ambacho wanaume wengi nashidwana nao hapo.

Wazazi na wanajamii wanaweza kukupa stress kweli, lakini ukiwa mtu unayejielewa haitakiwi kukusumbua maana watu wenye umri wako na hawajaolewa wapo wengi. Usikate tamaa, fanya yako ila kama kweli unatabia ya kupiga piga chenga au kauli tata kwa wanaume ni vema ukaziacha wanaume siku hizi hatupendi ussumbufu usikuwa na maana
 
Mungu anachukia Manung'uniko anataka tuombe bila kukoma. Uliomba kazi au mume,lakini uliomba kazi zaidi na Mungu amekupa kazi. Endelea kuomba mume zaidi utampata ufurahi.
 
Dada acha kukata tamaa,kuna wenye umri zaidi yako na bado wana matumaini.Mungu ni mwaminifu endelea kumwomba
 
  • Thanks
Reactions: Cyb
Habari za Jumapili wanajamii.

Mimi ni mwanamke mwenye umri wa miaka 32 kwa sasa. Napitia katika changamoto kubwa sana.

Hapo mwanzo kipindi ninasoma niliona si vyema kujiingiza katika mahusiano ya kufanya mapenzi kwani niliona yatanivuruga na ningejikuta napitia katika mahusiano mengi kitu ambacho sijawahi kukipanga maishani.

Nikamaliza chuo vizuri namshukuru Mungu.katika kutafuta ilikuwa ngumu kidogo nilitafuta mpaka nikakata tamaa nikaomba Mungu mpaka nikaona inatosha. Katikati ya kukata tamaa nikamuomba Mungu basi anipe kitu kimoja kwanza mme au kazi. Ila la kazi ndio nililoliwekea msisitizo kwani kwa kipindi hicho familia yangu ilikuwa inapitia changamoto nyingi kwa hiyo nikaona kazi itanisaidia kupunguza changamoto ama la basi niolewe ili nipunguze mzigo kwa familia yangu.

Siku isiyotarajiwa nikaitwa interview na nikapata kazi nzuri ambayo sikuwahi hata kufikiria wala kuiwaza. Nikashukuru Mungu na kuanza maisha mapya ya kazi na kusaidia familia yangu. Nikajikita kwenye kumuomba Mungu anijalie mme mwema atakayenifaa na kuongoza familia tutakayoipata katika misingi ya imani ta dini ya kikristo. Sikubagua kabila wala atakuwa mkirsto wa aina gani maadamu awe anaabudu jumapili maana mimi nilikuwa tiari kuhama katoliki ili tulee familia yetu tukiwa na muongozo wa dini moja.

Sikuwahi kudhani nitafikia huku maana mpaka sasa imekuwa ngumu kama ni Mungu hachelewi ama hawahi basi kwangu mimi kwa sasa imekuwa ni shida kubwa. Nimefunga novena nimesali sana mpaka naona nimeanza kuathirika na hili swala. Mwaka jana tarehe moja nikaona basi kama mme wangu hayupo nipate tu mwanamme nitakae zaa nae lakini awe mkirsto maana siko tiari kumtenga baba na mtoto wake hata kama hamhudumii, nikiamini kuwa uwezo wa kulea mwenyewe ninao hata kama watoto watakuwa zaidi ya mmoja niko tiari kupambana na maisha.

Nikaona kwa sababu nitakuwa pekeangu nikaanza kuwekeza ili watoto wangu wanikute nimejiandaa. Na penyewe Mungu akaona wakati wangu bado. Mwaka huu mwezi wa pili akatokea mme wa mtu kitu ambacho sijawahi hata fikiria kuwa kunasiku nitaangukia huko, Mwanzoni nilitaka tuzungumze mapema kabla hatujazoena sana matakwa yangu lakini akawa mtu wa kuona nampangia sheria mapema na kudai hizo mipango ninazotaka kupanga nae tukiwa hatujafika mbali ni mipango gani. Nikaona isiwe tabu.

Ikafika siku ya kukutana nikamwambia mimi sijawahi kabisa hakuamini na nikamwambia kama anajiamini aendelee ila ajue atakuwa na deni la kulipa, akatafakari akaona viatu ni vikubwa akaondoka.

Chenga zikaongezeka nikajiuliza ni nini shida, tukapanga tukutane ili tuone hatima ni nini kati yetu. Akaja na kudai yeye hayuko tiari kutoa bikira ya mtu asiye na mpango nae. nikamuelewa na nikaona yuko sahihi.Nikamuuliza wewe ulivyoanza ulitegemea mimi ni mti sina hisia za kufanya mapenzi akadai alijua anajihusisha na mapenzi ya kila mtu ana mtu wake hivyo wanakutana kulizishana tu. Akaniambia nahitaji nini hasa kwake nikamwambia kama ulishaona hisia zangu unadhani nahitaji nini? Niliona nisianze kutaja shida niliyonayo kwanza nimsikilize yeye ndio na mimi niseme ya kwangu. Yeye akadai aliona ni mahusiano ya kula na kuondoka. Akaniambia kama niko tiari ataweka sheria za kutuongoza za maandishi ili baadae tusijekupeana shida. Nikamwambia sheria zako utazoniwekea nitazifuata vilivyo japo najijua ninawivu lakini wewe ni mme wa mtu tiari nitavumilia.

Akaja na sheria na mipango mingi sana asee.sheria nyingi nilivyotafakari nikaona nyingi zinamlenga mtoto ambaye mimi ndio ninayemhitaji zaidi. na yeye akaona labda ni mmoja tu wakati mimi nishajipangia wakunitosha kabisa. Kwa maelezo yake nikaona hayuko tiari kuwa na mtoto nje ya familia na nikitokea kumpata basi nitoe mimba ama atamchukua. Nilichoka viungo vyote. Akaniuliza unalolote nikamwambia nizungumze nini wakati sheria zimekuwa ngumu.

Haki ya Mungu yaani natamani siku zirudi nyuma nizunguke na wanaume kama wafanyavyo wengine. Hukukujitunza kwangu kunanifanya nilie kila siku na kuomba Mungu usiku kucha kisa nilimtunzia mtu bikira. Jamii inayonizunguka itanitia wazimu maana swali la unaolewa lini limenichosha kabisa. Basi kama siolewi hata mtoto tu ni shida kumpata.

Kwasasa ninashida na mtoto kuliko maelezo na niendako nadhani nitawehuka. Msaada wenu tafadhalini sana.

NB. Hapo mwanzo nilifunga novena kwa muda wa mwaka mmoja na kuomba na kukabidhi mwili wangu uwe kwa ajili ya mtu mmoja tu ambaye ndio atakayekuwa mme au baba wa watoto wangu. Ndio maana inaniwia vigumu kuingia mahusiano mbalimbali.
Usipaniki kabisa,tulia na endelea kusali huku unakula vizuri,vaa vizuri na anza kutoka out na nenda kwenye baa,au klabu za hali ya juu.jitahidi kusavu pesa ununue gari yako na uwe unatoka,kila siku muombe mungu akukutanishe na mmeo na nakuhakikishia mmeo yu karibu mbele ya uso wako
 
Hivi kwani kuzaa watoto ni lazima??
Kuoa/ kuolewa ni lazima??
Miafrika inapenda kukopi kopi maisha ya ancestors wao bila kureason
 
Mind you, kuolewa na kuzaa ni majaaliwa ya Mwenyezi...kama kweli wewe ni muumini
 
Yanayokuletea matatizo ni haya:
1.Una haraka sana
2.Wewe ni social oriented,yaani unasikiliza watu na kutaka kutimiza matakwa yao,eti utaolewa lini!!
3.Huna akili,kwa mfano hujui jinsi ya kumpata mchumba yaani umekaa tu kama gogo unasubiri wanaume waje!!
 
Mimi niko desperate na kupata hela nyingi kwa kuwa hapa duniani kuna vitu viwili tu vinavyoweza kumpa mtu furaha ya kudumu:
1.Hela na
2.Upendo
 
Iv nao wanawake nao hupitia magumu kiasi hki!

Umepigana na ushindi wako haupo mbali wakati kama huu ndio MUNGU hutoa majibu yako ila kua makini!
 
Back
Top Bottom