Napinga sehemu ya malipo ya Lema...

Kwanini mnapenda kutunga kanuni pale CHADEMA inapokuwa imefanya vuizuri? mfano: kambi rasimi ya upinzani mlibadili kanuni, sasa lema kulipwa mafao mnataka kanuni zibadilike why? kwa taarifa yako kanuni zikibadilika za mafao zitawathili kuanzia wananchi wa kawaida hadi huko juu.

kuna viongozi fulani walianza muvu ya kuwa wakuu wa idara na wakurugenzi wa halmashauri wakiachishwa madaraka wanyang'anywe mishahara yao, wakasahau kuwa na wao wataathirika toka walipo jua hili hiyo move sijaisikia tena. why kanuni kwa ajili ya CHADEMA?
 
Kulipwa ni haki yake,tena ilipaswa na wale vizabizabina waswekwe lupango iwe fundisho.
 
Baada ya ushindi wa kesi yake nasikia Lema atalipwa mamilioni mengi sana , hela ambazo kama kweli angekuwa mzalendo ni either angezikataa kwa sababu sio vyema kulipwa bila kufanya kazi au angezitoa msaada kusaidia kitu chochote cha kuigusa jamii, lakini jamaa kazijaza mfukoni na wala hana mpango hata wa kuwanunulia walau mlo mmoja wale vijana wa mtaani walio mshangilia. Mkumbuke Zitto alizikataa kabisa hizi hela na mpaka leo hapokei posho yoyote. nadhani hii ndio sababu wenzake wanamchukia kwa sababu anaziba riziki.
Kumbe ubunge ni biahsra nzuri sana ngoja na mie niende bagamoyo nikagombee
 
wao wanamchafua mitandaoni yeye ZZK yuko busy kujijenga kwa wapiga kura....BABU PADRI SLAA kaazi kweli kweli
 
Huyo jamaa yako Mzitto anakataa fweza mchana,usiku anachukua!hapo hamna mtu!
 
No point hapo!!! U could rethink b4 ya kuandikia jamii statement kama hizi!! Hamna mahusiano ya chuki hapo kabisa!! Basi japo mwakani badirika come up na vitu vya kujenga

Sent from my BlackBerry 9900 using JamiiForums
 
VIKWAZO unataka upewe wewe? Mbona hupingi malipo ya mawaziri wakuu wastaafu, marais wastaafu n.k?
 
Last edited by a moderator:

wewe ni shabiki na utakuwa among masalia, ivi wajua mwandosya anakula salary na posho wkt hata ofisi hana na kazi hafanyi? ivi hujui kuwa kuna jamii ya watoto wengi uko arusha wanalipiwa ada na mh. Lema?Au waongea ili kuendeleza chokochoko mnazofundishwa na nnape?
 
Ndicho ninachopinga, malipo kama haya hapana kama yapo yaondolewe, watu walipwe mishahara yao tu

kwa nini unapinga sasa na haukupinga hapo awali, hii sio chokochoko tu sababu ni Lema na hasa kwa sababu yupo CDM? ili kufanukiwa kwa hoja yako fanya utafiti wa kina orodhesha wote waliolipwa fedha kama hizo ambazo unaziita sio halali na kutoa utoe thread kama hii ikiwataka hao wote warudishe hizo fedha wakiwemo Marais wastaafu, mawaziri wakuu wastaafu na walio jiuzuru kwani wanalipwa fedha kwa kazi ipi yenye tija na taifa hili.
 
ungehoji kama kuna malipo alipokea akiwa kasimamishwa ubunge ningekuona wamaana.

Ila kwa hili halina haja, mana baada ya kuonekana hana hatia katika kesi yake,inabidi apewe pesa yake aliyokuwa akipatiwa kabla ya kusimamishwa.

Jiulize
 
Atalipwa mbona katibu mkuu nishati bado analipwa adi kesho, je pesa za EPA zilizo ibwa BOT siyo sawa na hizo hela kamuulize CHENGE Endrew atakwambia hizo hela ata akienda nazo BILILA SERENGETI hawezi akaspend ata siku mbili coz kwake its unsuficient amount milioni 85 kwa mafisadi papa hapa tz hiyo ni hela ndogo sn au umesahau MANJI aliwai kutoa milioni 100 ili washabiki waingie uwanja wa CCM KIRUMBA umesahau? je izo hela kwann uczipangie matumizi hayo ulosema hapo na je ktk toleo maalum kuhusu matajiri wa tz uliona wanamiliki kiasi gani MWACHE LEMA coz nyie nyinyiem ndo memsumbua kipindi hicho chote kwani LEMA pamoja na kukaa nje ya ubunge si sawa na wabunge wengne wanaolala bungeni km TYSON so leave LEMA ALONE AS HE IS and die quitely with your low level of comparative analysis based on your narrow minds.
 
Kama Lema asingekata rufaa na kuamua kurudia uchaguzi na kushinda hapo asingekuwa na haki za kulipwa,lkn kakata rufaa hapo ni zengwe la kawaida tu hvyo ana haki za msingi kulipwa,
 
Hawa masalia na magamba wameungana ili kuiyumbishaCDM,kwasababu anayelipwa ni LEMA imekua tatizo.
 
Hawa masalia na magamba wameungana ili kuiyumbishaCDM,kwasababu anayelipwa ni LEMA imekua tatizo.

Mleta mada ni gamba chakavu. Hajui hizo kanuni zanaaply hata kwa wafanyakazi wa kawaida wanapokata rufaa dhidi ya kesi ya waajirii waahenzi kama liccm.
 

Binafsi naguswa na huu moyo wa kuumizwa na matumizi yasiyo stahiki ya kodi za wananchi. Hata hivyo ni vema ikakumbukwa kuwa tunachoongelea hapa ni

1.Lema alikuwa mbunge halali kwa KUCHAGULIWA na KWA RIDHAA YA WANANCHI WA JIMBO LAKE. Kwa hiyo kitendo kilichofanywa cha kuitoa mahakama nje ya utaratibu na kulazimisha hukumu, kilimnyang'anya haki yake ya kisheria ya kuwawakilisha wananchi kupitia KODI hizo na mengineyo.

2.Matakwa ya sheria yanakubaliana na uhalali wa ubunge wa Lema ndiyo maana baada ya kureview hukumu wameona bado ana haki hiyo.

Kwa hiyo:
Kwa kuwa Lema alichaguliwa kwa kura halali kuwa Mbunge, na kwa kuwa uamuzi wa kumsimamisha haukuwa wa haki, na kwa kuwa hukumu ya rufaa imemrudisha tena Kuwa mbunge, Hii nisawa na kusema: kwa mujibu wa sheria Lema alikuwa MBUNGE HALALI TANGU KUCHAGULIWA MPAKA SASA NA MPAKA WANANCHI WATAKAPOAMUA VINGINEVYO.
Kutokana na hilo Lema anastahili kila posho aliyotakiwa kupata akiwa mbunge HALALI kwa sababu hakuomba kusimamaishwa wala hakuwa na Matatizo ya kiutendaji. Kama kuna lawama za matumizi mabaya ya Kodi yanaweza kuelekezwa kunakostahili uchunguzi ufanywe, ipatikane SABABU ya kusimamishwa Lema at first place. Huyo aliyepika hilo ndo ALAUMIWE KWA UFUJAJI WA KODI ZA WANANCHI. Vinginevyo Lema, Kwa mujibu wa taratibu anatakiwa ALIPWE STAHILI YAKE KWANZA halafu, kama itaonekana sheria zinahalalisha ufujaji wa KODI kwa maana hiyo, ZIFANYIWE MAREKEBISHO ili kesho lisirudie hilo.

Kwa upande wa pili ikumbukwe kuwa Lema kama Binadamu, Mtanzania, Mwanamageuzi na Mzalendo, ana maoni na utashi wake. Hivyo badala ya kuanzisha mijadala kama hii tumpe nafasi ya kuamua anataka nini. Naamini atakuja na uamuzi wa busara kama ambavyo amekuwa anafanya. Nina imani kuwa Matumizi ya pesa hizo (KAMA ATALIPWA) yatakuwa kwa manufaa ya wanachi bado na HAITAKUWA HASARA KWA VYOVYOTE KUCHUKUA FEDHA KWENYE MFUKO WAKO WA KUSHOTO KWENDA WA KULIA........Hivi Ndivyo nionavyo mimi:smiling:
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…