Ndugu Vikwazo;
Kuna mambo mawili nayaona hapa;
1: Hoja ya kwanza ni ukaidi na maslahi ya CCM na serikali yake, kwamba CDM walipendekeza kutazamwa upya kwa sheria na kanuni zinazoruhusu posho kwa mfumo mzima wa serikali. Lakini bwana Vikwazo utakubali au kukumbuka jinsi wabunge wa CCM walivyo badili mada na kuwageuzia wabunge wa CDM kuwa wanafiki na kila neno la kuwabeza lakini haya ndio madhara yake. Na sio hilo tu hata MISHAHARA ya watumishi wa serikali na idara nyingi inatofautiana sana. Kwa mfano TCRA iliyo chini ya wizara ya Mawasiliano wana salary scale zao, TRA pia hivyo hivyo. Hata posho zao pia zinatofautiana sana. Nakubaliana na wewe kuwa sheria hizi ni mbovu.
2: La pili ni kuwa Lema hawezi kuwa kondoo wa kafara, anapaswa kulipwa stahiki zake zote, tujifundishe hapa sasa. Lakini naona swala moja, kama tunakubali alipwe mishahara yake kwa nini tunakataa posho zingine asilipwe!? Sioni sababu ya kumlipa mishahara yake afu tumkatalie. Hakulipwa mshahara kwa miezi 8 kwa kuwa hakuwa mbunge, ndio sababu hiyo hiyo hakupewa posho ya vikao, mafuta, na hela ya jimbo. Kama anapewa mishahara yake basi imebainika bila shaka kwamba Mahakama Kuu ilifanya makosa hivyo Lema alikua "forced" kuachia ubunge wake hakufanya kwa hiari yake. Basi haikua hiari yake asitekeleze majukumu yake ya kibunge (POSHO), kufanya shughuli za jimbo (MAFUTA na HELA YA JIMBO).
Lakini pia Lema mwenyewe amesema kama milion 60 hivi sio 80 na Katibu wa Bunge, Ndg Kashilila kasema pia wataangalia aina ya mafao/stahiki za kumpa.
ANGALIZO; Siasa na vyama vipo na vitapita tuweke mbele MASLAHI ya TAIFA, hoja ya msingi hata ikiletwa na wabunge wa upinzani ishughulikiwe kwa umakini sio sasa mambo yanavyokwenda CCM against CDM. Tazama hata hoja ya Katiba.
Shukurani sana mkuu kwa uchanganuzi wako.
Hoja ya kukataa asilipwe posho na kukubali alipwe mshahara imekaa kama ifuatavyo
Mshahara wa mtu ni kwa matumizi yake, hakuna hata auditing inayotakiwa kwenye mshahara wa mtu yaani matumizi yake.
Tuje kwenye posho, kuna posho za safari, mafunzo, etc etc
Mfano sio sahihi kumlipa mtu posho ya mafunzo wakati hakuudhuria semina wala mafunzo yoyote, au kumlipa posho ya safari bila kufanya safari ya kikazi.
Narudi kwa kesi ya lema, lema alitakiwa kupokea mshahara [ no debate about that] lakini pia angelipwa posho ya mafuta kwa safari zake jimboni wakati anahudumia jimbo [ regea posho za mafunzo nilivyofafanua hapo juu ] yaani awezi kulipwa posho ya mafuta kwa sababu akuendesha gari kama mbunge, hakufanya shughuli hiyo, hiyo shughuli ilisimama kwa wakati,
Naomba ieleweke kwamba hii posho ina matumizi yake legwa yaani mafuta ya gari, hicho kitu akikufanyika, atuwezi kuwa na sheria ambazo azina common sense, sense ya kumlipa lema ni kama angekuwa na shughuli ya kibunge kwa hiyo miezi sita,
Kuna wanao justify haya malipo kwa kusema kwamba kuna wabunge wanalipwa lakini awaendi majimboni mwao, hata hiyo nasema sio sahahi,
Strategic yangu inaweza isikubalike but attacking ni part ya forcing strategic, sisi kama wananchi tumesema sana kuhusu matumizi mabovu lakini hii hali bado inaendelea tu, sasa inatosha tutadili na mtu mmoja mmoja anayejulikana kupokea haya malipo HALAMU