Napinga sehemu ya malipo ya Lema...

Napinga sehemu ya malipo ya Lema...

Je Lema alijisimamisha ubunge au alisimamishwa? Kwa kuwa alisimamishwa na hakujisimamisha akipatikana hana hatia analipwa stahiki zake zote!
Ni kama mshitakiwa alieshutumiwa kesi,akapambana kwa muda mrefu baadae akaja kushinda....kisha akadai fidia za malipo aliyokuwa anaingiza kwa siku...nadhani hapa utaibuka na kusema kila siku ulikuwa unashinda mahakamani ulipwe hela ya nini? Ndio unanyotaka kusema hapa...
Kwa utaratibu huo basi serikali inaweza kuwa inawafungulia kesi na kuwapotezea muda wabunge wa upinzani ili wasiwalipe!
Sidhani kama ulijipa muda wa kutosha kabla ya kupost hili.....makosa ya kisheria yanagharama na gharama ndio hizi...kuna raha ukishinda 2!
 
Baada ya ushindi wa kesi yake nasikia Lema atalipwa mamilioni mengi sana , hela ambazo kama kweli angekuwa mzalendo ni either angezikataa kwa sababu sio vyema kulipwa bila kufanya kazi au angezitoa msaada kusaidia kitu chochote cha kuigusa jamii, lakini jamaa kazijaza mfukoni na wala hana mpango hata wa kuwanunulia walau mlo mmoja wale vijana wa mtaani walio mshangilia. Mkumbuke Zitto alizikataa kabisa hizi hela na mpaka leo hapokei posho yoyote. nadhani hii ndio sababu wenzake wanamchukia kwa sababu anaziba riziki.
Kumbe ubunge ni biahsra nzuri sana ngoja na mie niende bagamoyo nikagombee

Ndugu Farida,
Sidhani kama Lema ameshalipwa hizo pesa tayari, wala sidhani kama hata imeshaamuliwa atalipwaje. Pia haiko wazi kama atakubali au kukataa kulipwa au kama akikubali atafanyia nini hizo pesa.

Ushauri wangu:
Tuache kumsemea. tusubiri aseme kwanza ndiyo tuhukumu. Tuangalie kama atachukua hayo malipo atayapeleka wapi. I am confident atayatumia VIZURI kuliko mtakavyotegemea.
 
Kwa hiyo Lema kapata Excuse kuchukuwa hizo pesa ambazo ajazifanyia kazi.

Mkuu unamaanisha nini kusema lema kapata excuse? Ina maana hana haki kurudishiwa stahiki zake?je aliacha mwenyewe majukumu yake au aliachishwa?je time value for money imekuwa considered?kisheria lema ana stahiki kupata hats icho kilichotajwa. Sheria mbovu za taifa letu na serikali yetu ndo zinazofuatwa wala si excuse ndugu.
 
Kwa hiyo Lema kapata Excuse kuchukuwa hizo pesa ambazo ajazifanyia kazi.

Kumhenyesha na kesi mlikomhenyesha mimi naona mlijua kuwa mtaishia kumlipa, msiwasahau mliowatumia kufungua kesi nao muwalipe baada ya kulipa gharama za kesi
 
Kwanza salamu, pia niwatakie heri ya Christmas na mwaka mpya.

Hoja ya msingi ni
MALIPO YA LEMA YANAONYESHA UDHAIFU WA MFUMO WETU.

Lema atalipwa milion 85 Tsh/= kama malimbikizo kwa kusimamishwa baada ya kusimamishwa ubunge,
( kwa mchanganuo zaidi soma hapa
Lema kuzoa Sh85 Milioni - Siasa - mwananchi.co.tz )
kama mwananchi nina tatizo na Lema kulipwa hiyo pesa, sioni Value for money kwa sisi kuwa na mfumo dhaifu kiasi hicho.

Tatizo nililonalo Lema kulipwa hiyo pesa ni maeneo yafuatayo:

1.) Milion 20 za mafuta kama Mbunge, Lema aliposimamishwa ubunge shughuli zake zilikoma, hivyo matumizi ya mafuta kwa shughuli za kibunge yalikoma pia!!! kwangu mimi kumlipa Mbunge Milion 20 za mafuta bila kuwa kazini au kufanya kazi ni kudhurumu wananchi, huu ni mfumo onevu, hiyo pesa haipashwi kulipwa,
kwa maelezo zaidi ni kwamba Lema atarudishiwa ghalama za kesi, ni ghalama zipi hizo? hakuna nauli alizokuwa anatumia? na kama ndio balance ipo itakuwaje tukimlipa tena kama umma pesa ya mafuta?
lakini Je Lema kwa wakati huo alikuwa anafanya shughuli zipi? sio M4C ( i embrace M4C but TAIFA kwanza) huko akulipwa chochote?

2.) posho ya jimbo Sh40 milioni ....... jimbo lipi hali kazi ilisimamishwa? jimbo la Arusha alikuwa na mbunge kwa wakati wote wa kesi? lema akufanya shughuli za kibunge jimboni mwake.
Lakini pia kwa kwenda mbali ni kwamba Lema alikuwa na shughuli maalumu ya chama yaani M4C ( no problems) lakini je hapa kuna tofauti gani na wale wafanyakazi hewa? mtu ayupo kwenye kituo cha kazi analipwa tu? hivi sisi tunalipa majina au shughuli/kazi ya mtu? where is the value for my TAX?

3.) Posho nyingine Sh6.6 milioni Kwa kazi ipi analipwa posho? ubunge ulikoma nimeshaeleza hapo juu, ofisi ya mbunge haikuwa na kazi tena kwa kukosa mbunge, na kama ilikuwepo na ina fanya kazi vipi amri ya mahakama kusimamisha ubunge wa Lema, kwa misingi hiyo nina amini hakukuwa na shughuli ya sisi kama taifa kulipa posho.

<<<<<<
Nakubaliana kwamba Lema alipwe malimbikizo ya mshahara wake yanafikia Sh18.4 milion, hii ni haki pekee kwa Lema, sikupaliana kwamba kama mtu umesimamishwa wazifa wako basi umma uendelee kukulipa pesa bila kuutumikia.

CHOMBEZO

HITIMISHO:
Hoja yangu ni tuwe na kanuni zenye macho, zinazothamini kodi yetu, malipo lazima yenye thamani ya kazi, malipo holela ni hatari kwa taifa, napinda haya malipo regardless nani anapewa, msingi ni kuwa na taifa imala lenye uchumi unaonufaisha wote.

Kama kuna sheria zinatoa mwanya huu zifutwe mara moja ili kuongeza thamani ya pesa yetu katika matumizi (VALUE FOR MONEY)

Binafsi naguswa na huu moyo wa kuumizwa na matumizi yasiyo stahiki ya kodi za wananchi. Hata hivyo ni vema ikakumbukwa kuwa tunachoongelea hapa ni

1.Lema alikuwa mbunge halali kwa KUCHAGULIWA na KWA RIDHAA YA WANANCHI WA JIMBO LAKE. Kwa hiyo kitendo kilichofanywa cha kuitoa mahakama nje ya utaratibu na kulazimisha hukumu, kilimnyang'anya haki yake ya kisheria ya kuwawakilisha wananchi kupitia KODI hizo na mengineyo.

2.Matakwa ya sheria yanakubaliana na uhalali wa ubunge wa Lema ndiyo maana baada ya kureview hukumu wameona bado ana haki hiyo.

Kwa hiyo:
Kwa kuwa Lema alichaguliwa kwa kura halali kuwa Mbunge, na kwa kuwa uamuzi wa kumsimamisha haukuwa wa haki, na kwa kuwa hukumu ya rufaa imemrudisha tena Kuwa mbunge, Hii ni sawa na kusema: kwa mujibu wa sheria Lema alikuwa MBUNGE HALALI TANGU KUCHAGULIWA MPAKA SASA NA MPAKA WANANCHI WATAKAPOAMUA VINGINEVYO.
Kutokana na hilo Lema anastahili kila posho aliyotakiwa kupata akiwa mbunge HALALI kwa sababu hakuomba kusimamaishwa wala hakuwa na Matatizo ya kiutendaji. Kama kuna lawama za matumizi mabaya ya Kodi yanaweza kuelekezwa kunakostahili uchunguzi ufanywe, ipatikane SABABU ya kusimamishwa Lema at first place. Huyo aliyepika hilo ndo ALAUMIWE KWA UFUJAJI WA KODI ZA WANANCHI. Vinginevyo Lema, Kwa mujibu wa taratibu anatakiwa ALIPWE STAHILI YAKE KWANZA halafu, kama itaonekana sheria zinahalalisha ufujaji wa KODI kwa maana hiyo ZIFANYIWE MAREKEBISHO ili kesho lisirudie hilo.

Kwa upande wa pili ikumbukwe kuwa Lema kama Binadamu, Mtanzania, Mwanamageuzi na Mzalendo, ana maoni na utashi wake. Hivyo badala ya kuanzisha mijadala kama hii tumpe nafasi ya kuamua anataka nini. Naamini atakuja na uamuzi wa busara kama ambavyo amekuwa anafanya. Nina imani kuwa Matumizi ya pesa hizo (KAMA ATALIPWA) yatakuwa kwa manufaa ya wanachi bado na HAITAKUWA HASARA KWA VYOVYOTE KUCHUKUA FEDHA KWENYE MFUKO WAKO WA KUSHOTO KWENDA WA KULIA........Hivi Ndivyo nionavyo mimi:smiling:
 
Kumfungulia/kumbambikia kesi Lema kwako wewe ni sawa, kumlipa haki za kumbambikia kesi ni noma; hamuelewiki. Si serikali yenu choteni po pote mumlipe. Muwashauri CCM waache michezo kama hii bila kujipanga na gharama zitokanazo.
 
hoja yako ina mashiko ingawa ni tatizo la mfumo
na inawezeka baadhi ya vitu vikafanyika mfano mafuta kwa sababu alishindwa kutembelea maeneo yake kama mbunge hivyo inabidi atembee huko kwa nguvu zote yaani asubuhi mchana na jioni ni zaidi ya yale mafuta ya kawaida ambayo angetumia kwa mwezi
posho ya jimbo ile mara nyingi hutumika kwa shughuli za jimbo kwa sababu lema alisimashwa na shughuli hizo zilisimama hivyo itabidi alipwe ili shughuli ziendelee
 
Mawaziri wakuu wote vwastaafu wanalipwa 70% ya mshahara wa aziri mkuu aliyeko madarakani,hebu tuwahesabu mmoja mmoja.
1.Edward lowassa
2.Fredrick Sumaye
3.Joseph warioba
4 .Salim Ahmed
5.Cleopa Msuya
6.Sam Malechela.
Hawa wana tija gani kwa nchii hii?Kwani hawakulipwa mafao yao baada ya kuitumia nchi hii?Lyatonga nae nilimsikia bungeni akilalama nae alipwe,serikali imemtupa.Sioni shida Lema akilipwa,acha na yeye ale kidogo mbona wengine wanakula bila hata kunawa mikono?
 
Mawaziri wakuu wote wastaafu wanalipwa 70% ya mshahara wa waziri mkuu aliyeko madarakani,hebu tuwahesabu mmoja mmoja,kisha piga hesabu ni pesa ngapi inapotea kila mwezi.
1.Edward lowassa
2.Fredrick Sumaye
3.Joseph warioba
4 .Salim Ahmed
5.Cleopa Msuya
6.Sam Malechela.
Hawa wana tija gani kwa nchii hii?Kwani hawakulipwa mafao yao baada ya kuitumia nchi hii?Lyatonga nae nilimsikia bungeni akilalama nae alipwe,serikali imemtupa.Sioni shida Lema akilipwa,acha na yeye ale kidogo mbona wengine wanakula bila hata kunawa mikono?
 
Shukurani sana mkuu kwa uchanganuzi wako.
Hoja ya kukataa asilipwe posho na kukubali alipwe mshahara imekaa kama ifuatavyo
Mshahara wa mtu ni kwa matumizi yake, hakuna hata auditing inayotakiwa kwenye mshahara wa mtu yaani matumizi yake.

Tuje kwenye posho, kuna posho za safari, mafunzo, etc etc
Mfano sio sahihi kumlipa mtu posho ya mafunzo wakati hakuudhuria semina wala mafunzo yoyote, au kumlipa posho ya safari bila kufanya safari ya kikazi.

Narudi kwa kesi ya lema, lema alitakiwa kupokea mshahara [ no debate about that] lakini pia angelipwa posho ya mafuta kwa safari zake jimboni wakati anahudumia jimbo [ regea posho za mafunzo nilivyofafanua hapo juu ] yaani awezi kulipwa posho ya mafuta kwa sababu akuendesha gari kama mbunge, hakufanya shughuli hiyo, hiyo shughuli ilisimama kwa wakati,
Naomba ieleweke kwamba hii posho ina matumizi yake legwa yaani mafuta ya gari, hicho kitu akikufanyika, atuwezi kuwa na sheria ambazo azina common sense, sense ya kumlipa lema ni kama angekuwa na shughuli ya kibunge kwa hiyo miezi sita,

Kuna wanao justify haya malipo kwa kusema kwamba kuna wabunge wanalipwa lakini awaendi majimboni mwao, hata hiyo nasema sio sahahi,
Strategic yangu inaweza isikubalike but attacking ni part ya forcing strategic, sisi kama wananchi tumesema sana kuhusu matumizi mabovu lakini hii hali bado inaendelea tu, sasa inatosha tutadili na mtu mmoja mmoja anayejulikana kupokea haya malipo HALAMU

Mkuu,unachosema kuhusu posho ni sahihi kabisa,but ni hao hao wabunge wa chadema ndiyo walizipigia kelele wakaonekana mataahira,na sisi wananchi badala ya kuwasaidia nasi tukawaona walewale Chadema waropokaji,sasa nini?waache wazile kutokana na umbumbumbu wetu,na siyo hizo,wengine wanalipwa malipo ya uwaziri na ubunge,hulioni hilo?yako mengi na waache wale tuu!kuleni waheshimiwa sisi waTanzania ni MAZOMBI.
 
yaani post km hii haistahili comment hata moja maana it's extremely upuuzi, nategemea tujadili ideas ambazo zitatusaidia kudhibiti incompetent judges in this country to make absurd decisions km ktk kesi ya lema
 
Kwanza salamu, pia niwatakie heri ya Christmas na mwaka mpya.

Hoja ya msingi ni
MALIPO YA LEMA YANAONYESHA UDHAIFU WA MFUMO WETU.

Lema atalipwa milion 85 Tsh/= kama malimbikizo kwa kusimamishwa baada ya kusimamishwa ubunge,
( kwa mchanganuo zaidi soma hapa
Lema kuzoa Sh85 Milioni - Siasa - mwananchi.co.tz )
kama mwananchi nina tatizo na Lema kulipwa hiyo pesa, sioni Value for money kwa sisi kuwa na mfumo dhaifu kiasi hicho.

Tatizo nililonalo Lema kulipwa hiyo pesa ni maeneo yafuatayo:

1.) Milion 20 za mafuta kama Mbunge, Lema aliposimamishwa ubunge shughuli zake zilikoma, hivyo matumizi ya mafuta kwa shughuli za kibunge yalikoma pia!!! kwangu mimi kumlipa Mbunge Milion 20 za mafuta bila kuwa kazini au kufanya kazi ni kudhurumu wananchi, huu ni mfumo onevu, hiyo pesa haipashwi kulipwa,
kwa maelezo zaidi ni kwamba Lema atarudishiwa ghalama za kesi, ni ghalama zipi hizo? hakuna nauli alizokuwa anatumia? na kama ndio balance ipo itakuwaje tukimlipa tena kama umma pesa ya mafuta?
lakini Je Lema kwa wakati huo alikuwa anafanya shughuli zipi? sio M4C ( i embrace M4C but TAIFA kwanza) huko akulipwa chochote?

2.) posho ya jimbo Sh40 milioni ....... jimbo lipi hali kazi ilisimamishwa? jimbo la Arusha alikuwa na mbunge kwa wakati wote wa kesi? lema akufanya shughuli za kibunge jimboni mwake.
Lakini pia kwa kwenda mbali ni kwamba Lema alikuwa na shughuli maalumu ya chama yaani M4C ( no problems) lakini je hapa kuna tofauti gani na wale wafanyakazi hewa? mtu ayupo kwenye kituo cha kazi analipwa tu? hivi sisi tunalipa majina au shughuli/kazi ya mtu? where is the value for my TAX?

3.) Posho nyingine Sh6.6 milioni Kwa kazi ipi analipwa posho? ubunge ulikoma nimeshaeleza hapo juu, ofisi ya mbunge haikuwa na kazi tena kwa kukosa mbunge, na kama ilikuwepo na ina fanya kazi vipi amri ya mahakama kusimamisha ubunge wa Lema, kwa misingi hiyo nina amini hakukuwa na shughuli ya sisi kama taifa kulipa posho.

<<<<<<
Nakubaliana kwamba Lema alipwe malimbikizo ya mshahara wake yanafikia Sh18.4 milion, hii ni haki pekee kwa Lema, sikupaliana kwamba kama mtu umesimamishwa wazifa wako basi umma uendelee kukulipa pesa bila kuutumikia.

CHOMBEZO

HITIMISHO:
Hoja yangu ni tuwe na kanuni zenye macho, zinazothamini kodi yetu, malipo lazima yenye thamani ya kazi, malipo holela ni hatari kwa taifa, napinda haya malipo regardless nani anapewa, msingi ni kuwa na taifa imala lenye uchumi unaonufaisha wote.

Kama kuna sheria zinatoa mwanya huu zifutwe mara moja ili kuongeza thamani ya pesa yetu katika matumizi (VALUE FOR MONEY)

Akina wasira wanao lala na kukoloma bungeni mbona wanalipwa
 
Nenda mahakamani.. Ndo mahali pekee haki inapatikana! Ukianza na Dowans kulipwa!
 
Kwanini mnapenda kutunga kanuni pale CHADEMA inapokuwa imefanya vuizuri? mfano: kambi rasimi ya upinzani mlibadili kanuni, sasa lema kulipwa mafao mnataka kanuni zibadilike why? kwa taarifa yako kanuni zikibadilika za mafao zitawathili kuanzia wananchi wa kawaida hadi huko juu.

kuna viongozi fulani walianza muvu ya kuwa wakuu wa idara na wakurugenzi wa halmashauri wakiachishwa madaraka wanyang'anywe mishahara yao, wakasahau kuwa na wao wataathirika toka walipo jua hili hiyo move sijaisikia tena. why kanuni kwa ajili ya CHADEMA?

Kina nani wanapenda kutunga hizo kanuni? sitegemei kupata response za kiCCM ya kwamba kila anayepinga kitu ni mpinzani, hivi hii nchi haina RAIA wenye uchungu nayo, tusipeane vyama

Kulipwa ni haki yake,tena ilipaswa na wale vizabizabina waswekwe lupango iwe fundisho.
Hii ni kanuni mpya au ni kutojua kwangu,
anyway hiyo sio sehemu ya hoja yangu, siasa pembeni ndani ya hii hoja

Baada ya ushindi wa kesi yake nasikia Lema atalipwa mamilioni mengi sana , hela ambazo kama kweli angekuwa mzalendo ni either angezikataa kwa sababu sio vyema kulipwa bila kufanya kazi au angezitoa msaada kusaidia kitu chochote cha kuigusa jamii, lakini jamaa kazijaza mfukoni na wala hana mpango hata wa kuwanunulia walau mlo mmoja wale vijana wa mtaani walio mshangilia. Mkumbuke Zitto alizikataa kabisa hizi hela na mpaka leo hapokei posho yoyote. nadhani hii ndio sababu wenzake wanamchukia kwa sababu anaziba riziki.
Kumbe ubunge ni biahsra nzuri sana ngoja na mie niende bagamoyo nikagombee

Naomba kwa kukazi kwa kusema POSHO za MAFUTA na JIMBO zilizilipwa, apewe mshahara tu

njaa na ujinga ni kitu kimoja
You right, Taifa limeja njaa kwa mifumo kama hii, sasa lazima tu protest kwa matumizi ya kodi zetu

View attachment 76779wao wanamchafua mitandaoni yeye ZZK yuko busy kujijenga kwa wapiga kura....BABU PADRI SLAA kaazi kweli kweli

No politics please, hii ni issue nyeti kwa ustawi wa jamii
 
Akina wasira wanao lala na kukoloma bungeni mbona wanalipwa

Kwa hiyo ume support hoja, ya kwamba Lema ni sawa na hao kina wasira walilala na kulipwa, kwa haki wote wasilipwe
HONEST IS A BEST POLICY IN MY HEAD
 
Nenda mahakamani.. Ndo mahali pekee haki inapatikana! Ukianza na Dowans kulipwa!
Hivi TANESCO hawana kesi ya zidi ya DOWANS mahakamani?
na kama haya malipo ni sawa na ya DOWANS as the referring it, let me start with this one
 
yaani post km hii haistahili comment hata moja maana it's extremely upuuzi, nategemea tujadili ideas ambazo zitatusaidia kudhibiti incompetent judges in this country to make absurd decisions km ktk kesi ya lema

Yet you did comment, ....... walk your talk mate
 
Binafsi naguswa na huu moyo wa kuumizwa na matumizi yasiyo stahiki ya kodi za wananchi. Hata hivyo ni vema ikakumbukwa kuwa tunachoongelea hapa ni

1.Lema alikuwa mbunge halali kwa KUCHAGULIWA na KWA RIDHAA YA WANANCHI WA JIMBO LAKE. Kwa hiyo kitendo kilichofanywa cha kuitoa mahakama nje ya utaratibu na kulazimisha hukumu, kilimnyang'anya haki yake ya kisheria ya kuwawakilisha wananchi kupitia KODI hizo na mengineyo.

2.Matakwa ya sheria yanakubaliana na uhalali wa ubunge wa Lema ndiyo maana baada ya kureview hukumu wameona bado ana haki hiyo.

Kwa hiyo:
Kwa kuwa Lema alichaguliwa kwa kura halali kuwa Mbunge, na kwa kuwa uamuzi wa kumsimamisha haukuwa wa haki, na kwa kuwa hukumu ya rufaa imemrudisha tena Kuwa mbunge, Hii ni sawa na kusema: kwa mujibu wa sheria Lema alikuwa MBUNGE HALALI TANGU KUCHAGULIWA MPAKA SASA NA MPAKA WANANCHI WATAKAPOAMUA VINGINEVYO.
Kutokana na hilo Lema anastahili kila posho aliyotakiwa kupata akiwa mbunge HALALI kwa sababu hakuomba kusimamaishwa wala hakuwa na Matatizo ya kiutendaji. Kama kuna lawama za matumizi mabaya ya Kodi yanaweza kuelekezwa kunakostahili uchunguzi ufanywe, ipatikane SABABU ya kusimamishwa Lema at first place. Huyo aliyepika hilo ndo ALAUMIWE KWA UFUJAJI WA KODI ZA WANANCHI. Vinginevyo Lema, Kwa mujibu wa taratibu anatakiwa ALIPWE STAHILI YAKE KWANZA halafu, kama itaonekana sheria zinahalalisha ufujaji wa KODI kwa maana hiyo ZIFANYIWE MAREKEBISHO ili kesho lisirudie hilo.

Kwa upande wa pili ikumbukwe kuwa Lema kama Binadamu, Mtanzania, Mwanamageuzi na Mzalendo, ana maoni na utashi wake. Hivyo badala ya kuanzisha mijadala kama hii tumpe nafasi ya kuamua anataka nini. Naamini atakuja na uamuzi wa busara kama ambavyo amekuwa anafanya. Nina imani kuwa Matumizi ya pesa hizo (KAMA ATALIPWA) yatakuwa kwa manufaa ya wanachi bado na HAITAKUWA HASARA KWA VYOVYOTE KUCHUKUA FEDHA KWENYE MFUKO WAKO WA KUSHOTO KWENDA WA KULIA........Hivi Ndivyo nionavyo mimi:smiling:

As a patriotic RED is the only line i do care, kushinda au kusimamishwa ubunge lema kuna matokeo, moja ya matokeo yake ni permanent mfano kupoteza miezi minane ya kulitumikia jimbo lake, atuwezi kusema uchaguzi wa Arusha ufanyika May 2016 kwa sababu mbunge alipoteza miezi nane, hiyo ni un-reversibly condition, pia kwenye record itajulika hivyo kwamba Lema aliwahi kusimamishwa,
Lema analipwa kulingana na sheria za kazi kama watu wengine na si kutokana na kazi yake bali kutokana na haki zake kama wananchi wengine, ya kwamba shughuli ya ubunge ni sehemu ya kipato chake na kilisimamishwa, hivyo basi mshahara wake ni haki kwa sababu ni matumizi yake.
Sasa naomba nijibu swali hili kwa makini JE POSHO za Mafuta wabunge wanapewa kwa shughuli gani? na Posho za Jimbo Je? je lema aliendesha gari kufanya hizo shughuli miezi nane iliyopita?
 
Wanasiasa bana linapokuja swala la mahela wote ni wale wale tu
Hapa Lema na washirika wake watatetea ni sheria zilizopo zina mpa haki na anakubaliana nazo sababu ni mahela.............lakini labda ikija swala la kulipwa Richmond japo lipo kisheria katu hata kuelewa sbabu tu halimuhusu yeye.
 
Mbaya zaidi watu wanaleta vyama, eti nimetumwa hivi hii post kuna ccm anayeishabikia? ninawezaje kutumwa na ccm ambao wameweka hizi sheria mbovu? yaani sawa na ccm kujishitaki wenyewe!!!!!!
Hii bora ina mazala makubwa kwa ccm kuliko chadema maana lema anawezakufanya action ya kizalendo na kuiumbua serikali na chama.

Tatizo la nchi yetu ni vyama, tumegawanyika sana kwa vyama kiasi kwamba kila mwenye hoja lazima apewe chama cha siasa, kuna watu wanataka tuamini kwamba hakuna tena maoni huru nchini kutokana na wao kubeba vyama mgongoni mwao
 
Back
Top Bottom